1.Kabla hujaanza chochote anza na sala ya toba, tubu ujinyenyekeze, jishushe umuombe mungu akusamehe makosa yako unayoyafahamu na usiyo yakumbuka.
2.Pili mshukuru mungu kwa kile kidogo alicho kujaalia afya na yale yoote mabaya/mabalaa aliyokuepusha ajali, magonjwa etc
3.Samehe wale wote waliokukosea ambao unakinyongo nao, wadeni wako hii sii kwamba ukaonane nao hapana samehe tu ndani ya moyo wako.
5. Udhuria misa takatifu, watu wengi wanafeli hapa ukienda kanisani utapata amani ya moyo hata kama hiyo wiki kuna kitu unafatilia ukienda kanisani ukasali kwa imani mungu atakutendea jambo.
6.Hii ndio main kama unavyojua sala ya kuu ya kuomba ambayo yesu alitufundisha ni Baba yetu. Sasa Tafuta rozali takatifu halafu uwe unaamka usiku kuanzia saa 9 hadi 10 alfajiri usivuke hapo .
Kisha uanze kusali kuanzia huo utaratibu niliokueleza hapo juu ukimaliza chukua rozali uanze kusali baba yetu kulingana na idadi ya zile kete za rozali.
Zile kete zilizoungana ziko jumla 53 sasa utarudia baba yetu mara 53 halafu zile zilojitenga moja moja ziko jumla 6 hizo utasali salamu maria mara 6.
7.Ukimaliza utaunganisha na mahitaji yako unayoomba mungu akutendee. Na usilazimishe wala kulaumu muache mungu akutendee kadri ya mapenzi yake na sio wewe unavyotaka, pengine unaweza kuwa unataka kufanikisha ilo jambo kwa matazamio yako ila mungu anaweza kukuvusha kwa njia nyingine usiyotarajia hadi ukabaki unashangaa