Nifanye ibada kwa njia ipi ili Mungu wangu ajibu maombi yangu kwa haraka?

Nifanye ibada kwa njia ipi ili Mungu wangu ajibu maombi yangu kwa haraka?

Mwenzenu nina shida ya haraka, ambayo nikiweza kutatua ndani ya siku 3, maisha yangu yatakuwa yamefunguliwa upya. Kila nikiwaza binadamu gani wa kunisaidia simuoni. Tumaini ninaloliona ni kupata msaada toka kwa Mwenyezi Mungu. Wana bodi, Nifanye ibada gani Ili Mungu anisaidie kwa uharaka?
Toa sadaka mkuu huku sadaka Hiyo ukiinuia dhidi ya matatizo uliyonayo au Jambo ulilonalo
 
Mwenzenu nina shida ya haraka, ambayo nikiweza kutatua ndani ya siku 3, maisha yangu yatakuwa yamefunguliwa upya. Kila nikiwaza binadamu gani wa kunisaidia simuoni. Tumaini ninaloliona ni kupata msaada toka kwa Mwenyezi Mungu. Wana bodi, Nifanye ibada gani Ili Mungu anisaidie kwa uharaka?
Amka saa 9 usiku na ongea naye Mungu kwa namna utayo ona inafaa, halafu concentrate- mweleze Mingu shida zako- atakusikiliza ukinuia haswa... hii bi kutokana na uzoefu wangu kwa mambo niliyopitia na hajawahi kuniangusha katika maombi yangu hasa katika muda huo...
 
Msione kimya Wadau nawafuatilia wote maoni yenu.Kuna mtu amedokeza kwamba,kulileta hapa swali langu,huenda nikapata muafaka,na mimi nimeanza kuona.Hebu tuendelee kutoa maoni,najua utanufaisha na wenzangu wenye kiu kama yangu
 
Mungu anajibu kwa wakati wake na siyo wakati wako. Sasa kama atakujibu ndani ya miaka 100 ukiwa umekufa ndiyo utajua unajua au hujui
 
(Anyone can) TRY THIS!!

1 Asubuhi kabla jua halijachomoza nenda njia panda (sehem ambapo njia/barabara zinatengeneza +.

2 Simama kwa kuangalia mashariki (jua linapochomoza)

3 Fumba macho, Sali ile sala ya BABA YETU ULIE JUU MBINGUNI....(ukimaliza hii sala)...

4 Muombe Mungu (unaemwamini wewe binafsi) ukimuelezea shida yako.

Baada ya hapo rudi nyumbani/ endelea na siku yako kama kawaida.

Ni kitendo cha dakika 1-2
 
"Nitajibu maombi yako kesho" ya Mwenyezi Mungu sawa na kusema nitajibu maombi yako baada ya siku elfu moja! (Du!)

12hrs = 500 days
6hrs = 250 days
3hrs = 125 days
90min = 62.5 days
45min = 31.25 days
22.5min = 15.63 days
11.25min = 7.81 days
5.63mib = 3.9 days
2.8min = almost 2 days
1.9 min = almost 1 day
1 min = may mean in six hours.

Hivyo fanya maombi ili "Mwenyezi Mungu" ajibu kwa kusema, "wait a minute"

Kama ni Muislamu piga 24434 kila siku, na usisahau kupiga 2 usiku wa manane.

Kama ni Mkristu au imani nyingine fanya vile viongozi wako wa kiimani wanavyoshauri.

Mungu hujibu maombi.
 
Mwenzenu nina shida ya haraka, ambayo nikiweza kutatua ndani ya siku 3, maisha yangu yatakuwa yamefunguliwa upya. Kila nikiwaza binadamu gani wa kunisaidia simuoni. Tumaini ninaloliona ni kupata msaada toka kwa Mwenyezi Mungu. Wana bodi, Nifanye ibada gani Ili Mungu anisaidie kwa uharaka?
Mungu hana shortcut
 
Msione kimya Wadau nawafuatilia wote maoni yenu.Kuna mtu amedokeza kwamba,kulileta hapa swali langu,huenda nikapata muafaka,na mimi nimeanza kuona.Hebu tuendelee kutoa maoni,najua utanufaisha na wenzangu wenye kiu kama yangu
Unasali dini ipi ndugu ?
 
Mwenzenu nina shida ya haraka, ambayo nikiweza kutatua ndani ya siku 3, maisha yangu yatakuwa yamefunguliwa upya. Kila nikiwaza binadamu gani wa kunisaidia simuoni. Tumaini ninaloliona ni kupata msaada toka kwa Mwenyezi Mungu. Wana bodi, Nifanye ibada gani Ili Mungu anisaidie kwa uharaka?
Well inategemea Mungu wako ni yupi nikimjua nitaweza kukushauri jambo.
 
Mimi ni a Catholic cristian
1.Kabla hujaanza chochote anza na sala ya toba, tubu ujinyenyekeze, jishushe umuombe mungu akusamehe makosa yako unayoyafahamu na usiyo yakumbuka.

2.Pili mshukuru mungu kwa kile kidogo alicho kujaalia afya na yale yoote mabaya/mabalaa aliyokuepusha ajali, magonjwa etc

3.Samehe wale wote waliokukosea ambao unakinyongo nao, wadeni wako hii sii kwamba ukaonane nao hapana samehe tu ndani ya moyo wako.

5. Udhuria misa takatifu, watu wengi wanafeli hapa ukienda kanisani utapata amani ya moyo hata kama hiyo wiki kuna kitu unafatilia ukienda kanisani ukasali kwa imani mungu atakutendea jambo.

6.Hii ndio main kama unavyojua sala ya kuu ya kuomba ambayo yesu alitufundisha ni Baba yetu. Sasa Tafuta rozali takatifu halafu uwe unaamka usiku kuanzia saa 9 hadi 10 alfajiri usivuke hapo .
Kisha uanze kusali kuanzia huo utaratibu niliokueleza hapo juu ukimaliza chukua rozali uanze kusali baba yetu kulingana na idadi ya zile kete za rozali.
Zile kete zilizoungana ziko jumla 53 sasa utarudia baba yetu mara 53 halafu zile zilojitenga moja moja ziko jumla 6 hizo utasali salamu maria mara 6.

7.Ukimaliza utaunganisha na mahitaji yako unayoomba mungu akutendee. Na usilazimishe wala kulaumu muache mungu akutendee kadri ya mapenzi yake na sio wewe unavyotaka, pengine unaweza kuwa unataka kufanikisha ilo jambo kwa matazamio yako ila mungu anaweza kukuvusha kwa njia nyingine usiyotarajia hadi ukabaki unashangaa
 
Back
Top Bottom