Nifanyeje nimpende mama yangu hii kitu inanitesaa saana msaada

Nifanyeje nimpende mama yangu hii kitu inanitesaa saana msaada

binadamu bhana kwavile wapo wa kukudhika mkono unaona inatosha ngoja Mungu aje akuoneshe nafasi yake kwako katika maisha yako ndo utajua mti lazima uwe na matawi ndio utaleta matunda mazuri usijifanye kenge sasa, na utaona aibu mwenyewe moyoni mwako.
 
Wakuu kwema?

Kuna jambo limekua likinitafuna kwa miaka mingi saana kuhusu mimi na mama yangu sina hata chembe ya upendo nae ila hela namtumia namsaidia kwa maana ni Maskini samahani kwa kusema hivi.

kwa kifupi kabisa mimi nimetoka kwa mama yangu nikiwa na umri wa miaka 3 nakuja kuonana na mama yangu nikiwa na umri wa miaka 19 kwa kipindi chote hicho mama yangu sikuwahi kumuona wala kusikia sauti yake siku nakutanishwa nae nilishindwa kufahamu mama mkubwa ndo alinitambulisha.. hakuwahi kunilipia ada, hakuwa kunipa hela ya yoyote .

Mimi nimelelewa na Bibi yangu na baba nampenda saana bibi yangu kuliko mama yangu mama yangu huwa ananipigia simu analalamika kwa nini simpigii simu? nakosa cha kumjibu namuomba tuu msamaha natamani kumpenda ila nashindwa naombeni msaada kama naweza kuwa na upendo na mama yangu

Asanteni.
tumeamrishwa kuwaheshimu wazazi wetu. hilo ni agizo. wewe mheshimu tu
tena haya maislam yenyewe yanakuambia mama ni muhimu zaidi. ukimsonda na kidole hicho kidole kinatakikana kukatwwa. they are very serious linapokuja suala la mama
 
Haya ni mambo binafsi sana, kila mtu ana watu anaowapenda na kuwachukia
 
Nadhani hapa wengine mmejibu tu kwa mihemko,huyu bwana sio kama ana chuki na mama yake,ndio maana hakutaja mapungufu yake,anachoelezea yeye ni ile hali ya upendo ambao umepotea kutokana na yeye kukuzwa na bibi.Hii pia huwapata wale wanaokuzwa na mama peke yake,kiwango cha mapenzi kwa baba huwa ni kidogo,kwahiyo cha kufanya ni kuendelea kujilazimisha tu,ingawa hiyo kitu haitafanya uwe na upendo mwingi kivile kwakuwa hiyo hali huwa inajengeka tokea utotoni...
 
Kumpenda mtu ni hisia "Feeling" wewe huna hisia na Mama yako coz hakuishi na wewe,huna hisia nae,

Inaonekana kulikua na matatizo kati ya Baba yako na Mama yako,bila shaka waliachana ukiwa mdogo sana,

Sasa,ugomvi wa wazazi wako,wewe haukuhusu,hakuna umuhimu wa wewe sasa hivi kujua nini hasa kilitokea,kua karibu na Mama yako na utaanza kua na hisia nae kisha utampenda,kama una kwako,mchukue Mama yako uishi nae,kumtumia tu hela haitoshi,mzazi huhitaji upendo toka kwa mwanae,

The way utakavyodeal na Mama yako basi tegemea na watoto wako watadeal na wewe hivyo hivyo,bado hujachelewa,do something ili uwe karibu na Mama yako,upendo utakuja wenyewe tu,it's a self control.
Umekurupuka,hujaelewa andiko la huyu mtu.
 
Hii pia itakuja kuwatokea wale wazazi wanaopekeka watoto wao shule za bweni wakiwa wadogo mpaka wanaenda vyuoni.
 
malezi mama yangu hakuwa na maisha mazuri..
Si bure wewe una laana. Ungesema alikutelekeza,ningekuelewa. Kama alishindwa kukulea kisa maisha magumu,akapata wa kumpiga kampani,hao ndo wenye makosa. Huenda hata nauli ya kukupeleka kwake au yeye kumleta ulipolelewa,alitegemea apewe,na hakupata wa kumpa. Leo hii,eti sina upendo na mama. Kumtumia,ni ishara kuwa wewe umejipata na msaada bado anategemea kwa watu. Sasa, ulitaka afanyeje? Kwani yeye hakupenda kujilelea? Una tatizo si bure wewe. Ukute umejiona unakaa geto,midemu inapishana,pengine anasubiri umjengee msingi wa maisha,simu zake unaona kero. Pole yako.
 
Wewe ambaye hujakurupuka na umeelewa andiko,uko wapi huo mchango wako kwa mleta mada?

Anyway mimi mchango wangu ni kwa watu wenye uelewa na sio kwa watu wa aina yako
Soma andiko namba #28 la stephot ndio nilichoomasnisha acha kukurupuka
 
Kuna watu wamezaliwa hawawajui mama zao!. We leo hii unamchukia mama ako na husemi chanzo ni nin mpaka kumchukia we una matatizo binafsi ndugu!..


Au maelezo hayajakamilika kuna jambo hutaki Kuliweka sawa ila sio kumchukia maza kisa hujaishi nae kwa muda mrefu
Kusema tu mama yake masikini sana,na yeye leo hii anapata chochote,hujaona kasoro? Limbukeni tuu
 
Amri Kuu UPENDO.
Japo Wazazi wetu wakati mwingine huwa wanatuumiza sana. Lakini ndivyo ilivyo na hiyo ndio mitihani ya ulimwengu. Itafute nguvu ya kumpenda huyo Mama yako.
Nilishawahi kuandika uzi humu jinsi Mama alivyonitimua nyumbani kisa mdogo wangu niliyemsomesha kapata kazi na Mimi nilipoteza kazi kutokana na kupata ajali iliyonisababishia matatizo ya kiafya kwa miaka miwili na miezi 7
 
Ushatupa jibu. Humpendi kwa sababu NI MASIKINI
 
Back
Top Bottom