Nifanye nini? Ndoa ina miezi 10, mke wangu kabadili dini kaolewa na mwanaume mwingine

🤣🤣🤣🤣 Mkuu kegel tena!. Atakuambia yeye ana pihechdii.
😂😂na ilo ndo tatizo la wasomi wetu mkuu, Code yake ipo wazi sana, kuna vitu anafeli
 
  • Thanks
Reactions: al1
Niliunganishwa na huyu mke wangu na shangazi yangu. Kipindi hicho nilikuwa nimetoka masomoni Uingereza, na kwa kuwa nilitoka huko nikiwa na kazi tayari, hivyo nilikuwa nishajipanga kimaisha na mambo yalikuwa mazuri. Sikupanga kuoa kwa kipindi hicho, lakini kama unavyojua familia zetu, ukiwa na miaka 36, una PhD na kipato kizuri basi kelele ni kuoa.

Kipindi naondoka Tanzania nilikuwa na mchumba, ila kutokana na umbali, alishindwa kuvumilia miaka 3 hivyo nilirudi nikiwa sina mtu. Shangazi yangu aliniunganisha na huyu binti akiniambia ni mtoto wa rafiki yake hivyo anamjua na anajua familia yake vizuri.

Sikupenda mambo ya kuunganishwa lakini baada ya kumuona basi nilichanganyikiwa na mapenzi yakaanza. Kusema kweli tulikuwa vizuri, tunazungumza, tunacheka na ndani ya miezi 6 tulishafika mashabahuni na kuapa mpaka ki*fo kitutenganishe.

Sikujua chochote kuhusu mahusiano yake ya nyuma mpaka wiki mbili baada ya ndoa, baada ya kuwa karibu sana na mke wangu ndipo nikagundua kuwa ile furaha aliyokuwa ananionyesha ilikuwa ni ya kuigiza. Kulikuwa na namba fulani alikuwa anachati nayo mara kwa mara. Sikutaka kumfuatilia ila niliona ni kama ni mama yake, lakini kuna siku meseji za mapenzi zikaingia na nikajiuliza, anachati mapenzi na mama yake?

Basi nikaamua kufuatilia, na kwa ujuzi wangu haikuchukua muda nikajua alikuwa anawasiliana na X wake. Hapo ndipo niligundua kuwa mke wangu kabla yangu alikuwa na mchumba kwa miaka kama 7 hivi, walipendana sana, lakini alipompeleka kwao, mama yake alimkataa kwa sababu ya dini.

Waligoma kupokea mahari na mwaka mzima walikuwa wakimsumbua, binti alikuja kukubali kuachika baada ya kijana kuamua kuoa mwanamke mwingine. Ila bado waliendelea kuwasiliana, lakini binti hakutaka kuniambia akiamini kuwa ningemuacha. Ukweli ni kuwa ningemuacha lakini tayari tumeshaingia kwenye ndoa, tena ya Kikatoliki, utatoka vipi?

Basi tulizungumza, akaomba msamaha na kuniambia hawatawasiliana tena. Lakini baada ya hapo ndipo ikawa shida tena ndani, kila kitu ni kugombana, kuninunia bila sababu. Alikuwa ananifanyia vituko mpaka nikagundua kuwa anatafuta sababu za kugombana ili tu tukinuniana awe bize kuchati na mwanaume wake. Ilifikia kipindi hali ilinichosha, nikamtafuta yule mwanaume kumuomba amuachie mke wangu, si ana mke wake bwana!

Hapo ndipo niliharibu, maana alinitukana sana, akanisema mambo mengi, lakini kubwa lililoniumiza ni kuniambia kuwa mke wangu ni mjamzito na mimba ni yake. Sikuamini kwani nikikumbuka juzi mke wangu ndiye aliyeniambia nimnunulie pedi, ujauzito unatoka wapi? Lakini niliporudi nyumbani kuongea na mke wangu, akaniambia ni kweli ana ujauzito wa miezi 3, lakini mimba ni yangu kwani hajawahi kulala na huyo mwanaume.

Nilipomuuliza kwa nini hukunambia, aliniambia sikujua, kwani bado nilikua naona siku zangu. Nilivyokuwa mjinga niliamini, ila mwezi uliopita mke wangu aliniaga anaenda kwao kujifungua.

Basi tukaongea vizuri nilitaka kumpeleka akaniambia Hapana nitaenda mwenyewe. Sasa juzi mama yake akanipigia simu kuniuliza kwa nini sijampeleka mke wangu kujifungua wakati tulishakubaliana hivyo. Nikamwambia mbona kaniambia anakuja huko! Basi katika kutafuta na kuhangaika, naambiwa mke wangu kaenda ukweni, yaani kwa huyu mwanaume, na huko ndiyo ameenda kujifungua na amebadili dini wamefunga ndoa ya Kiislamu.

Nilimtafuta, akaniambia ni kweli. Akasema nimeamua nisidanganye tena, huyu mtoto si wako, ni wa huyu mwanaume wangu. Nimeamua kubadili dini ili kufuata moyo wangu. Wewe ni mwanaume mzuri sana, ulinipokea na kunikubali na machungu yangu, naamini Mungu atakubariki na mwanamke mwingine.

Lakini mimi sasa ni mke wa mtu, endelea na maisha yako! Kwa kweli sijui nifanye nini, nimechanganyikiwa hata kutoka ndani nashindwa. Sijaweza kumuambia mtu yeyote hata wazazi wangu, siwezi kuongea nao
Mbona amekurahisishia, napenda sana wakuondoka mwenyewe. Umri bado mdogo na utapata wa kueleweka
 
1.Toka mnaanzisha mahusiano huyo mwanamke hakuwa wako ,inawezekana alikuwa nawe kimwili ila moyo wake ulikuwa kwa Ex wake.(HAKUWAHI KUKUPENDA NA HATAKUJA KUKUPENDA kama anavyompenda ex wake aliyemuoa mke wa pili.
Alijaribu kuigiza kukupenda ,au pengine kujaribu kumsahau ex wake ili awe na wewe either kwa sababu ya kunufaika na mahusiano yenu au sababu alikorefishwa na ex wake ,lakini akashindwa kuigiza kukupenda akashindwa kumsahau ex wake.Na AKASHINDWA KUIDANGANYA NAFSI YAKE AU KUIDHULUMU NAFSI YAKE.AMANI YA MOYO WAKE.
2)Shukuru sana huyo mwanamke ameamua kuwa muwazi na mkweli kwa kuamua KUKUACHA na kwenda kumrudia ex wake.SHUKURU SANA KWA YEYE KUFANYA HIVYO.Kama asingeondoka hapo angekupa stress ,ungeumizwa sana na mapenzi kwa kuwa wewe ulimpenda ,wakati yeye hakupendi ,wewe ungeteseka sana ,ungepitia machungu makubwa sana.KUPENDA USIPOPENDWA NI MAUMIVU MATESO BILA CHUKI.
3)Haukutakiwa kwenda kigombana na ex wake baada ya kugundua anakusaliti na ex wake,ulitakiwa a)UMUACHE PIGA CHINI mana mwanamke mtu mzima mwenye akili timamu akiamua kukusaliti huwa anafanya kwa kudhamiria na kwa kupenda sio kwa tamaa au kipitiwa,na moyo wake huwa kwa huyo anyekusaliti naye.Mwanamke akishakusaliti ina maana moyo wake mapenzi yake yapo kwa huyo sio kwako.Ina maana moyo wake umetekwa huko na akili zake na mwili na yupo tayari kimsillkiliza na kumuheshimu huyo mgoni wako ,na wewe atakudharau na kukuona kama kituko moyoni mwake wewe huna thamani hata kama asipokuonyesha ila ndani yake wewe haupo .
Sasa kwenda kugombana na mgoni wako sio sahihi kwa sababu wakikaa wawili wanakua kitu kimoja wote wapo against wewe.Kwenda kumuomba asitembee na mke wako ni kujichorasha na kujidharaulisha ,infact hakuwa wako ,japo mlikuwa mnaishi pamoja,na kulala pamoja ila moyoni hakuwa wako.
4)UMEJIFUNZA KITU kila jambo linalotokea linafundisha kiti na elimu ni bahari haina mwisho,tinajifunza kila siku kitoka kwa kila mtu/kila jambo,tunajifunza kutokana na makosa.
5)AKILI inatakiwa itawale HISIA kuna wakati unatakiwa ufanye maamuzi au mambo kwa kutumia akili Mungu alizokupa usiruhusu hisia utapotea,ndio mana unaona wachangiaji wana hoji elimu ya PHD na maamuzi yako au kufikiri kwako.
 
Chai chapati 2

20240910_234515.jpg
 
Niliunganishwa na huyu mke wangu na shangazi yangu. Kipindi hicho nilikuwa nimetoka masomoni Uingereza, na kwa kuwa nilitoka huko nikiwa na kazi tayari, hivyo nilikuwa nishajipanga kimaisha na mambo yalikuwa mazuri. Sikupanga kuoa kwa kipindi hicho, lakini kama unavyojua familia zetu, ukiwa na miaka 36, una PhD na kipato kizuri basi kelele ni kuoa.

Kipindi naondoka Tanzania nilikuwa na mchumba, ila kutokana na umbali, alishindwa kuvumilia miaka 3 hivyo nilirudi nikiwa sina mtu. Shangazi yangu aliniunganisha na huyu binti akiniambia ni mtoto wa rafiki yake hivyo anamjua na anajua familia yake vizuri.

Sikupenda mambo ya kuunganishwa lakini baada ya kumuona basi nilichanganyikiwa na mapenzi yakaanza. Kusema kweli tulikuwa vizuri, tunazungumza, tunacheka na ndani ya miezi 6 tulishafika mashabahuni na kuapa mpaka ki*fo kitutenganishe.

Sikujua chochote kuhusu mahusiano yake ya nyuma mpaka wiki mbili baada ya ndoa, baada ya kuwa karibu sana na mke wangu ndipo nikagundua kuwa ile furaha aliyokuwa ananionyesha ilikuwa ni ya kuigiza. Kulikuwa na namba fulani alikuwa anachati nayo mara kwa mara. Sikutaka kumfuatilia ila niliona ni kama ni mama yake, lakini kuna siku meseji za mapenzi zikaingia na nikajiuliza, anachati mapenzi na mama yake?

Basi nikaamua kufuatilia, na kwa ujuzi wangu haikuchukua muda nikajua alikuwa anawasiliana na X wake. Hapo ndipo niligundua kuwa mke wangu kabla yangu alikuwa na mchumba kwa miaka kama 7 hivi, walipendana sana, lakini alipompeleka kwao, mama yake alimkataa kwa sababu ya dini.

Waligoma kupokea mahari na mwaka mzima walikuwa wakimsumbua, binti alikuja kukubali kuachika baada ya kijana kuamua kuoa mwanamke mwingine. Ila bado waliendelea kuwasiliana, lakini binti hakutaka kuniambia akiamini kuwa ningemuacha. Ukweli ni kuwa ningemuacha lakini tayari tumeshaingia kwenye ndoa, tena ya Kikatoliki, utatoka vipi?

Basi tulizungumza, akaomba msamaha na kuniambia hawatawasiliana tena. Lakini baada ya hapo ndipo ikawa shida tena ndani, kila kitu ni kugombana, kuninunia bila sababu. Alikuwa ananifanyia vituko mpaka nikagundua kuwa anatafuta sababu za kugombana ili tu tukinuniana awe bize kuchati na mwanaume wake. Ilifikia kipindi hali ilinichosha, nikamtafuta yule mwanaume kumuomba amuachie mke wangu, si ana mke wake bwana!

Hapo ndipo niliharibu, maana alinitukana sana, akanisema mambo mengi, lakini kubwa lililoniumiza ni kuniambia kuwa mke wangu ni mjamzito na mimba ni yake. Sikuamini kwani nikikumbuka juzi mke wangu ndiye aliyeniambia nimnunulie pedi, ujauzito unatoka wapi? Lakini niliporudi nyumbani kuongea na mke wangu, akaniambia ni kweli ana ujauzito wa miezi 3, lakini mimba ni yangu kwani hajawahi kulala na huyo mwanaume.

Nilipomuuliza kwa nini hukunambia, aliniambia sikujua, kwani bado nilikua naona siku zangu. Nilivyokuwa mjinga niliamini, ila mwezi uliopita mke wangu aliniaga anaenda kwao kujifungua.

Basi tukaongea vizuri nilitaka kumpeleka akaniambia Hapana nitaenda mwenyewe. Sasa juzi mama yake akanipigia simu kuniuliza kwa nini sijampeleka mke wangu kujifungua wakati tulishakubaliana hivyo. Nikamwambia mbona kaniambia anakuja huko! Basi katika kutafuta na kuhangaika, naambiwa mke wangu kaenda ukweni, yaani kwa huyu mwanaume, na huko ndiyo ameenda kujifungua na amebadili dini wamefunga ndoa ya Kiislamu.

Nilimtafuta, akaniambia ni kweli. Akasema nimeamua nisidanganye tena, huyu mtoto si wako, ni wa huyu mwanaume wangu. Nimeamua kubadili dini ili kufuata moyo wangu. Wewe ni mwanaume mzuri sana, ulinipokea na kunikubali na machungu yangu, naamini Mungu atakubariki na mwanamke mwingine.

Lakini mimi sasa ni mke wa mtu, endelea na maisha yako! Kwa kweli sijui nifanye nini, nimechanganyikiwa hata kutoka ndani nashindwa. Sijaweza kumuambia mtu yeyote hata wazazi wangu, siwezi kuongea nao
phd imegonga mwamba kwa mahusiano
na hujui cha kufanya. serious hujui cha kufanya. utakuwa umerogwa
wa darasa la saba B nakushauri move on , oa mwanamke mwingine maisha yaendelee
wanaume hatujilizilizi kisa mapenzi
 
Lakini mimi sasa ni mke wa mtu, endelea na maisha yako! Kwa kweli sijui nifanye nini, nimechanganyikiwa hata kutoka ndani nashindwa. Sijaweza kumuambia mtu yeyote hata wazazi wangu, siwezi kuongea nao

Simama,funga macho,vuta pumzi taaaaaaaratiiiiiiiibu Kisha fungua macho taaaaaaaratiiiiiiiibu,angalia anga, shusha kichwa angalia milima ,miti na miamba , (vitu vya asili tu)Kisha tafakari uzuri wake , utagundua huyo dada alikuja akuharibie mambo mengi,japo mchawi wa kwanza ni shangazi Yako, kuondoka kwa huyo dada unapaswa ushukuru sana, pia wake wa kulengeshwa ,walengeshaji Huwa ni jamii yenye agenda ya Siri ,na possibly hata ni chain ya uchawi, yaani shangazi Yako,mkweo na mkeo wote wanaweza kuwa wachawi hujui, fanya faster ufuatilie talaka mahakamani mana jamaa amekuibia mke, wakiwa na roho mbaya wanaweza mtumia kuja kuleta vurugu kwako coz Bado ni mkeo
 
Mleta mada,kwanini akili yangu inaniambia wewe haukusoma Uingereza?

Yaani hata mada sijaimaliza lakini kichwani kunalia alarm kwamba huyu mleta mada hiyo kwenda kusoma nje ameiweka tu kama kibwagizo asionekane hamnazo sana.
Ila watu jamani🤣🤣🤣
 
Ukweli ni kuwa ningemuacha lakini tayari tumeshaingia kwenye ndoa, tena ya Kikatoliki, utatoka vipi
Kama huwezi kutoka jinyonge ukufe.

Mimi hata kama ndo tumemaliza kula kiapo mbele ya paroko nikibaini Kuna uhuni Haina mjadala napiga chini.
Hapo ndipo niliharibu, maana alinitukana sana, akanisema mambo mengi, lakini kubwa lililoniumiza ni kuniambia kuwa mke wangu ni mjamzito na mimba ni yake. Sikuamini kwani nikikumbuka juzi mke wangu ndiye aliyeniambia nimnunulie pedi, ujauzito unatoka wapi? Lakini niliporudi nyumbani kuongea na mke wangu, akaniambia ni kweli ana ujauzito wa miezi 3, lakini mimba ni yangu kwani hajawahi kulala na huyo mwanaume.
Imavyoonekana hata huko UK ulienda kusomea ujinga na kutunukiwa PhD(Pengine hana Degree)ya ujinga
Mwanamke ukimfuma tu jua kabisa wewe hakupendi hata kama mwanzo alikuwa anakupenda vipi. Huwa hakuna mjadala ni kupiga chini tu maana ukijifanya kusamehe lazima ikugharimu tu ni lazima!
 
Hao wote ulio wataja ni kuwa sumbua tu mbona yeye hakutaka kuwaambia hao wote hata wazazi wake mbali kaenda Moja Kwa Moja ukweni?

Mwanaume lazima uwe na maamzi magumu ya kusonga mbele tu hao wote Kwa pamoja hawawezi lingana mawazo wapo watakaoshauri kuwa ni pepo tu limempata hivyo aombewe wengine watamwabia ashike ugoni maana Tyr anacheti Cha ndoa nk.

Kama hataki kumuacha huyo mwanamke afanye kama ulivyo shauri.

Wengine muda kama huu Kuna kimada ndani ananipunguzia stress
Pole kwa matatizo mkuu naamini hii story ni ya kweli na yamekukuta wewe.

Biblia inasema mke haachwi ila kwa zinaa tu. Kwa hiyo una kila sababu ya kumuacha na hamna kitu atafanya.

1. Shirikisha mshenga wako jambo hili na ataita pande zote mbili kumaliza hiyo ndoa.
2. Shirikisha viongozi wa kanisa lako ilipofunga ndoa uvunje hiyo ndoa.
3. Shirikisha wazazi wako.
4. Tafuta namna ya kusahau hilo jambo. Shiriki mazoezi, kuwa busy na kazi, nenda vacation n.k

NB: Hakikisha juu chini ndoa inavunjwa na mahakama na uwe una ushahidi.

Wazazi wake wanajua wanakuchezea shere tu.
 
Ahsanteni wote kwa salamu zenu za pole aisee! Na ahsanteni wengine kwa kunikejeli pia! Ila nasema hajawakuta tu ila siku yakiwakuta aisee!
 
Back
Top Bottom