Nifanyeje mke wangu aache kula kitimoto?

Nitajie mnyama asiyekua
Kwani anakula nyama mbichi? Mbona hao tapeworm pia wanapatikana kwa ng'ombe na hamleti hayo mabango yenu?
 
Wataalamu uchwara hao maana hao minyoo wanapatikana hata kwa ng'ombe ila wao kampeni yao ni against nyama pendwa Tu😄
 
Acha ujinga wewe. Huo ni upumbavu wa hali ya juu unaotaka kufanya.

Kitimoto hakina shida yoyote, kama wewe huli basi baki na ujinga wako.

Halafu ni ujinga wa hali ya juu kumlazimisha mtu afuate imani yako ya kidini.
 
Kama wewe huli, Baki mwenyewe usile, Usifosi na kulazimisha na mwenzako asile kwa kigezo cha Dini.
 
Kama vipi achana nae tu, kama umeshindwa kuvumilia hiyo karaha.
 
Umenipa hamu, naenda kutafuta kiti moto, ni nyama nzuri sana, muache kwani ni chaguo lake nawe tafuta chaguo lako. Hakika Mungu alituandalia kitoweo kizuri sana. Mungu wa Wasabato na Wakatoliki ni mmoja, muache apige kiti moto.
 

Ni mkatoliki ndo sababu, mwache ale, sio msabato, alibadilika ili umuoe!
 
Ni mkatoliki ndo sababu, mwache ale, sio msabato, alibadilika ili umuoe!
Upo sahihi, kuitoa imani ya mtu aliyelelewa nayo ni ngumu sana..Nilipata binti wa kiislam ila kabadili dini kwa maneno yake.

Ila bado ana zile mambo za uisalm, japo anasema kwa sasa ni mkristo na kanisani anaenda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…