Nifanyeje mke wangu aache kula kitimoto?

Nifanyeje mke wangu aache kula kitimoto?

Mimi ni Msabato kindakindaki. Nilibahatika kufunga ndoa na binti Mkatoliki, alihamia Sabato na akabatizwa ubatizo wa Kisabato.

Huyu binti ni mpigaji mzuri wa kitimoto, yaani balaa. Nimemwambia achana na hugo gudude ni gubaya.

Akaniahidi kuwa ameacha, lakini kila baada ya muda kidogo namkuta tena anakula gudude.

Je, nifanyeje aache kula hugo gudude?
Tumbo ni lako au lake? Pilipili ya shamba yakuwashia nini?
 
Tafuta majani ya mgomba mchemshie pamoja na nyama ya paka mwitu halafu mpe anywe mchemsho wake haitafika wiki ataacha.
Umesahau kumwambia achanganye na magadi ya mawe
 
Mimi ni Msabato kindakindaki. Nilibahatika kufunga ndoa na binti Mkatoliki, alihamia Sabato na akabatizwa ubatizo wa Kisabato.

Huyu binti ni mpigaji mzuri wa kitimoto, yaani balaa. Nimemwambia achana na hugo gudude ni gubaya.

Akaniahidi kuwa ameacha, lakini kila baada ya muda kidogo namkuta tena anakula gudude.

Je, nifanyeje aache kula hugo gudude?
Tatizo ume-base kwenye DINI (religious view) badala ya IMANI (spiritual view). Imani yake ndio itamfanya aache ila sio kinyume na hapo.
 
Tumbo ni lako au lake? Pilipili ya shamba yakuwashia nini?
Mke ni wangu au wako? Kati yangu na wewe nani anateswa na pilipili ya shambani?
 
Endele tu kumpa elimu ipo siku atakuelewa. Ila usitumie nguvu kumkataza
 
wanasema huyu mdudu nyama yake ina minyoo ambayo madhara yake hutokea baaday sana ,ingia Google utakuta sema mtu akishaonja ladha ya kitu kumrudisha ni kupunguza kasi ya kula
 
Back
Top Bottom