Nifanyeje nizoeane na majirani?

Tofauti na huko mbele, huku kwetu ukimkaribisha jirani kwako pamoja na kufaidika kwa fadhira zako, anatumia ku-scan nyumba yako nje ndani badala ya siku kadhaa unapata ugeni wa majambazi usiku mwigi.😀
Hahahha anakutumia wazee wa kazi
 
Hahahahah alijiona star wakati kapanga uswahilini?
 
Utakuwa mtu wa ibada sana bila shaka
 
Nilifahamiana na jirani yangu salun baada ya mwaka tena bint yangu mdogo ndio alitutambulisha, tukaelewana Sana si Kwa kutembelea Ila ikitokea kitu mtaani tunaambizana, kuna siku niliona turubai nyumba ya tano au ya sita kutoka kwangu nikavaa kanga nikaenda japo na wenyewe siwajui nikaingia ndani na kuuliza hilo turubai kuna nini? Wakanijibu kulikuwa na msiba siku tatu zilizopita nikawaomba msamaha kwamba sikujua wakajibu hata jirani yako Hana habari maana hatujamuona nilipitia nikamuonyesha turubai alistuka nikamweleza akaenda kutoa pole. Napenda MAISHA haya tujuane shida, Raha wabiki nayo wenyewe
 
Hahahaha..that's true
 
Njia rahisi ni kutembelea vijiwe ambavyo unadhani utakutana nao! Kama kuna Car wash mtaani jimix hapo weekend nunulia vijana soda mpige soga! Kama kuna ka duka mahali unaweza pata hata mtindi ukawa unapiga piga story na watu maeneo hayo! Kama ni mtu wa dini jiunge na jumuiya uwe unakutana na wenzio kila weekend.
 
Being genuine, being you.
Watu wanaogopa msiba kwamba utazika mwenyewe, mimi nakataa. Mtu anaenda kwenye msiba kwa sababu ya heshma ya marehemu na sio vinginevyo, haya mengine ni 'socialist way of life' ni uamuzi wako na 'perception' yako.
Naonaga misiba ya kimagharibi kwenye runinga, unakuta padri/mchungaji na wanafamilia ndugu na watu wa karibu hawazidi 20. Ukiona msiba una watu wengi basi marehemu ni mtu maarufu.
Muda unakwenda na maisha yanabadilika kwa kasi sana, tamaduni zingine nazo zitabadilika pia. Mfano sasa hivi serekali inataka watu wakazikwe kwenye makaburi ya uma na sio kwenye miji yao
 
msizoeane sana, jitahidi ukikutana nao salimia kwa unyenyekevu, ikiwezekana unashuka kwenye gari unawasalimia unaendelea na mmbo yako, hakikisha hamzoeani sana,na ukisikia kwa jirani kuna tatizo nenda kamsaidie endelea na mambo yako!!
 
Tatizo tunaogopana sana.
Watu wanaweza wakakuogopa kwa class uliojiweka ila ukiwa bro mchangamfu hata vijana watakupenda tu hapo mtaani! Weekend egesha hata car wash, tia nao strory mfano kuna mwana ni engineer life safi ila anachezaga draft na wana kitaani tu on weekends. Anazungusha kahawa bill kwake maisha yanaenda na anajulikana freshi!

Watu wakuzoee ila sio ile sana mpaka mtu anajua unafanya kazi wapi! Anajua una asset au biashara gani beyond ambavyo alitakiwa akufahamu inaletaga dharau at last. Mie hiki ndio sipendagi
 
Eid ya keshokutwa kagonge maget yao uwaalike hata wasipokuja watakuona na watauthamini utu wako kwahiyo hata ukiwa na shda unaweza kuwaomba msaada au wao kukuomba msaada
 
Kuogopana ninakozungumzia ndio ile ukikaribisha jirani ataleta wezi,mara utalogwa,wataleta dharau yaani binadamu tunaogopana sana
 
Kama vipi na huku jamii Fulani atokemo ili asiingiliane na watu kwa stori ama kubadilishana stori mbili tatu.
Yeye si anaweza kuishi bila watu tuone Sasa.ulaya watu wanaugua Sana sijui Nini ule ugonjwa may be sonoma.mtu Ana socialize mtandaoni Ile live kabisa na watu hakuna kitu. Na binadamu tunahitaji binadamu wengine Ile live la sivyo ufanye hata mapenzi kidigital tuone.fanya party YouTube tu view tu comment,
Hata kanisani hudhuria tu kwa tv sadaka tuma mpesa.
Funga mdomo wako bila kuufungua kwa binadamu mwenzako tuone Kama wewe ni peculiar species.
Kuna sex phone,pia yaani life ni watu.
Mie nashukuru napita ni salamu tu na karibia wote ni mageti, nimekuwa wa kwanza kuleta umeme huu mtaa,simu wanaleta nawachajia,wakiwa wanachomelea mageti Yao umeme nawapa sema wananunua luku waliyoitumia wanaiweka wanatumia,
Maji tunapata once per week Nina tank wasio na tank wakiishiwa wananiomba nawapa.binafsi nafurahi Sana kuishi vizuri na kusaidiana na majirani vidogo vitu. Ila tu mazoea sio Sana kivile,yupo nikiyekuwa naazima jembe na ngazi, jembe baadaye nikanunua.
Mie ni watu bila watu mie sipo
 
Mkuu watu ambao hatuna mazoea na wengine huwa tunadhani hawa wengine hawatuoni kumbe wanatuchora tuuu.

Ulichosimulia kimenikuta na mimi...


Kuna siku nilienda dukani kuulizia kitu flani hapa ahpa mtaani,sasa nikaambiwa kile kitu hakipo,

yule muuzaduka kumbuka kuwa simjui jina ila tunajuana kwa sura tu

Basi wife akaenda baadae kuulizia tena kile kitu alafu alikuwa amevaa nikabu(ninja) katika duka lile lile.

Muuza duka akamuambia "hiki kitu sina na mumeo katoka kuulizia muda sio mrefu"

Wife alichoka akasema wamejuaje kuwa mimi na wewe ni wanandoa wakati ni mara chache mno huwa tunafuatana tena tukifuatana basi tunaenda safari na sio kuzunguka hapa mtaani na ajabu zaidi wife huwa anavaa ninja mara nyingi lakini bado wakamjua kwamba huyu ni mke wa safuher.

Hivyo mtaani watu wanakuchora tuu unaweza dhani hawana deta zako zozote vile wanavyojikausha ukiwa umekutana nao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…