Nifanyeje ili mbwa wangu wawe wakali?

Nifanyeje ili mbwa wangu wawe wakali?

Joined
Oct 6, 2024
Posts
147
Reaction score
303
Nimefuga mbwa wawili, kuanzia mwaka Jana, mbwa wangu hawabweki, hawana utisho, na wakiona mgeni huuficha mkia kwenye uvungu wa paja na kisha kakimbia kwenda kujificha.

Tabia ya mbwa hawa inanisikitisha sana na kunifedhehesha sana mtaani kwetu. Msaada tafadhali
 
1. Mlishe chakula Chenye pilipili kali.
2. Mfungie ndani muda mwingi isipokua muda ya ulinzi (wakati ninyi mmelala).
Huwa nawafungia ndani kuanzia saa 12/asubuhi hadi saa mbili usiku ndio wanatoka. Lakini ni waoga sana.

Je ni pilipili gani unayopendekeza niitumie, mwendokasi, pilipili nyembamba, pilipili kichaa, pilipili mbuzi, au pilipili manga?
 
Mfungie ndani asionane na watu muda wa mchana
Kufanya mbwa wako wawe wakali inaweza kuwa changamoto, lakini kuna njia kadhaa za kuwasaidia kuwa na ujasiri zaidi na kuwa na tabia za ulinzi:

Mafunzo ya Ulinzi: Tafuta mkufunzi wa mbwa ambaye ana uzoefu katika kutoa mafunzo ya ulinzi. Mafunzo haya yatawasaidia mbwa wako kujifunza jinsi ya kutambua na kukabiliana na vitisho.
 
Back
Top Bottom