Kwanza nikusahishe tu, Huo sio ushirikina bali ni mambo ya tamaduni zetu za afrika, Mfano Mkwawa alikuwa na wake 15 hivi, Alikuwa na mtambo wake kumgundua aliechepuka, Nenda makumbusho ya Kaelnga utapewa full story 🙂🙂
Ok, back to the topic, Huyo mme wako inaonekana nae wamemmegea kateknolojia ka kudukua ama kuhack mawasiliano yako kwa njia za asili kabisa, ni heri mtu adukue simu yako kwa teknolojia ya mzungu kuliko mtu akudukue mawasiliano yako kwa njia asili, hata kufeki hautaweza.
Haijalishi una elimu gani au cheo kipi, mwenzio kashakuzidi nguvu huyo, ukae kwa kutulia bila kumkwaza, endelea kuufaidi utimamu wako kihisia lasivyo anaweza kukuchapa limbwata usione wengine zaidi yake,
Labda cha kukusaidia tu utupe kabila lake, kuna makabila mengine mbinu zao zinajulikana na zinaweza kuwa unlocked, Hivyo ingependeza uelezee katokea wapi.