Nifah: Rasmi, Mimi & The Bold tumeachana

View attachment 2858656

Mapenzi kama yalivyo mambo mengine yana mwanzo na mwisho pia. Ni wachache waliobarikiwa na wenye bahati katika mapenzi huishia pamoja kwa kudumu milele hadi kifo kuwatenganisha, Huku wengi wakiishia njiani na hakuna ubaya katika hilo. Ndio maisha na mapenzi…. Ni safari isiyotabirika.

Miaka kadhaa iliyopita nilipata kuingia katika mapenzi yaliyofahamika na wengi hapa jamvini.
Hivyo basi, kwa kuwa mapenzi yale hayapo tena, imeniwia vyema kurudi tena hapa kuweka hilo wazi.

Tulikuwa na malengo ya kufika mbali, lakini kutokana na kutofautiana katika mambo mengi tulishindwa hata kufikia hatua za kuyarasimisha mahusiano yetu kuwa halali.

Tulitengana rasmi mwezi August mwaka huu 2023, na kutokana na hilo pengine huenda yakawa ndio mahusiano yangu ya mwisho kuyaweka wazi.

Mapenzi ya wazi hapa yamenipa wakati mgumu kujibu mamia ya wanachama waliokuwa wakihoji endapo bado tupo pamoja, na ndio sababu kuu naweka uzi huu kuwafahamisha wote kwa pamoja, hatupo tena katika mahusiano.

Tumeachana kwa amani, na kwa dhati kabisa namtakia kheri katika maisha mapya bila ya uwepo wangu kwa aliyekuwa mwenzangu.

Nifah

Sbb mlikuwa katika mapenzi tu, na hamjafikia hatua ya ndoa, sio mbaya, mme enjoy and things didn’t go to your expectations, let it go…!!

Keep moving, opportunity dances with those already on the dance floor..!! So never stop looking for your next soulmate..!!! Life is full of sweet moments…!! Kila la kheri..!!
 
🤣🤣🤣Unamuonea sana huyo jamaa
Mimi Raia mwema napambana sana jamaa Maghayo aache bange yeye pamoja na genge lake kwani madhara yake ni makubwa kwa members humu.

Cheki mfano hapo chini Ghayo's gang wakiingia Jf baada ya kushambulia vipisi vya bange , Bora hata dronedrake Bakari Nondo yake haikeri members humu.
IMG_20231102_220344.jpg
 
Mimi Raia mwema napambana sana jamaa Maghayo aache bange yeye pamoja na genge lake kwani madhara yake ni makubwa kwa members humu.

Cheki mfano hapo chini Ghayo's gang wakiingia Jf baada ya kushambulia vipisi vya bange , Bora hata dronedrake Bakari Nondo yake haikeri members humu.View attachment 2858733
hahahahaha dah
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
View attachment 2858656

Mapenzi kama yalivyo mambo mengine yana mwanzo na mwisho pia. Ni wachache waliobarikiwa na wenye bahati katika mapenzi huishia pamoja kwa kudumu milele hadi kifo kuwatenganisha, Huku wengi wakiishia njiani na hakuna ubaya katika hilo. Ndio maisha na mapenzi…. Ni safari isiyotabirika.

Miaka kadhaa iliyopita nilipata kuingia katika mapenzi yaliyofahamika na wengi hapa jamvini.
Hivyo basi, kwa kuwa mapenzi yale hayapo tena, imeniwia vyema kurudi tena hapa kuweka hilo wazi.

Tulikuwa na malengo ya kufika mbali, lakini kutokana na kutofautiana katika mambo mengi tulishindwa hata kufikia hatua za kuyarasimisha mahusiano yetu kuwa halali.

Tulitengana rasmi mwezi August mwaka huu 2023, na kutokana na hilo pengine huenda yakawa ndio mahusiano yangu ya mwisho kuyaweka wazi.

Mapenzi ya wazi hapa yamenipa wakati mgumu kujibu mamia ya wanachama waliokuwa wakihoji endapo bado tupo pamoja, na ndio sababu kuu naweka uzi huu kuwafahamisha wote kwa pamoja, hatupo tena katika mahusiano.

Tumeachana kwa amani, na kwa dhati kabisa namtakia kheri katika maisha mapya bila ya uwepo wangu kwa aliyekuwa mwenzangu.

Nifah
Pole sana na hongera kwa kuweka wazi kuanzia mwanzo na mwisho wake umeuweka wazi pia.

Haya maisha yana vitu vingi sana kuna wakati tunaepushwa jambo fulani bila kujua pengine mahusiano yenu yangedumu mmoja wenu angekata moto ili lisitokee hilo mahusiano inabidi yajifie so wakati mwingine hatupaswi kulaumiana ni kuiacha nature iamue. Ombi moja kwako nakuomba basi hata kama mmeachana mwambie arudishe majeshi jf bado tunawajitaji wote.
 
Back
Top Bottom