Nimetumia muda mrefu nikiwaza ni maneno gani ya kukuambia ndugu
Dam55
Na hii yote ni sababu ya tone iliyopo ktk maandishi yako,umeandika kwa uchungu sana [emoji17]
Well,sina cha zaidi ya kukupa pole. Naweza kuyahisi maumivu yako kabisa.
Lakini hili lisiishie ktk maumivu pekee,naomba hili liwe fundisho kwako.
Huwa napenda msemo mmoja "
Wakati mwingine subira ni kupoteza fursa"
Nikiwa na maana ya kwamba sio kila jambo linahitaji subira.
Kwanini nimesema iwe fundisho basi? Usirudie makosa uliyoyafanya juu yangu kwingine,sema...fikisha ujumbe wako kwa muhusika bila kusubiri.
Hata hivyo,usisikitike. Kila jambo hutokea au hata lisipotokea basi kuna sababu zake na kwetu sisi tunaoamini ktk Mungu tunasema huenda Mungu kakuepusha na jambo ambalo wewe hulijui.
Who knows?Huenda in real life nisingekupendeza kama ulivyopendezwa nami kupitia mwandiko wangu.
Baada ya kuyasema yote hayo basi,nikutakie kila la kheri.
Na nakuombea Mungu akupe aliye mbora zaidi ya Nifah,usisikitike wala kuhuzunika...amini Mungu ana mipango iliyokuwa bora juu yako,kila la kheri,
Nifah.