NIDA yangu imefutika kabisa, personal details zote hazionekani kimebaki ki card blank tu. Je Kuna uwezekano wa kupata on same day?

Kama Kuna yeyote aliwahi kupereka akabadilishiwa Kwa wakati at least 1 week atupe mrejesho. Maana nimefatilia comments za watu Instagram page ya NIDA naona watu wanalalamika kuwa walipereka vibovu wapewe vingine ila mpaka Sasa hawajapata almost 3 months na wengine walilipia 20k
 
mwanangu inatokea hivo unakuta kwenye harakati ya utengenejazi saa zngn mashin inazingua
 
Bora usumbufu ungekuwa kwenye mtu anayejisajiri Kwa mara ya kwanza. Sasa mtu tayari una number, au una ID imefutika au imepotea wanakuzungusha 3 months za nini wakati taarifa zako walizihakiki ndo maana ukapewa ID au number ya ID?
 
Shida ni kulalamika kabla hujafuata taratibu fuata kwanza ndio uje kulalamika tatizo mnataka shortcut bila kuwajibika mkiombwa rushwa mnakuja lalamika huku

Mfano tu hilo tangazo halijatoka leo ni miezi sasa toka nida watoe hilo tangazo wewe huenda umelijua au hukua na kazi ya hicho kitambulisho sasahivi yamekukuta ya kuhitaji nida ndio unakuja wanguwangu na lawama kibao
 
Nyie ndio wanasiasa uchwara tusiowataka nchi hii, Kila mahali unataka kufanya siasa
Inamaana wewe huelewi kipi kwa jamaa anachokisema??
Hapo unaweza kukuta na mwenyew hapo alipo hana ID card halisiπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Yangu nimechukua mwaka jana,sijawahi ifulia wala ikanyaga kukaa tu kwenye wallet imefutika 🀣🀣🀣
Sina power ya kufatilia tena!
Bora ufanye harakati za kufuatilia passport utakuwa rahisi kuliko kufuatilia NIDA.
 
Sawa kaka acha tuwajibike
 
Nyie ndio wanasiasa uchwara tusiowataka nchi hii, Kila mahali unataka kufanya siasa
Inamaana wewe huelewi kipi kwa jamaa anachokisema??
Hii ndio shida ya jf, yaani unatakiwa uwe na mawazo sawa na watu wote humu ambao karibia wote ni wahanga wa serikali na chama tawala ukiwa tofauti na wao wewe ni chawa au ccm, mtaumia sana kwa fikra zenu hizo sisi wengine hatujali

Yaani usifuate utaratibu uje ulaumu huku tukuache? Mleta mada mwenyewe hata ofisi za nida hajaenda, tangazo la kurudisha vitambulisho halijui ila analalamika kama kashaenda na hajashughulikiwa tatizo lake kwa chochote bado mnataka tumsapoti kwakuwa inayopondewa ni serikali ya ccm tukiongea eti siasa ajabu hii
 
Kiongozi usiende mbali Sasa! CCM inahusika vipi hapa Sasa? We are addressing issue ambao inajulikana kuwa kuna changamoto Kwa muda mrefu Sio mambo ya vyama au siasa. Unadhani nimekurupuka na kuleta maada hapa bila kujua kama Kuna hiyo changamoto? I know nikienda sitapata NIDA hiyo on same day that's why nikataka kujua ikiwa naweza kupata mkato wa haraka kutokana na uhitaji wangu wa haraka. Na compain kubwa yetu ni pale ID mhimu kama NIDA inachukuwa zaidi ya mwezi kupata wakati ni kitambulisho kikubwa kuliko vyote nchini mwetu ukitoa passport.
 
Niliem-quote ndio kaongelea siasa mkuu sio wewe angalia vizuri na soma comment yake
 
Mbona kinatoa harufu ya Konyagi Mkuu?! Ndiyo chanzo,usiwe unaenda nacho Bar ukipata kingine nadhani uhakika wa kupata kingine ni kwenye September -2029 huko,Ma CCM yatakuwa na hekaheka tena za kupora Uchaguzi wa Serikali za Mitaa!!!
 
Mbona kinatoa harufu ya Konyagi Mkuu?! Ndiyo chanzo,usiwe unaenda nacho Bar ukipata kingine nadhani uhakika wa kupata kingine ni kwenye September -2029 huko,Ma CCM yatakuwa na hekaheka tena za kupora Uchaguzi wa Serikali za Mitaa!!!
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ Kiongozi hivo vitu sutumii kabisa
 
Zanzibar ID kuna baadhi zina zaidi ya miaka 25 na hazijwahi kufutika. Hayo makorokoro ya NIDA sijawahi kuyaelewa. Wizi mtupu, watu kila pahali wanawaza upigaji tu. Shame
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…