Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Walishe vyura na konokono.Miongoni mwa mambo ya maana katika hii dunia mbaya ya siku za mwisho ni Elimu. Kila mzazi anatamani kama mimi ninavyotamani wanangu wawe vichwa darasani katika masomo yao, lakini wengi, kama mimi pia tunaishia kutamani tu hasa tunapoona watoto wa wengine wakifanya maajabu katika masomo yao.
Kwangu mimi wanangu hawaendi nitakavyo, mimi pamoja na wanangu kusoma shule za binafsi, English mid. Anayejua siri ya watoto kufanya vizuri anipe wandugu.
Nimejitahodi kuwakazania kusoma na kuwasaidia mimi mwenyewe. Tuition za kufa mtu, vitabu nanunua. Wakifeli na fimbo wanapata, wakifaulu zawadi wanapata. Lakini sioni kufanya vizuri kule mimi ninakotaka, inaniuma sana.
NIFANYEJE
Sagaa ni kitu ipiTengenezeaa Juicee wanywe mkuu
Tabia za wazazi na elimu ya Dunia, (life learning skills), huathiri akili ya mtotoAkili ina_tegemeana na mazingira wanayoishi.
Akili pia inarithiwa kutoka kwa wazazi.
mfano nna shda ya pesa, nawezaje kupata hela kwa kumeditate?Hii ndo dawa ya matatizo yote duniani Pesa , elimu na Afya
Hakuna ukweli mwingine zaidi ya huu..Fanya unaloona linafaa, wengine tukiwa watoto tulikua vilaza wa kutupwa ila kadri siku zinavyosonga ndo mtu anazidi kujitambua.
Kuna bwa.mdogo alikua kinara kuanzia darasa la 5-7, form 1 vipaji maalum na huko akawaongozea kiwilaya mitihani yote hadi anamaliza form 4.
Ila kabla ya hapo darasa la 1 hadi la 4 nafasi zake zilikua 20+, lakini kadri siku zinaenda kijana aliimprove sana, so wape muda.
Uongoo huo kufanya vizuri sio elimu ya wazazi ni uelewa wa mtu binafsi kuna wale wazito kuelewa na wepesi kuelewajua hilo so usiseme huo ujinga elimu mtu aliyonayo sio vigezo vya watoto kupata ufaulu darasani.Kinachofanya mtoto awe na uwezo mzuri darasani ni two factors:
1. Hereditary factor - biological factor
Kwenye hiyo factor baba ukiwa na elimu ya kuunga unga na mam elimu ya kuokoteza okoteza basi hata ikitokea baba ukabahatisha kupata fedha za kutosha na uwezo mkubwa wa kiuchumi usije tegemea mtoto wako atakuwa na akili darasani.
Na ndio maana mnapotaka kuoa mnashauriwa usichague mwanamke kwa kuangalia shepu lake mkadhani mwanamke akiwa na mshepu ndio akili, matako makubwa sio indicator ya kusema huyu mwanamke atanizalia watoto ambao watakuwa bright, au mwanamke mweupe ukadhani uzuri - weupe wake mwanamke ndio utafanya watoto wawe na akili. HILO SAHAU KABISA.
Wanaume wengi walio oa wanafeli kwenye hili.
2. Factor ya pili ni environment unayowalelea watoto wako. Ukiwalea watoto kwenye mazingira duni don't expect kuwa watakuwa na akili darasani. Lakini hii factor ni supplement tu kwenye factor namba moja hapo.
Kwa maana nyingine hata uishi masaki, osysterbay, mikocheni etc with very good life lakini una mwanamke akili kisoda au wewe mwenyewe akili yako ya kitapeli tapeli tu halafu ndio ukaangukiwa na bahati ya mtende kuwa na FEDHA, ndugu yangu hata ufanye vipi toto lako litaendelea kuwa la hovyo hivyo hivyo.
Imagine mke darasa la saba, baba diploma au degree ya kuunga unga halafu mtoto awe na akili darasani kweli kwa ku-compete na watoto wenye mama zao ambao ni Bachelor degree holders? Hiyo sahau mkuu, kwa maana ya never ever!
Ulishapotea kwenye kufanya choice ya mke wa kuoa.
NB: MIMI NDIO MAANA KWENYE TANGAZO LANGU LA KUTAFUTA MKE NIMEKUWA VERY CLEAR - mwanamke awe Bachelor degree holder or above it na wala sitaki mwanamke mwenye elimu ya kuunga unga eti mara nilisoma certificate mara diploma, no please 🥺
Kaka ulishayakanyaga, endelea kukomaaa tu na hali yako
Uongo huoMfumo wa maisha yako hapo nyumbani ndio mashine ya kunoa akili ya wanao.. wewe mwenyewe unaishi nao vipi.
1. Unakuta mzazi saa nne usiku upo na mwanao sebuleni mnaangali tamthilia, hapo ukipanga darasani sahau, ingawa wachache wanafanikiwa.
2. Mzee unakuta everyday unarudi upo nyingi kichwani haufuatilii maendeleo ya shule hapo ukipanga sahau.
3. Mzazi atakuzuga mara Moja Moja na wewe upo kibarazani unasoma kakitabu hakuna.
4. We Kila siku ukirudi nyumbani kumzukia tu mama Yao Kwa kauli chafu na muda mwingine unampa kisago mbele yao, hapo ukipanga sahau.
5. Mzazi kutwa kuwaza birthday ya mwanao kuliko kumnunulia vitabu na kutafuta mwalimu wa ziada.
6.
Mwanangu anajua Sana mahesabu yupo kayumba standard 4 akili nyingi sanaa amekua wa 5 Kati ya 278Miongoni mwa mambo ya maana katika hii dunia mbaya ya siku za mwisho ni Elimu. Kila mzazi anatamani kama mimi ninavyotamani wanangu wawe vichwa darasani katika masomo yao, lakini wengi, kama mimi pia tunaishia kutamani tu hasa tunapoona watoto wa wengine wakifanya maajabu katika masomo yao.
Kwangu mimi wanangu hawaendi nitakavyo, mimi pamoja na wanangu kusoma shule za binafsi, English mid. Anayejua siri ya watoto kufanya vizuri anipe wandugu.
Nimejitahodi kuwakazania kusoma na kuwasaidia mimi mwenyewe. Tuition za kufa mtu, vitabu nanunua. Wakifeli na fimbo wanapata, wakifaulu zawadi wanapata. Lakini sioni kufanya vizuri kule mimi ninakotaka, inaniuma sana.
NIFANYEJE