Hii nchi rushwa haitokaa iishe, kitambulisho Cha mpiga kura tulikipata siku hiyo hiyo Moja na Kiko vzr sana, mimi changu kina miaka 10 sasa lkn ubora ni huo huo, hakukuwa na usumbufu wa aina yoyote, lkn hata kitambulisho Cha mpiga kura kikipotea kikifika kipindi Cha kujiandikisha hakuna usumbufu wowote wananchi wanaupata.
Lkn hivi feki upatikanaji wake ni shida kweli kweli, gap la usumbufu linatengeneza mazingira ya rushwa ya wazi wazi lkn wanajifanya kama hawaoni. .
Kwa mfano: hizo NIDA zingekuwa zinatolewa serikali za mitaa kungekuwa na shida Gani? Mbona kwenye vitambulisho vya mpiga kura hatuamlishwi kulundikana kwenye halimashauri??(Ukilundika watu sehemu moja na wote wasubilie huduma Moja unatengeneza mazingira ya Rushwa)
Kama ni taarifa muhimu za mtu anaeomba hicho kitambulisho basi serikali za mitaa wanataarifa nzuri za muhusika kuliko hata huko halimashauri, kikubwa tu hao watumishi wa NIDA waliolundikana sehemu moja wasogezwe serikali za mitaa wawafanyie kazi wananchi.
Binafsi nishakata tamaa na mamilolongo Yao,Kila siku nenda ludi nenda ludi na unashinda siku nzima uko kwenye foleni.