Nifatilie toka shambani kilimo cha mahindi, maharage na alizeti hatua kwa hatua

Hongera sana 💪🏾
 
Changamoto nilizokumbana nazo hadi sasa.
1.Wadudu( Viwavi vamizi). Dawa nilizotumia Duduba,Wilcrom,Master. Zote zimefanya vizuru. Gharama kichupa cha mils100 ni 5000 na 10,000/= kwa Master.
Nb. Dawa za kuthibiti hawa wadudu ni nyingi inategemea hapo ulipo zipi zilizopo.

2.Mchwa kutafuna mahindi. Hii ndo changamoto kubwa inayonitesa. Dawa za mchwa ni gharama sana. Lita moja ambayo inatosha kwenye ekari moja ni Tsh.70 000/=. Kichupa kidogo cha mils 100 ni elfu 22,000= Dawa inaitwa Gradinet,nilifanikiwa kumudu hiyo ya elfu22,000 ni nzuri sana japo haikutosha.

Changamoto zingine ni za kawaida. More updates to come hadi mavuno.

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 

Kila jema
 
Hongera sana, piga palizi
 
Msimu huu wa kilimo ntakua natoa maelezo ya kitaalamu na picha live toka shambani kwa vitendo kuanzia kuaandaa shamba, kuchagua mbegu, kupanda, kuzuia wadudu na magonjwa, mbolea, kupalilia hadi kuvuna endelea kunifatilia.
NAMBA YAKO MKUU
 
Msimu huu wa kilimo ntakua natoa maelezo ya kitaalamu na picha live toka shambani kwa vitendo kuanzia kuaandaa shamba, kuchagua mbegu, kupanda, kuzuia wadudu na magonjwa, mbolea, kupalilia hadi kuvuna endelea kunifatilia.
Shukrani mkuu kwa huu uzi.
Mimi pia nimelima mahindi, hekari moja na jumatano yalitimiza wiki 3 tangu nipande. Nimepanda mbegu inaitwa DK777, nipo Ifakara.

Sasa hiv nafanya palizi ya kwanza then niweke mbolea. Nina mbolea 2 ambazo ni CAN na NPK ya kopo ambayo inawekwa kwa kuspray. CAN ina Nitrogen 27% Na hiyo NPK ina nitrogen 24%. Unashauri niitumie ipi mkuu?
 
Tumia CAN
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…