Nichukue pikipiki gani kati ya hizi tatu?

Joined
Jul 8, 2017
Posts
86
Reaction score
73
Wakuu, baada ya kufanya utafiti na kukusanya maoni toka kwa watumiaji wengine kabla ya kununua, nimepata pikipiki tatu ambazo zinashindana kwa vigezo ninavyovihitaji mimi. Vigezo hivyo ni:
1. Uwezo wa kutumia mafuta kidogo kwa safari za km 50 kila siku.
2. Ubora wa injini (sitegemei kumwona fundi kila wiki).
3. Uwezo wa kutembea njia rough na lami, maana naishi mjini ila nafanya kazi kijijini.

Baada ya upembuzi huo nimepata pikipiki hizi ambazo naomba mnichagulie moja ya kununua.


Hii ni TVS HLX 150 yenye gia 5.


Honda ACE150 hii.


Boxer 150 X hii.

Nichukue ipi wakuu maana zote zinanichanganya kimaamuzi.
 
Boxer BM 150 ni nzuri kama wewe una kimo cha wastani. Ninayo tangu 2023 mwanzoni bado iko powa naitumia kwa matumizi yote off road na Rami maana naishi mjini ila shughuli zangu za kiuchumi zinategemea zaidi shambani.

-Ulaji mzuri wa mafuta
-Comfort ability hasa ukizingatia mie sio mrefu sanaa kwahyo inanipa hali ya utulivu ukilinganisha na Tvs kidogo ndefu sanaa
-Muonekano pia huwa sipendi ile show ya nyuma ya Tvs
 
Boxer 150 chuma hicho mdomo wa mamba
Mkuu, Domo la Mamba naona ni lugha ya mtaani, hasa wale wa Dar, sisi wa mikoani (niko Iringa) naona mnaniacha mbali. Kuna Boxer 2 hapo kwenye hiyo 150.

1. Boxer 150HD
2. Boxer 150 X

Domo la Mamba ni ipi kati ya hizi? Samahani kwa hii illiteracy yangu kwenye lugha yenu mkuu πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 
Hii hapa
 
Ningekuwa mimi ningechukua Boxer 125 nisave mafuta zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…