Kwa nadharia hii biashara kila mtu huona ni rahisi hivi, ila kivitendo unakuja kugundua ina changamoto nyingi sana, mfano unaweka makadirio ya chakula katika miezi 6 inakuja kuzidi nje ya bajeti, na kupata quality ya chakula bora nayo ishu, kuna chakula unaweza lisha miezi 8 kuku hawaongezeki uzito tu na unaweza kufika muda wa kuuza ukakuta soko limeshuka, ukahangaika mwezi na bei na kila kuku wakizidisha kukukalia hata siku3 wanakukosti gharama zaidi, unaishia kuwauza kwa shoti. Na mwisho ukitaka kukwepa hasara ni lazima unapoanzia hii biashara umuajiri kijana ambaye tayari ana uzoefu wa kutosha ili kukupa uzoefu na mfano chakula cha vifaranga, muda wa kubadilisha chakula, muda wa chanjo, namna ya kusafisha mabanda na kadhalika. Kila kitu katika hii biashara kinategemea Timing ukikosea imekula kwako big time.