Mwenzenu nina shida ya haraka, ambayo nikiweza kutatua ndani ya siku 3, maisha yangu yatakuwa yamefunguliwa upya. Kila nikiwaza binadamu gani wa kunisaidia simuoni. Tumaini ninaloliona ni kupata msaada toka kwa Mwenyezi Mungu. Wana bodi, nifanye ibada gani Ili Mungu anisaidie kwa uharaka?
kuna siri moja wengi hawaijui. nayo ni hii; MAOMBI YENYE UHAKIKA KWAMBA YAMEFIKA KWA MUNGU NA MUNGU ATAJIBU, NI MAOMBI KWA ROHO MTAKATIFU, YAANI YA KUNENA KWA LUGHA. achana na lugha za kuiga, na lugha ambazo sheteni anawajaza watu ili wajione kama wamejazwa kumbe sio, ile inayotokea kwa hakika, baada ya mtu kuokoka, ametakaswa akajazwa Roho Mtakatifu na kunena kwa lugha, na moyoni unashuhudiwa hivyo. maombi hayo ni 100% yanajibiwa yote. why? kwasababu ni Mungu mwenyewe anakusaidia kuomba (Roho Mtakatifu) na utaomba sawasawa na mapenzi yake.
Warumi 8:26 - 27 INASEMA; Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa. na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.
Wagalatia 4:6 Na kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, Aba, yaani, Baba.
hii inaweza kuleta discussion ndefu sana kwasasbabu wapo wanaopinga kabisa ujazo wa Roho Mtakatifu, wapo wanaomkataa kabisa kama wakatoliki na wengine. wanaamini wao wanaweza peke yao, na kujazwa wanasema sio lazima kwasababu wanamini hicho ni kipawa mtu mmoja aweza kupewa na mwingine asipewe, wakati Yesu alisema bila huyo hatuwezi kufanya lolote.
kwa ushauri, unaweza kuomba kwa akili, na unaweza kuomba kwa Roho Mtakatifu (kunena). ila maombi ya Roho ni asilimia mia yamefika na yatajibiwa, ya akili ni machache hata yakifika yatajibiwa kwasababu akili yako utaomba kwa tamaa za mwili wako na hauwezi kuomba sawasawa na mapenzi ya Mungu. Okoka, mpe Yesu maisha yako, omba akujaze Roho Mtakatifu, naye atakusaidia kuomba na atakuwa Mungu wako.
Waefeso 2:20-21 inasema, Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yale tuyaombayo au tuyawazayo kwa kadiri ya Nguvu itendayo kazi ndani yetu. (
hiyo nguvu itendayo kazi ndani yetu sio ya kibinadamu ni Nguvu ya Roho, hapa anaongelea watu waliookoka na kuishi na Roho Mtakatifu, sio watu wote, kwasababu ni wale waliookoka na kuongozwa na Roho tu ndio wana hiyo nguvu).