Nifanyeje nimpende mama yangu hii kitu inanitesaa saana msaada

Nifanyeje nimpende mama yangu hii kitu inanitesaa saana msaada

Wakuu kwema?

Kuna jambo limekua likinitafuna kwa miaka mingi saana kuhusu mimi na mama yangu sina hata chembe ya upendo nae ila hela namtumia namsaidia kwa maana ni Maskini samahani kwa kusema hivi.

kwa kifupi kabisa mimi nimetoka kwa mama yangu nikiwa na umri wa miaka 3 nakuja kuonana na mama yangu nikiwa na umri wa miaka 19 kwa kipindi chote hicho mama yangu sikuwahi kumuona wala kusikia sauti yake siku nakutanishwa nae nilishindwa kufahamu mama mkubwa ndo alinitambulisha.. hakuwahi kunilipia ada, hakuwa kunipa hela ya yoyote .

Mimi nimelelewa na Bibi yangu na baba nampenda saana bibi yangu kuliko mama yangu mama yangu huwa ananipigia simu analalamika kwa nini simpigii simu? nakosa cha kumjibu namuomba tuu msamaha natamani kumpenda ila nashindwa naombeni msaada kama naweza kuwa na upendo na mama yangu

Asanteni.
Bond na MTU inatengezwa.
Anza kutengeneza bond na mama yako.
Km una kwako mchukue ukae naye then utaanza kumpenda.
 
Nje ya mada kidogo.
Kuna watoto na vijana wengi wamekosa upendo wa wazazi wao kwa sababu mbalimbali.
Ukiwa na uwezo wa kuwaonyesha upendo fanya hivyo tuu.
Kuna mwl mmoja Ni above fifty,Hana mtoto wa kuzaa Wala hajaolewa,yeye amekuwa akuwafariji Sana wanafunzi mayatima kwa kuwapa mahitaji yao mbalimbali.
Mwisho wa siku amemchukua mmoja nyumbani kwake na anamsomesha.
Yaani ukiwaona utafikiri Ni mtoto wa kumzaa jinsi wanavyopendana.
Hivyo kila kitu Ni kutengeneza bond tuuu.
Mkuu km una kwako mchukue mama ukae naye,baada ya muda utaanza kumpenda zaidi
 
Wakuu kwema?

Kuna jambo limekua likinitafuna kwa miaka mingi saana kuhusu mimi na mama yangu sina hata chembe ya upendo nae ila hela namtumia namsaidia kwa maana ni Maskini samahani kwa kusema hivi.

kwa kifupi kabisa mimi nimetoka kwa mama yangu nikiwa na umri wa miaka 3 nakuja kuonana na mama yangu nikiwa na umri wa miaka 19 kwa kipindi chote hicho mama yangu sikuwahi kumuona wala kusikia sauti yake siku nakutanishwa nae nilishindwa kufahamu mama mkubwa ndo alinitambulisha.. hakuwahi kunilipia ada, hakuwa kunipa hela ya yoyote .

Mimi nimelelewa na Bibi yangu na baba nampenda saana bibi yangu kuliko mama yangu mama yangu huwa ananipigia simu analalamika kwa nini simpigii simu? nakosa cha kumjibu namuomba tuu msamaha natamani kumpenda ila nashindwa naombeni msaada kama naweza kuwa na upendo na mama yangu

Asanteni.
Msamaha una nguvu kuliko chochote.. Mtafute muongee wawili tuu.. Kuna vitu hujawahi kuambiwa popote na yeyote .. Ila yeye atakuambia .. A VERY SAD UNTOLD STORY🤔😪
Ndiye mamaako mzazi pekee.. Nje yake hakuna mwingine.. Mtafute muongee
 
Unakiri kuwa uliondoka sababu ya umaskini, halafu eti hakukulipia ada? Wewe mpaka unafikisha 19 yrs huko ulikokuwa unakaa walikwambia kuwa una mama? Ulifanyaje? Zaidi ya kukosekana bond kati yenu una sababu nyingine ya kumchukia. Mpende tuu, ikiwa unaweza mpenda mtu baki huwezi shindwa mpenda mama yako mzazi.
 
Pole Mkuu siyo tatizo lako! Uliachwa bila malezi ya Mama ukiwa mdogo mno!
Mimi ningependa kujua kama Baba yako na Mama yako wanaishi pamoja.
Kama waliachana Mama anaishi na mwanamme mwingine? au Baba ana mke mwingine?
Lakini pamoja na yote,hata kama humpendi Mama,mheshimu tu! msikilize,mtembelee,msaidie pale ambapo inawezekana!
Hiyo ni Moja ya Amri 10 za Mungu-"
(Kutoka20:12)-Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.
Mama ni Mama hata kama angekutupa Jalalani.
 
Kwa maelezo yako mama yako ni victim tu wa hali halisi ya maisha uliyozaliwa nayo, thats why mama alikubali ukalelewe kwa bibi yako kwani aliamini huko utapata mahitaji muhimu katika makuzi yako ambayo yeye asingeweza kukupatia. Shida iko kwa baba yako na bibi yako ambao hawakuwahi kukwambia ukweli kwanini upo hapo kwa bibi na sio kwa mama.
Kuna watu toka wazaliwe walipotezana na mama zao na kwa bahati wanakuja kukutana wakiwa watu wazima sana na bado wanajega bond ya upendo wa mama na mwana sembuse wewe uliyekuwa unajuwa mama yuko sehemu furani na maisha yanampiga kiasi gani. Ebu changamka kabla hujachelewa mtafute mama mpe muda ongea naye afunguke utampenda na kumwonea huruma na hautajutia kwa kufanya hivyo.
 
Hii pia itakuja kuwatokea wale wazazi wanaopekeka watoto wao shule za bweni wakiwa wadogo mpaka wanaenda vyuoni.
Hii ilishamkuta jirani yangu, aliwapeleka watoto wake wawili wa kike na wa kiume kusoma Uganda toka wakiwa chekechea, sasa sababu ya kutokuhudhulia sana zile visiting day sababu ya kazi na umbali watoto wakajenga chuki zidi ya wazazi wao. Ikafika siku wazazi wote wawili wakajikusanya na kwenda kuwatembelea shule. Watoto wengine wanatoka mbio kuwafuata wazazi wao kwa shauku na furaha kuu, ikafika zamu ya wale watoto wa jirani yangu kuambiwa kuwa wazazi wenu wameshafika njooni mkawasalimie watoto wakatoka zao nje taratibu na kusimama kwa mbali wakiwaangalia wazazi wao kama vile hawawajuwi mama akajaribu kuwaita kwa ishara na kwa kuwaita majina lakini wapi watoto wanawaangalia tu then wakaondoka kwenda kucheza na watoto wengine ambao wazazi wao hawajaja, mama yao alipiga uwiiii ya nguvu na kuwafuta kwenda kubebeleza mpaka walimu wakaingilia kati. Mwisho wa siku mama aliondoka na watoto kurudi bongo.
 
Mimi nimeishajifunza,siwezi kupeleka watoto shule za bweni
 
Back
Top Bottom