- Thread starter
- #201
Asante sanacrushed kuna aliekushauri kujikita sana katika maombi. Kiukweli na mimi nasupport kama mdau wa wanawake kusimama katika imani. Sina experience sana kwenye hii sector lakin kwa machache ninayoyajua.. you need peace right now. Kweli umeshasacrifice sana kwa ajili ya mume wako na too bad inataka kukurudi vibaya. The time, efforts, love involved inakuumiza sana. Hasa kama wewe unasimama katika nafasi yako.
Neno la Mungu linasema "kila jaribu lina mlango wa kutokea (1 Kor 10:13)." Haya mambo sometimes yanatutokea ili kupimwa namna tunavyoweza kusimama na kumuamini Mungu. Your Faith is being tested. Ninachoweza kukushauri...Kwanza omba Mungu amuondoe mumeo moyoni mwako. And mnyang'anye mmeo moyo wako. Its a very hard statement lakin sina namna ya kuandika. Mungu kasema tumpende kwa Moyo, Roho, Akili na Nguvu zetu zote. Ni muda mzuri umepata wa kuwa addicted to God. Lets be addicted to seeking the Kingdom of God. Simaanishi umuignore ama umdharau. Utakuwa humpendi Mungu. Namaanisha tuanze sasa kusoma scriptures kama machizi. Umepata a very great time ya kutengeneza uhusiano binafsi na Mungu.
Usimuangalie mjamaa maana hutaweza kusimama. Afu pia tafuta foundations ambazo huwa zinapenda kutoa misaada. Charity groups labda. Jiunge nazo. Weekends kama huna ratiba kazini ama vikoba unashughulikia nyumba yako. Unawapikia watu chakula kizuri. Unakuwa busy inshort. Ndo unajikita katika utoaji mara kwa mara. Ukienda kutembelea hospitals, yatima, wazee, wajane sikufichi akili yako itahama kabisa kwa huyu anaekutatiza. Maana hata yeye ni shetani anampepeta. Hate the devil behind him do not hate him. Maana shetani anapenda kuiba, kuharibu na kuchinja. Lakin nakuamin unaweza kusimama na kuomba kupambana nae.
Wanaowindwa si wewe wala mumeo, wanaowindwa ni uzao wako uishi maisha ya mara leo kwa baba mara kwa mama. Inatengenezaga bad psychology ni basi tu sometimes wengne inawabidi. Adui anataka kukupokonya nafasi ya mke na ni wajibu wako kukataa. Ombea nafasi yako kama mke..tena nakupa tip..jifunze kuamka saa tisa usiku kuomba. Maombi ya usiku yana nguvu sana. Ask the Holy Spirit akusaidie maana we mwenyewe hutaweza. Lakin nikutie moyo kwamba Ndoa yako inapona kabisa..wala haina shida iyo. Ni shetani anataka kucloud your judgement ili uamue kwa hisia. You are a strong woman..najua unaweza kusimama na kumpiga huyo bata!