Niffah; msema kweli mpenzi wa Mungu

Niffah; msema kweli mpenzi wa Mungu

Kwa kweli leo acha tu nitoe yangu ya moyoni.
Kila mtu hapa JF anasababu yake ilimfanya ajiunge humu.

Kwa kusema ukweli na Mungu wangu ni shahidi, mtu aliyenipelekea kujiunga humu ulikuwa ni wewe.!

Nilikuja JF kwasababu yako ila kilichonikuta kikaniuza sana, nimevumilia na nashukuru Mungu kuwa nimeweza kwa asilimia Kubwa.

Nilijua nikijiunga humu itakuwa rahisi kupata namna ya kuwa na we karibu lakini kumbe zilikuwa ndoto za mchana kweupee.
Kwasababu kaka mkubwa ndo kesha wahi Tayari kiasi gani niliumia baada ya kufahamu hilo nashindwa hata kueleza.

Nikaamua kuweke heshima kwako na kwa kaka Mkubwa The Bold.
Ila leo naomba tu niwe muwazi mbele ya wana JF wote kuwa Mimi nilikuwa mateka wako bila wewe kujua na kamwe sikuwahi kukwambia hata siku moja na hata PM yako sijawahi kugusa yote kwa sababu ya kuheshimu na sikutaka kuwa msumbufu.

Samahani sana kama nitakukwaza kwa hili lakini nimeamua tu niweke wazi hata hivyo sina lengo la kutaka kukuharibia kwa Bro.
Kwasababu sita kufuatilia hata kidogo.

Kaka mkubwa unisamehe tu mdogo wako kwa kumpenda huyu kipenzi chako lakini sikuwa na kosa kwasababu sikuja kama ni wako.
Kwasasa nimekubali matokeo kamwe sitatia mkono wangu.

Ahsante.
Mwanaume wa Dar ndo keshatongoza hapo... Hahahaa.... Anajiliiiza na samahani nyiingi.
 
uzembe wako huo sas ungemtokea mapema sas hv angekuwa wako acha uzembe kama umpenda mwingine him nenda pm fast hatutaki vijan wazemb kam ww
na ukome kutaman shemejizo

Sawa mkuu ila Mimi sikujua hilo mapema kiukweli sioni kosa langu
Ila pia nimeshasema sina tamaa yoyote.
 
Aisee!! Sijui nikupe pole au nisemeje... Nadhani labda ni sahihi zaidi nikikupa hongera kwa hatimaye kujitutumua na kutoa kilichopo moyoni... Ndio uanaume

Nifah ni mwanamke wa kipekee kwa hiyo sishangai kwanini aliuteka moyo wako bila hata ya yeye mwenyewe kujua! Ni mwanamke ambaye kama mwanaume unajivunia kuwa naye na hata ukiwa kwenye hadhara lazima 'uvimbe' coz yuko ubavuni kwako...

So, no hard feelings here ndugu yangu! Nimeelewa... Ila nikukumbushe tu kuwa last month nilikuwa kwa Kamanda Sirro pale nimetoka ku-renew kibali cha kumiliki silaha... Kwa hiyo watch it, not to that extent [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Asee nimekuelewa vizuri sana kaka mkubwa ila ilikuwa haina haja ya kwenda kwa sirro kwasababu nimeshakubali matokeo muda mrefu bila hata ya kutia neno so kuwa na amani tu.
Hizo risasi zihifadhi tu kwa akili ya kumlinda dhidi ya watekaji mana si unajua tena kaka, ikiwezekana Hata AK47 usikae nayo mbali kwasababu wanaweza wakaja na jeshi zima kama pale kwenye kituo cha ile TV/redio.

Ahsante kaka.
 
Nimetumia muda mrefu nikiwaza ni maneno gani ya kukuambia ndugu Dam55
Na hii yote ni sababu ya tone iliyopo ktk maandishi yako,umeandika kwa uchungu sana [emoji17]

Well,sina cha zaidi ya kukupa pole. Naweza kuyahisi maumivu yako kabisa.
Lakini hili lisiishie ktk maumivu pekee,naomba hili liwe fundisho kwako.
Huwa napenda msemo mmoja "Wakati mwingine subira ni kupoteza fursa"
Nikiwa na maana ya kwamba sio kila jambo linahitaji subira.

Kwanini nimesema iwe fundisho basi? Usirudie makosa uliyoyafanya juu yangu kwingine,sema...fikisha ujumbe wako kwa muhusika bila kusubiri.

Hata hivyo,usisikitike. Kila jambo hutokea au hata lisipotokea basi kuna sababu zake na kwetu sisi tunaoamini ktk Mungu tunasema huenda Mungu kakuepusha na jambo ambalo wewe hulijui.

Who knows?Huenda in real life nisingekupendeza kama ulivyopendezwa nami kupitia mwandiko wangu.

Baada ya kuyasema yote hayo basi,nikutakie kila la kheri.
Na nakuombea Mungu akupe aliye mbora zaidi ya Nifah,usisikitike wala kuhuzunika...amini Mungu ana mipango iliyokuwa bora juu yako,kila la kheri,

Nifah.
 
Huyu popoma Nifah yuko busy kufuatilia matokeo ya simba kama yanamuhusu vile, anaacha kufuatilia nyuzi kama hii inayo muhusu. Hebu kuja huku useme neno tu ili tusipoteze mwanajf huku.
Hahahaaaaaa yani kaka yangu tokea ujue mimi ni Yanga umenimind sana.
Matokeo ya Simba...bahati yenu,subiri kesho wanaume washuke dimbani [emoji123]
 
Kama wewe ni wa dar nafuu hukumtongoza,
 
Hahahaaaaaa yani kaka yangu tokea ujue mimi ni Yanga umenimind sana.
Matokeo ya Simba...bahati yenu,subiri kesho wanaume washuke dimbani [emoji123]

Nyie washabiki wa Yanga mnakera sana asee, yaani mnavyofuatilia mambo yasiyowahusu kama mmetumwa. Anyaways, najua kwa Mbeya city hamtoboi, na mbao anakuja kuwavunja vunja, watu tujichukulie ubingwa wetu. Toto najua ni wenu, hivo sina tatizo. Haya hebu malizana na kijana hapa,
 
Nimetumia muda mrefu nikiwaza ni maneno gani ya kukuambia ndugu Dam55
Na hii yote ni sababu ya tone iliyopo ktk maandishi yako,umeandika kwa uchungu sana [emoji17]

Well,sina cha zaidi ya kukupa pole. Naweza kuyahisi maumivu yako kabisa.
Lakini hili lisiishie ktk maumivu pekee,naomba hili liwe fundisho kwako.
Huwa napenda msemo mmoja "Wakati mwingine subira ni kupoteza fursa"
Nikiwa na maana ya kwamba sio kila jambo linahitaji subira.

Kwanini nimesema iwe fundisho basi? Usirudie makosa uliyoyafanya juu yangu kwingine,sema...fikisha ujumbe wako kwa muhusika bila kusubiri.

Hata hivyo,usisikitike. Kila jambo hutokea au hata lisipotokea basi kuna sababu zake na kwetu sisi tunaoamini ktk Mungu tunasema huenda Mungu kakuepusha na jambo ambalo wewe hulijui.

Who knows?Huenda in real life nisingekupendeza kama ulivyopendezwa nami kupitia mwandiko wangu.

Baada ya kuyasema yote hayo basi,nikutakie kila la kheri.
Na nakuombea Mungu akupe aliye mbora zaidi ya Nifah,usisikitike wala kuhuzunika...amini Mungu ana mipango iliyokuwa bora juu yako,kila la kheri,

Nifah.

Nashukuru sana Kwa angalau kutambua kiasi gani nimeumia kwa hilo.
Kuna kitu huwa nakiamini kuwa kutoa au kuweka wazi kinachokuumiza ni njia pekee ya kukupunguzia mateso hata kama ukikosa msaada.

Nashukuru pia kwa ushauri wako na hapo nakili kuwa makosa ni yangu.
Na kwasasa kwako sina tena namna ya kuyarekebisha kama ujuavyo muda haurudi nyuma kamwe.

Umesema kweli kuwa inawezekana Mungu hakupanga.
Kweli labda yupo mwingine maalumu kwaajili yangu kwa hilo sina budi kukubali.

Mwisho nikutakie kila kheri na we pia.

Naomba niishie hapa sina sababu ya kusema mengi zaidi kwasababu hayawezi badili chochote.

Ahsante sana Nifah.
 
Back
Top Bottom