Nifah: Rasmi, Mimi & The Bold tumeachana

Nifah: Rasmi, Mimi & The Bold tumeachana

Yani Wana ujasiri aisee wanafaa hata kwenda kwenye vita [emoji3]
Watu wadate kimya kimya mkiachana kilamtu anakula hamsini zake maisha yanaendelea
Si ndiyo...

Kuna hilo Husiano moja lilikuwaga humu[emoji1]Enzi hizo Bidada kila sehemu ni kumtaja jamaa...

Jamaa akija ana'like tu.. hajibu wala nini...Ni kama jamaa alikuwa hapendi ile kitu..

Sasa hivi sijui hata lilishiaga wapi[emoji1]
 
View attachment 2858656

Mapenzi kama yalivyo mambo mengine yana mwanzo na mwisho pia. Ni wachache waliobarikiwa na wenye bahati katika mapenzi huishia pamoja kwa kudumu milele hadi kifo kuwatenganisha, Huku wengi wakiishia njiani na hakuna ubaya katika hilo. Ndio maisha na mapenzi…. Ni safari isiyotabirika.

Miaka kadhaa iliyopita nilipata kuingia katika mapenzi yaliyofahamika na wengi hapa ojamvini.
Hivyo basi, kwa kuwa mapenzi yale hayapo tena, imeniwia vyema kurudi tena hapa kuweka hilo wazi.

Tulikuwa na malengo ya kufika mbali, lakini kutokana na kutofautiana katika mambo mengi tulishindwa hata kufikia hatua za kuyarasimisha mahusiano yetu kuwa halali.

Tulitengana rasmi mwezi August mwaka huu 2023, na kutokana na hilo pengine huenda yakawa ndio mahusiano yangu ya mwisho kuyaweka wazi.

Mapenzi ya wazi hapa yamenipa wakati mgumu kujibu mamia ya wanachama waliokuwa wakihoji endapo bado tupo pamoja, na ndio sababu kuu naweka uzi huu kuwafahamisha wote kwa pamoja, hatupo tena katika mahusiano.

Tumeachana kwa amani, na kwa dhati kabisa namtakia kheri katika maisha mapya bila ya uwepo wangu kwa aliyekuwa mwenzangu.

Nifah
Ok. SASA UNATAKA TUFANYE NINI? AU HILO LINATUATHIRI VIPI SISI WA JF?
 
Back
Top Bottom