Nifanyeje wanangu wawe na akili nyingi darasani

Nifanyeje wanangu wawe na akili nyingi darasani

Miongoni mwa mambo ya maana katika hii dunia mbaya ya siku za mwisho ni Elimu. Kila mzazi anatamani kama mimi ninavyotamani wanangu wawe vichwa darasani katika masomo yao, lakini wengi, kama mimi pia tunaishia kutamani tu hasa tunapoona watoto wa wengine wakifanya maajabu katika masomo yao.

Kwangu mimi wanangu hawaendi nitakavyo, mimi pamoja na wanangu kusoma shule za binafsi, English mid. Anayejua siri ya watoto kufanya vizuri anipe wandugu.

Nimejitahodi kuwakazania kusoma na kuwasaidia mimi mwenyewe. Tuition za kufa mtu, vitabu nanunua. Wakifeli na fimbo wanapata, wakifaulu zawadi wanapata. Lakini sioni kufanya vizuri kule mimi ninakotaka, inaniuma sana.

NIFANYEJE
Dunia ya sasa akili za darasani zinaweza zisiwasaidie kama unavyodhani. Huko dunia imehama, cha msingi zingatia interests na passion zao.
 
Miongoni mwa mambo ya maana katika hii dunia mbaya ya siku za mwisho ni Elimu. Kila mzazi anatamani kama mimi ninavyotamani wanangu wawe vichwa darasani katika masomo yao, lakini wengi, kama mimi pia tunaishia kutamani tu hasa tunapoona watoto wa wengine wakifanya maajabu katika masomo yao.

Kwangu mimi wanangu hawaendi nitakavyo, mimi pamoja na wanangu kusoma shule za binafsi, English mid. Anayejua siri ya watoto kufanya vizuri anipe wandugu.

Nimejitahodi kuwakazania kusoma na kuwasaidia mimi mwenyewe. Tuition za kufa mtu, vitabu nanunua. Wakifeli na fimbo wanapata, wakifaulu zawadi wanapata. Lakini sioni kufanya vizuri kule mimi ninakotaka, inaniuma sana.

NIFANYEJE
Vipi ukoo wenu una akili lakini?
 
Sisi tulifanya vizuri kwasababu ya lifestyle! Hatukua na mambo mengi ya kidigitali yanayotuzonga...
Kuna mtoto jirani hapa jana anamwambia mama ake ampe simu atumie calculator kufanya hesabu ya 12 ×15 yuko la6 english medium fulani inasifika Hapa Daslam! Na mama ake anachekelea tu! Sasa mtu hataki kusumbua ubongo atafauluje? Tatizo kubwa ni malezi sikuhizi ya kijinga jinga! Mwingine anasoma kayumba darasa la 5 amepewa homework ataje faida 5 za madini hajui na kafundishwa mama ake akaumiza kichwa mimi nikamjibia na wala hakuonyesha kukwazwa kwamba mwanangu aandike chochote akakose akichapwa fimbo ajitambue aaah! Karidhika tu.

Sasa sisi zamani Tv yenyewe nyumbani hamna wazazi wako ndo muda wa kukufundisha hawana ukipigwa shule wanakuja kukuongezea! Yani ule ugumu nao ulitukomaza kujitambua
Sasa mtu ashajua hata nikifeli mzee atanipeleka popote nikasome atanipambania asome sana ili iweje?
 
Ukitaka kuwa na watoto vipanga darasani hakikisha unaoa mke kipanga haswa.Yaani mkeo awe mwerevu Kweli Kweli.

Then hakikisha watoto wako hawali ugali kbsa coz Ni chakula kinachodumaza akili.
Wale nini ambacho hakidumazi akili??
 
Mama ni wa la saba tu, baba ana diploma ya IT, na anadigrii ya uongozi na maendeleo ya jamii, pia anacheti ya veta ya udereva. Huyo bado sio, hata kwao baba ndugu zake ni wasomi waziristan tu hata mzazi wa baba naye msomi mzuri tu.
wazazi vilaza mnataka watoto wawe genious sasa watakuwa wamerithi kwa nani? au mchepuko?
Cha muhimu hapo hakikisha wanaenda shule wanatimiziwa mahitaji yao yote ya muhimu na sio kuwalazimisha ujinga wako.

Mtu amesoma maendeleo ya jamii unasema ni msomi mzuri?
 
Cha msingi waangalie sehemu gani wako very bright alafu warlekeze uko wenzetu wazungu ndio wanavyofanya ndio unakuta wana professionalism kwenye kila nyanja
 
Kama utaweza mkuu wajengee ratiba ya kulala mapema then uwe unawaamsha saatisa usiku unakaa nao mnafanya ibada na wanasoma kuanzia dk 40-60 wakishindwa kutoboa kwa viwango ujue hapo hakuna Mwalimu atawaweza.
ujinga huu
 
Mitoto akili itoleee wapi,wakati kutwa kukariri miziki misingeli na amapiano hku wanakata mauno

Ova
 
Kwanza wanajitambua yaani wana uelewa mzuri ukitoa mambo ya shule?

Ikiwa jibu ni ndio waelekeze katika vipawa vyao zaidi .

Mfano ikiwa hawapati A Ila pia hawapiati D basi hao wako vizuri.

Mimi Kama Mwalimu natoa ushauri kuwa tumia mbinu za kuwajengea mentality ya ushindi kuanzia ndani yao. Hii waweza tumia subconscious mind.

Usitumie nguvu kubwa mfano viboko nk hizo mbinu hazisaidii chochote.

Mtoto mjenge taratibu kwa kumtia moyo na hata akipata marks ndogo wewe mtie moyo
Una kitu mkuu hembu fafanua...krk malezi kiaakili
 
Binafsi huwa siamini sana katika akili ya kurithi kwa wazazi, hii naipa asilimia kidogo sana. Nijuavyo, hakuna mtu anazaliwa mtupu..kila mtoto ana kitu, na hicho kitu ni muhimu wazazi/walimu kukibaini na kukiendeleza. Baada ya darsani(masomo) wajenge watoto utaratibu wa kufanya vitu vingine nje ya ratiba za shule/tuition; mfano kuchora, kufinyanga, kucheza mpira, kusimulia hadithi, nk. Watie moyo na kuwajengea imani kuwa wanaweza, na wanaweza kuwa kama fulani aliyefanikiwa...
Unajidanganya kuna watoto wengine vichwa maji hata ufundishe vp haelewi huyu anakuwa anakipaji sehemu nyingine mpeleke huko
 
Elimu sio kwa kila mtu.

Angalia historia ya familia yenu mjikite huko.
 
Miongoni mwa mambo ya maana katika hii dunia mbaya ya siku za mwisho ni Elimu. Kila mzazi anatamani kama mimi ninavyotamani wanangu wawe vichwa darasani katika masomo yao, lakini wengi, kama mimi pia tunaishia kutamani tu hasa tunapoona watoto wa wengine wakifanya maajabu katika masomo yao.

Kwangu mimi wanangu hawaendi nitakavyo, mimi pamoja na wanangu kusoma shule za binafsi, English mid. Anayejua siri ya watoto kufanya vizuri anipe wandugu.

Nimejitahodi kuwakazania kusoma na kuwasaidia mimi mwenyewe. Tuition za kufa mtu, vitabu nanunua. Wakifeli na fimbo wanapata, wakifaulu zawadi wanapata. Lakini sioni kufanya vizuri kule mimi ninakotaka, inaniuma sana.

NIFANYEJE
Walishe ndizi Kwa sana!
Rejea Wala ndizi sana!
Wachaga
Wanyakyusa
...
Ukikaa nao darasani huwawezi!
Sasa unawalisha samaki Wanao Kwa sana lazima wawe wambeya!
Rejea Wala samaki!; limtokalo mdomoni sio lililo Rohoni!
Samaki yupo baharini macho hafumbi😆😆😆😆😆
Na kama unawalisha nyama Kwa sana lazima wawe na hasira!; nyama Iko bucha instetemeka😆😆😆
Rejea Wanyambwa, Kurya.....akitoa kisu hakirudi Bure mpaka akupasud ngeu.
KAMA UTAONA HUU NI UBUYU POTEZEA....
 
Miongoni mwa mambo ya maana katika hii dunia mbaya ya siku za mwisho ni Elimu. Kila mzazi anatamani kama mimi ninavyotamani wanangu wawe vichwa darasani katika masomo yao, lakini wengi, kama mimi pia tunaishia kutamani tu hasa tunapoona watoto wa wengine wakifanya maajabu katika masomo yao.

Kwangu mimi wanangu hawaendi nitakavyo, mimi pamoja na wanangu kusoma shule za binafsi, English mid. Anayejua siri ya watoto kufanya vizuri anipe wandugu.

Nimejitahodi kuwakazania kusoma na kuwasaidia mimi mwenyewe. Tuition za kufa mtu, vitabu nanunua. Wakifeli na fimbo wanapata, wakifaulu zawadi wanapata. Lakini sioni kufanya vizuri kule mimi ninakotaka, inaniuma sana.

NIFANYEJE
Unataka waje kuwa wakina nani hao watoto wako.? Maisha yamebadilika sana ni zaidi ya kupata div one unapokuja kwenye mazingira halisi. Chunguza uwezo wa watoto wako upo kwenye nini, inawezekana wana vipaji labda vya michezo kama mpira wa miguu au wana ujuzi wa jambo fulani. "Ufaulu darasi siyo ufaulu maisha maishani".
 
Back
Top Bottom