Nifanyeje? Mpangaji mwenzangu amekuwa ombaomba sana mpaka kero

Nilishawahi wafanyia hivo, wanapumzika siku 4 au 5.
Ya sita hawa hapa
Tupo kwenye hali moja.
Niko jirani na single maza mmoja hivi hadi namhurumia tu.

Anaomba huyo hadi huruma.

Ana watoto kama saba hivi, sema yeye amepanga nyumba ya vyumba vitatu..

Nikimnyima kitu utasikia maneno excel hanipendi, mara nanuniwa na Familia nzima.

ana binti wa miaka 18
 
Nakazia
 
Bora wewe unaombwa na wapangaji wenzako, kuna kipindi naishi Kijitonyama ilinibidi niikimbie nyumba niliyokuwa napanga. Mtoto wa mwenye ile nyumba ni Mama mwenye watoto 4 na kila mtoto ana baba yake, yule mdada pamoja na wanawe kwa kweli ni kero. Wanawe wote waliacha shule ili wakae tu kijiweni, kwa kipindi naishi pale wote walikuwa nyumbani hawana hili wala lile na cha kushangaza eti wameoa na wanaishi nyumba hiyo hiyo ya babu yao. Nilikuwa najiulizaga mno kila niwaonapo wale wasichana walioolewa na wale vijana, je huko makwao ni kwamba maisha yao yalikuwa duni kiasi hiki mpaka kuamua kuja kuolewa na hawa vijana wasio na hili wala lile kweli?
Basi yule mdada akawa anawatumia vijana wake kutongoza wasichana wa kazi wa wapangaji wao ili maboss zao wakienda makazini wawe wanaomba vyakula vya kupika na wakawa wanafanya hivyo kweli na kufanikiwa. Wapangaji wengi baada ya kugundua hivyo walifukuza wafanyakazi wao na kuhama pale. Nyumba haina maji na kila siku wanakatiwa umeme kwa sababu hawana hela ya kulipia. Kwa matatizo haya, vijana wa yule Mama wamekuwa vibaka kupitiliza. Wanatumia marafiki zao kukaba wapangaji wao na majirani. Kila mtu mtaani anawacheka na kumshangaa yule dada kwani hata naye pia hana issue, inabidi achakalike yeye ili vijana wake na wajukuu waweze kula.
Ilikuwa kila ninaporudi kazini wale vijana wananifuata chumbani kwangu kuja kuniomba hela au chakula wakidai eti shemeji zangu (wake zao wasio na uhusiano na mimi) wana njaa, nilikuwa nawatolea nje wanakasirika na kunitafutia visa ili tu tugombane na wanifanyizie mtaani. Nyumba ile haikai na wapangaji maana kila anayekuja anapatwa na kero hizo hizo, vijana hawataki kufanya kazi, wao kazi yao kubwa ni kukaa kijiweni tu kubishana juu ya Simba na Yanga au Ali Kiba na Diamond siku nzima huku Mama yao akibangaiza kutafuta chakula.
 
bila kujali mwonekano na umri wake umkule halafu sitisha misaada, we siyo UN
 
 
 
Kama Haina madhara makubwa kwenye uchumi wako saidia bila kuchoka mbegu unayopanda kuna siku itazaa matunda
 
Wape kwa uwezo wako hiyo ni sadaka safi mbele za Mungu, maisha ya Dar es Salaam ni magumu ukichukulia tena mzigo wa kulea watoto wa 5 sio mchezo.
 
Uwezo kama upo wape utaendelea kubalikiwa ila kama uwezo haupo yaani kama ni mdogo achana nao waambie ukweli
 
hama kabla hujapata stroke man!!
 
Sio zote kuna mabachelor pia wanaomba. Kuna mabachelor hata ufagio hana au hata ndoo ya kuogea hana ukikaa vibaya sabuni wanashare yako so ni tabia tu ya mtu
Huyo bachelor hata kumchana si unamchana tu, ishu ya mleta uzi ni hao watoto.

Ukimkazia maza anatuma watoto, binadamu kikawaida tuna huruma kwao, mleta uzi ndio anategwa hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…