Nifanyeje wanangu wawe na akili nyingi darasani

Nimeipenda hii
 
Nimeipenda hii
 
Nimeipenda hii
 
Mtu kaomba ushauri, kama huna ushauri kaa kimya, sasa mkianza kubishana inamsaidiaje mleta mada?
 
HAHAHAHAH! Such a funny story.
 
Muda wao bado. Tunaita kufunguka kwa akili. Kuna watoto hufunguka wakiwa form 1-4, kila mtoto ana muda wake wa kufunguka.
Mie mtoto wangu drs 4 alikuwa anakuwa wa 50. Sasa amekuwa wa 19. Nahisi nilimuwahisha sana shule, alianza drs la 1 akiwa na miaka 4.5.
Kuna mkufunzi alisema yeye mtoto wake kitendo cha kujua kusoma ma kujitambua basi ni kipimo tosha kuwa mtoto wake anafanya vizuri bila kujali anakuwa wa ngapi.
Wengi wamekariri kuwa kufanya vizuri mtoto awe wa 1-10.
Watoto wapo ktk ukuaji wasilazimishwe matakwa yetu.
 
Sijaona neno LISHE BORA.
 
kwanza nimesoma kila comment kwa utulivu mkubwa kana kwamba ndio mtaka ushauri

Nianze kwa kupinga kwamba mtoto anarithi akili za baba au mama,sio sahihi,kwasababu tunakuja watupu kabisa ila tunapata maarifa kutokana na mazingira yanayo tuzunguka

Ila je ni kwa kiasi gani huyu mama au baba anatengeneza mazingira mazuri ya watoto kusoma? mfano wa kweli kabisa kutoka kwa mama yangu mdogo mke wa pili wa baba,huyu hakusoma kwahiyo hata umuhimu wa elimu haujui,kipindi ambacho baba analala kwa mama yangu,kule kwa mamdogo watoto wanaangalia movie za kinigeria dstv mpaka saa nane usiku,hapa mama huyo hakuwa mlezi mzuri,matokeo yake watoto wanapelekwa shule na dereva wanasinzia,mpaka walimu wakawa wanamuuliza driver inaelekea hawa watoto hawalali

Kwahiyo hapa ni mzazi kutowapa watoto malezi mazuri,,,nawapa mfano mwingine Ben Carson bingwa wa operesheni wa ubongo na mtunzi wa kitabu cha gifted hands,alikuwa na mama ambaye ni house girl kwa wazungu,na Ben hakuwa vizur darasani lkn kwakuwa mama alikuwa anaona maboss wake wana utaratibu wa kusoma vitabu basi akaanza kuleta utaratibu huo kwa watoto wake na kuwasimamia kila wiki lazima wamalize kitabu kimoja,matokeo yake watoto walibadilika na kuwa wazuri darasani

Naona mmeona mazingira mawili kwa mama wawili ambao hawajasoma lkn walitumia mazingira tofauti kuwalea watoto wao,,kwahiyo ufahamu wa watoto hauhusiana na kiwango cha elimu cha wazazi

Pili wakati mwingine lishe nayo uchangia kama walivyosema wengi hapo juu,,na sababu nyingine huenda labda kuna udumavu ulifanyika toka wakiwa tumboni kwahiyo wanakuwa slow learner

Kikubwa kama walivyosema wadau wengi badilisha approach kutoka kuwapiga na kuwasapoti na kuwa rafiki bora kwao,wape nguvu kwa maneno mazuri waambie wana akili kama watoto wenzao,wanweza kuwa katika nafasi nzur,waambie uko proud kwao na unaamini katika uwezo,,yaani wape moyo na waonyeshe wanaweza,trust me unaweza kuja kushangaa kitakacho tokea

Na jifunze kuwaelewa wakati wanapitia katika changamoto hiyo,,tatizo wengi wetu tunataka watoto wawe kama wewe ulivyofanya zamani kitu ambacho si sahihi,kumbuka mazingira ni tofauti na uwezo wa ufahamu ni tofauti
 
Watoto wengi hawapati muda wa kucheza na kufungua akili zao.

Pili watoto wengi bado hawana exposure na mambo yanayowazunguka,akili zao ni ngumu kufunguka.

Kama wewe unampeleka mtoto darasa la kwanza akiwa na miaka mi4 jambo ambalo ni ukatili kwa mtoto na kumnyima haki yake ya msingi ya kucheza na kufurahia maisha,wakati huo pengine wewe ulianza shule ukiwa na miaka 7,ulipata muda mzuri wa kucheza.


Lakini jambo lingine ni watoto wanakitu inaitwa ADHD yaani wanashindwa kuwa makini na wanakuwa na tatizo la kuwa na shughuli nyingibza mwili ama michezo mingi au kukosa utulivu.
 
Mkuu haukukosea kujiita andrew tate maana umeelezea hii inshu kwa undani kabisa na uhalisia wake kama ambavyo the Top G alivyo.

Wazazi ndio watu wa kutupiwa lawama pale ambapo mtoto anakuwa ni kilaza shuleni,hakuna mwingine.

Binafsi nilipoigundua hii siri ya kwamba akili ya mtoto inakuwa kwa mujibu wa mazingora na malezi basi nikawa makini sana na kijana wangu.

Nikaanza kumshirikisha kwenye kazi ninazofanya nyumbani kama vile kung'oa majani na kuyaweka kwenye mifuko na kwenda kutupa.

Au kufua nguo naye huwa namuwekea beseni lake na nguo huku akifua na niasema kabisa "baba tufue nguo" ili misamiati hiyo iingie kichwani mwake na kutengeneza uwezo mpya katika ubongo.

Hata kama kazi inanzofanya hatofanya kama mimi ila lengo ni kumuongezea uwezo na kulanua ubongo wa mtoto ili ije kumsaidia huko mbeleni.

Watu wengi hawafahamu kwamba kila jambo analojifunza mtoto kwa kufanya ama kuongea basi jambo hilo linaenda kufungua milango fulani kwenye ubongo na hatimae sasa mlango unakuwa wazi na linapotokea jambo fulani ambolo linafanana kidogo ama sana na jambo lileee ambalo lilifungua mlango basi unakuta mtoto ni rahisi kuelewa kwa sababu mlango ulishafunguka.

Siku moj nilimkuta mwanangu amefungua bomba la maji anachezea yale maji yanayochuruzika hiku akipitisha mkono kana kwamba alitarajia yale maji yatakwamisha mkono wake kama ilivyo kamba,lakini haikuwa hivyo na aliendelea na mchezo huo,binafsi nilijua kwamba hapo kuna kitu anatafiti japokuwa mwenyewe hajui kama anatafiti na hawezi kusema kwamba baba ee hapa nafanya utafiti ila unconsciously anatafiti(curiosity)na utafiti huo unaenda kufungua milango mlango wa ufahamu katika ubongo wake.

Imagine leo mzazi anamkuta mtoto anachezea maji eti anampiga na kumkataza,ukatili ulioje huu.

Lakini pia kazi ndogondogo ambazo utamshirikisha mtoto naye azifanye alaafu akawa anazifanya hata kama sio kwa ukamilifu,hapo maana yake unamtengeneza mtoto awe na tabia ya kuelewa yaani kule kufanya kwake hizo kazi basi kazi hizo zinaenda kufungua milango ya kuwa muelewa kwenye akili yake.

Yaani maanayake ni kusema kwamba kama ameelewa task nyingi anazopewa nyumbani vipi atashindwa kuelewa task za shule ?

Hapo sasa tunamtengeneza mtoto awe na tabia ya kuelewa na mimi huu ndio msemo wangu kwa watoto kwamba KUELEWA NI TABIA,hivyo tabia hiyo inatakiwa ianzie nyumbani.

Na ili tabia hiyo ianze nyumbani basi lazima mzazi awe anamfundisha mwanawe mambo mbalimbali nyumbani na ashirikiane nae kufanya kazi za nyumbani.

Kama mama anamenya vitunguu swaumu basi mpe na mtoto naye amenye hata kama hatofanya kwa usahihi ila unamtengeneza akili iwe komavu kuhandle tasks anazopewa.

Kama inaosha vyombo mpe chombo naye ashikeshike hata kama ni vya kuvunjika mpe hata akivunja kimoja atajua kwamba kumbe vinavunjika,hiyo itakuza akili.

Haya yote yanachangia katikabkukuza uelewa wa mtoto na kumfanya awe na akili njema.

Wazazi wanaogopa kuwapa task watoto nyumbani kwa kudhani hawastahili lakini ndio wanawauwa vibaya sana na kuwafanya wawe na akili iliyojifunga ambayo haina experience na vitu vingi.

hAta kwenye kula mtoto wa miaka mi3 utakuta analishwa eti kisa yeye hawezi kula vizuri,muache ale hata akimwaga chakula chini mwache aenjoy utoto wake na muda sio mrefu ataweza kula vizuri.

Yapo mengi ya kuandika kwa kuwaelimisha wazazi,nikushukuru sana bwana Andrew Tate ate kwa mchango wako murua ambao nilikuwa nautafuta kwenye comment karibia zote.
 
Kuna thread niliandika a few years back inahusu why Africa haina maendeleo, nenda kaicheck. Nimeelezea baadhi ya haya mambo.
Mkuu fanya unitag kwenye huo uzi ili nami nikajifunze huko tafadhali..
 
Ongea nao, waulize maswali ujue nini changamoto zao.
 
Awali ya yote Muombe Allah ajaalie wanao wawe wenye kuitafuta na kuishika Elimu,wawe na kumbukumbu ya wanachofundishwa na kujibu vyema wanachofundishwa au kuelekezwa imma shuleni au nyumbani,kuna watt unaweza kujua bongo zao kupitia namna anavyo behave ukiwa nae nyumbani,atafanya kwa usahihi maagizo unayompa,atazingatia,kukumbuka na kutenda km ulivyomuelekeza,hapa utapata jibu kua mwanangu ana kichwa cha kushika ama laah!
Pili,zingatia lishe kwa watoto. Mboga mboga na matunda,protini,samaki na vyakula vya kuimarisha afya ya akili,mm sio mtu wa lishe,ukiwaona watu wa lishe utaelezwa zaidi.
Tatu,walimu wanaomfundisha mwanao wana mchango ktk kumfanya mwanao aipende shule? Walimu wa chekechea au shule za msingi ndio nguzo,hapa mtoto anaweza kufanywa aipende shule au kuichukia kutokana na approach mbaya za walimu,mfano watoto kuchapwa fimbo ovyo,adhabu kali,kufokewa na kadhia zingine.
Nne,km msingi wa maarifa ya mwanao (ufaulu wake) ni mbovu usitegemee kua atafanya vyema madarasa ya juu,mfano mwanao toka la kwanza hadi la nne/tano anakua nafas za mwisho usitegemee la sita/saba atafanya miujiza,tafuta mwalimu atakaeweza kudadisi mtoto alianzia wapi kuanguka amnyanyue,ni mada zipi katika level ipi/darasa lipi zinamshinda? Baada ya kushughulikia changamoto hizo+mazoezi ya kutosha na masahihisho,naimani mtoto atakaa sawa na atafaulu vyema.
Tano,wape watoto muda wa kucheza na ku-refresh,wajichanganye kidogo na watoto wenzao na kufanya ubunifu wa kitoto,tv,cartoon za kuelimisha sio mbaya ila vyema zaid kujichanganya na watt wenzao.
Sita,wajengee watoto msingi wa kumjua Mungu,wajue mafundisho kwa uchache juu ya imani yao,kwa umuhomu walau hata wajue sala na maombi,maombi yana nguvu kubwa haswa ukianza kujiombea mwenyewe kabla hujaombewa.
NA ALLAH NDIYE MJUZI ZAIDI.
 
Kuwa na akili nyingi kuna changiwa na brain cells , sasa kuna wengine inatokea wana brain cells nyingi hivyo wanakuwa na akili tayari hivyo taarifa kwenye ubongo zinakuwa zinapita kwa haraka na urahisi na brain cells zikiwa chache basi mtoto taarifa zinakuwa hazipiti kwa haraka na urahisi , ila pia mzazi anaweza changia mtoto kuwa na akili akiwa chini ya miaka mitano kwa kumpa vyakula vyenye virutubisho vitakavyochochea brain cells kuzaliwa kwa wingi au kumpa mtoto actvities nyingi za kufanya ile michezo kama ya kupanga vitu mtoto asiwe idle, kuchora au kumuexpose kwenye rangi rangi tofauti na vitu vingine. Sasa akizidi miaka mitano brain cells zinaachwa kuzalishwa alizokuwa nazo ndio hizo hizo sasa hapo unachoweza kufanya ili awe na akili nyingi ni kufanya vitu kwa kurudia rudia ambayo hii itastrech urefu wa brain cells alizonazo sasa kama ni darasani inabidi awe anasoma sana basi na brain cell zinakuwa stretched na inakuwa rahisi kukumbuka kutokana na nafasi kati ya brain cells kupungua , au kama ni michezo basi inabidi afanye mazoezi sana hapo napo uwezo/akili zitangezeka.
 
Fuata ushauri wa watafiti wa akili na maombi kwa mwenyezi Mungu, hakikisha watoto wako wanakula vyakula vinavyosaidia katika ukuaji wa akili tangu wakiwa wadogo, lakin pia mtu anaweza kuwa na akili akashindwa kuzitumia vizuri, akifika ngazi za juu kabisa kama vyuoni ndio akili inafunguka na anakupigia shule, labda awe na matatizo ya kiakili, mazingira pia yanachangia...
 
Na akili za watu zinatofautiana, mwingine atashika vya darasani (kukariri) na kila mtihani akifanya atafaulu vizuri sana, mwingine darasani anashika kidogo lakini ubongo wake upo vizuri kwenye kufkiria vitu vya ziada na kulielewa jambo kuliko hata mwalimu mwenyewe (wavumbuzi) na magenius, wengine hata bila kufundishwa ila akiona swali au kitu hajawahi ona akili yake inaprocess hicho kitu na kujitengenezea majibu yake makini.


Zingatia tu kupitia History za vipanga na jinsi walivyoishi, afu pia akili ya mtu huongozwa na mtu mwenyewe, akiamua hata ufanye nini haifungui, kwahiyo hapo angalia namna ya kuwafanya wanao wajue uthamani wao na faida ya elimu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…