Nifanyeje wanangu wawe na akili nyingi darasani

Nifanyeje wanangu wawe na akili nyingi darasani

Sawa mama yao hajasoma sana, baba yao amesomasoma na kifanya vizuri shuleni.
Hahahaha hiyo amesoma soma imenipa picha, vipi elimu Yako Wazazi walipambana sana kwako hadi kukuletea ticha home? 🤣

Form IV ulitoka na Div III au IV?
 
Miongoni mwa mambo ya maana katika hii dunia mbaya ya siku za mwisho ni Elimu. Kila mzazi anatamani kama mimi ninavyotamani wanangu wawe vichwa darasani katika masomo yao, lakini wengi, kama mimi pia tunaishia kutamani tu hasa tunapoona watoto wa wengine wakifanya maajabu katika masomo yao.

Kwangu mimi wanangu hawaendi nitakavyo, mimi pamoja na wanangu kusoma shule za binafsi, English mid. Anayejua siri ya watoto kufanya vizuri anipe wandugu.

Nimejitahodi kuwakazania kusoma na kuwasaidia mimi mwenyewe. Tuition za kufa mtu, vitabu nanunua. Wakifeli na fimbo wanapata, wakifaulu zawadi wanapata. Lakini sioni kufanya vizuri kule mimi ninakotaka, inaniuma sana.

NIFANYEJE

Tangu ujauzito mama yao lishe ilikuwaje?
Je watoto walipozaliwa mfumo wa lishe ulikuwaje ?
Au ndio kunywa chai ya rangi na kitumbua ?

Je hali ya akili ya mama na baba ikoje?

Mazingira ya makuzi na ulezi yakoje ?

Nyendo za wazazi na mioyo yenu ikoje?
Maana wengine dhurumat wa haki za watu usizani utapona uzao wako.

Mfano Mchawi unaharibu maisha ya watu , unaua usitegemee vizazi vyako kupona 👌👌

Tujitafakali.
 
Uwezo wa kuelewa haufanani mkuu... Hata Harvard kuna rank ya Kwanza mpaka mwisho. Cha muhimu mtoto ajue kusoma, kuhesabu na kuandika. Mengine Mungu anajua, leo DJ Ally B amejenga maisha kuliko vipanga wengi tu 🤣🤣🤣
 
Daa! Sikujua kama ugali unadumaza akili. Labda kwa miaka ya kizazi hiki cha sasa. Miaka ya zamani kidogo, wengine ugali ndio ilikuwa chakula kikuu. Vyakula vingine kama ubwabwa ilikuwa ni kwa siku maalumu tu, kama sikukuu, lakini tulikuwa tunazigonga A za kutosha.
Ubwabwa na ugali vyote siyo vyakula, ni vitoweo tu.

Vyakula (Main sdishes) ni Kuku, mayai, nyama, samaki, mboga, maziwa.

Unatakiwa ule nyama kwa wali/ugali siyo Wali au ugali kwa nyama.

Upo hapo ulipo?
 
Ubwabwa na ugali vyote siyo vyakula, ni vitoweo tu.

Vyakula (Main sdishes) ni Kuku, mayai, nyama, samaki, mboga, maziwa.

Unatakiwa ule nyama kwa wali/ugali siyo Wali au ugali kwa nyama.

Upo hapo ulipo?
Hii ni kweli kabisa!
Ila wengi wetu tunafanya kinyume kutokana na wingi wa familia ukijumlisha kipato kidogo
 
Ukitaka kuwa na watoto vipanga darasani hakikisha unaoa mke kipanga haswa.Yaani mkeo awe mwerevu Kweli Kweli.

Then hakikisha watoto wako hawali ugali kbsa coz Ni chakula kinachodumaza akili.
Ugali wa sembe ndio una shida. Atumie mtama, ulezi, ngano, mahindi ambayo hayajakobolewa.
 
Ubwabwa na ugali vyote siyo vyakula, ni vitoweo tu.

Vyakula (Main sdishes) ni Kuku, mayai, nyama, samaki, mboga, maziwa.

Unatakiwa ule nyama kwa wali/ugali siyo Wali au ugali kwa nyama.

Upo hapo ulipo?
nakazia nakazia, ephen_ unakumbuka nilikuambiaje kuhusu ugali dagaa?

soma nifute nisije nikatukanwa bure maana siku hz nikikutag kuna watu roho zinataka kuwatoka
 
Miongoni mwa mambo ya maana katika hii dunia mbaya ya siku za mwisho ni Elimu. Kila mzazi anatamani kama mimi ninavyotamani wanangu wawe vichwa darasani katika masomo yao, lakini wengi, kama mimi pia tunaishia kutamani tu hasa tunapoona watoto wa wengine wakifanya maajabu katika masomo yao.

Kwangu mimi wanangu hawaendi nitakavyo, mimi pamoja na wanangu kusoma shule za binafsi, English mid. Anayejua siri ya watoto kufanya vizuri anipe wandugu.

Nimejitahodi kuwakazania kusoma na kuwasaidia mimi mwenyewe. Tuition za kufa mtu, vitabu nanunua. Wakifeli na fimbo wanapata, wakifaulu zawadi wanapata. Lakini sioni kufanya vizuri kule mimi ninakotaka, inaniuma sana.

NIFANYEJE
Walete Kawe Kwa Mwamposa
 
Hakuna mtoto asiye na kichwa.

Anzia nyumbani, home schooling, shule ni kumalizia tu.

Unatakiwa kama mzazi usimame kidete, kujuwa wanachosoma nini, njia rahisi ya kumsomesha mtoto ni wewe kuwa mwanafunzi wake.
Vyakula vipi vina husika

Ova
 
Mimi binti yangu ananiona toka akiwa kadogo kabisa nikijisomea vitabu ,kakua kwenye hiyo hali yakuiga na yeye kupenda kujisomea ,kwa sasa nipo nae mbali ila hata tukiongea kwa simu tu anaomba nimletee vitabu vizuri vya stories mbalimabali .

Hii ilimjengea uwezo wa kupenda kusoma na kudadisi mambo mbalimbali, wewe kama mzazi matendo yako yanamchango mkubwa sana kumjengea mwanao mazoea mazuri au mbaya ambayo yatamjenga au kumbomoa kwenye makuzi yake na hata maisha yake ya baadae .

Wadada wengi wenye watoto na wazazi wengi wanapenda kushinda wanachati mda wote huku wakitaka mtoto wao apende kujisomea !! Apo Lazima wafeli tu.
 
Back
Top Bottom