plan z
JF-Expert Member
- Jun 10, 2019
- 1,394
- 1,434
Chukua milioni 10 fungua fixed akaunti NMB.
Milioni 10 iliyobakia nenda Silverland Tanzania/Silverland Dar nunua vifaranga aina y SASSO 1000 kila mmoja ni 1400, wafuge ndani ya miezi minne watakuwa wamekuwa wakubwa kweli kweli utauza kwa 15,000 au 20,000 kwa mmoja.
NB: SASSO ni kuku chotara wanaovumilia magonjwa na hali ngumu zote.
Gharama ya kuwahudumia SASSO 1000 pamoja na banda, madawa n.k havitazidi hata milioni 5.
Pia jifunze formula ya kutengeneza chakula cha kuku wewe mwenyewe ili kupunguza gharama.
Babu ufugaji wa kuku sio mwepesi kama ulivyoandika, tena vifaranga wanahitaji matunzo ya hali ya juu ukiwazembea hata masaa manne unaweza kuta wamekufa kama robo ya idadi uliyonunua, mpaka wanakua unakuta umekuza robo ya idadi ya uliyonunua mpaka hapo unakuwa ushaingia hasara bado hatujapigia gharama ya chakula na dawa ulizonunua, ikumbukwe hao ni vifaranga hivyo hakuna mayai hapo yaliyotagwa useme utauza mayai urudishe hela.
Kwa nadharia ni rahisi kweli ila ukiingia mzigoni utaona mziki wake, mbaya zaidi ukute mtu ndo mara ya kwanza umemshauri hivyo na hajawahi kufuga, hajui changamoto zake atajikuta anaua vifaranga vyote na kuanza kukuachia laana wewe uliyemshauri. Ukitaka kuamini ingia mtaani ufanye research kuhusiana na hilo ulilomshauri. It is not a win to win situation 100%