Nifanyeje nimpende mama yangu hii kitu inanitesaa saana msaada

binadamu bhana kwavile wapo wa kukudhika mkono unaona inatosha ngoja Mungu aje akuoneshe nafasi yake kwako katika maisha yako ndo utajua mti lazima uwe na matawi ndio utaleta matunda mazuri usijifanye kenge sasa, na utaona aibu mwenyewe moyoni mwako.
 
tumeamrishwa kuwaheshimu wazazi wetu. hilo ni agizo. wewe mheshimu tu
tena haya maislam yenyewe yanakuambia mama ni muhimu zaidi. ukimsonda na kidole hicho kidole kinatakikana kukatwwa. they are very serious linapokuja suala la mama
 
Haya ni mambo binafsi sana, kila mtu ana watu anaowapenda na kuwachukia
 
Nadhani hapa wengine mmejibu tu kwa mihemko,huyu bwana sio kama ana chuki na mama yake,ndio maana hakutaja mapungufu yake,anachoelezea yeye ni ile hali ya upendo ambao umepotea kutokana na yeye kukuzwa na bibi.Hii pia huwapata wale wanaokuzwa na mama peke yake,kiwango cha mapenzi kwa baba huwa ni kidogo,kwahiyo cha kufanya ni kuendelea kujilazimisha tu,ingawa hiyo kitu haitafanya uwe na upendo mwingi kivile kwakuwa hiyo hali huwa inajengeka tokea utotoni...
 
Umekurupuka,hujaelewa andiko la huyu mtu.
 
Hii pia itakuja kuwatokea wale wazazi wanaopekeka watoto wao shule za bweni wakiwa wadogo mpaka wanaenda vyuoni.
 
malezi mama yangu hakuwa na maisha mazuri..
Si bure wewe una laana. Ungesema alikutelekeza,ningekuelewa. Kama alishindwa kukulea kisa maisha magumu,akapata wa kumpiga kampani,hao ndo wenye makosa. Huenda hata nauli ya kukupeleka kwake au yeye kumleta ulipolelewa,alitegemea apewe,na hakupata wa kumpa. Leo hii,eti sina upendo na mama. Kumtumia,ni ishara kuwa wewe umejipata na msaada bado anategemea kwa watu. Sasa, ulitaka afanyeje? Kwani yeye hakupenda kujilelea? Una tatizo si bure wewe. Ukute umejiona unakaa geto,midemu inapishana,pengine anasubiri umjengee msingi wa maisha,simu zake unaona kero. Pole yako.
 
Wewe ambaye hujakurupuka na umeelewa andiko,uko wapi huo mchango wako kwa mleta mada?

Anyway mimi mchango wangu ni kwa watu wenye uelewa na sio kwa watu wa aina yako
Soma andiko namba #28 la stephot ndio nilichoomasnisha acha kukurupuka
 
Kusema tu mama yake masikini sana,na yeye leo hii anapata chochote,hujaona kasoro? Limbukeni tuu
 
Soma andiko namba #28 la stephot ndio nilichoomasnisha acha kukurupuka
Sasa hapa huoni kua wewe ndiye unayekurupuka? hujui hata umemquote nani,

Comment 29# huoni kua umeniquote mimi? kunywa japo maji baridi upate nafuu.
 
Amri Kuu UPENDO.
Japo Wazazi wetu wakati mwingine huwa wanatuumiza sana. Lakini ndivyo ilivyo na hiyo ndio mitihani ya ulimwengu. Itafute nguvu ya kumpenda huyo Mama yako.
Nilishawahi kuandika uzi humu jinsi Mama alivyonitimua nyumbani kisa mdogo wangu niliyemsomesha kapata kazi na Mimi nilipoteza kazi kutokana na kupata ajali iliyonisababishia matatizo ya kiafya kwa miaka miwili na miezi 7
 
Ushatupa jibu. Humpendi kwa sababu NI MASIKINI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…