Niffer atoa majibu baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kutaka akamatwe kwa uchangishaji wa fedha kwa ajali ya maafa Kariakoo

Niffer atoa majibu baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kutaka akamatwe kwa uchangishaji wa fedha kwa ajali ya maafa Kariakoo

Kitoto kijinga hiki,kinajipiga kifua sasa
Mwana umleavyo ndivyo akuavyo. Ameshazoea Kuona ................... Zao Sasa anawatunishia kifua😂😂😂🤣🤣🤣........
Nakumbuka mwamba Magufuli kule mwanza gerezani mfungwa alisema yule askari anawanyanyasa , yule askari kuulizwa anasema Magu labda amekuja ili yeye ainuliwe.... Wewe we we we kuliwaka moto.....
Sasa haka katoto nani wa kukawashia moto????
 
Eti kunitaja na nimejisikia faraja,unamjibu waziri mdandaoni kwa herufu kubwa,Unamfokea! Mh
 
Mfanyabiashara maarufu Jennifer Jovin, anayefahamika kama Niffer, ametoa majibu yake baada ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, kumtaja katika hotuba yake ya hadhara akitaka afuatiliwe na kueleza nani aliyempa mamlaka ya kuchangisha fedha kufuatia ajali ya kuporomoka kwa gorofa la Kariakoo.

Soma: Live Updates Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Watu 7 wengine waokolewa

Kupitia majibu yake yaliyojaa shukrani na kueleza nia njema, Niffer amesema:

"Kwanza kabisa, Alhamdulillah, namshukuru sana Allah kwa kunipa nafasi ya kuiona siku ya leo. Kwa kweli, ni jambo kubwa sana kwangu kuona Waziri Mkuu wa nchi yangu ametaja jina langu mbele ya hadhara ya watu mashuhuri. Hii ni ndoto kubwa iliyotimia kwa ulimwengu wa roho."

Niffer ameeleza kuwa nia yake kuu ilikuwa kusaidia wahanga wa ajali hiyo, akisisitiza kuwa hakujua sheria zinazohusiana na uchangishaji wa fedha kwa ajili ya mafaa kama hayo. Ameeleza:

"Nilikuwa tayari tangu mwanzo kutoa ushirikiano kwa Serikali na jamii kwa ujumla. Niliomba muongozo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa kabla ya kuanza zoezi hili. Ninaamini nia yangu haikuwa mbaya, na kupitia changamoto hii, nimeona umuhimu wa kuwa na taasisi inayotambulika rasmi, Niffer Foundation."

Waziri Mkuu Majaliwa, wakati akizungumza eneo la Kariakoo, alisisitiza kuwa hakuna mtu anayepaswa kuchangisha fedha bila kibali maalum kutoka serikalini na akatoa agizo kwamba Niffer atafutwe ili aeleze ni nani aliyempa mamlaka hiyo.

Soma, Pia: Jeshi la polisi tayari limempata Niffer kwa kuchangisha michango ya wahanga wa Kariakoo

Baada ya agizo hilo, taarifa zilitolewa kuwa Niffer ameshapatikana na yuko tayari kushirikiana na mamlaka husika.
Duh huyu ana utoto sana . Anajua nguvu ya Waziri Mkuu ? Amewezaje kuandika hivi baada ya Tamko la waziri mkuu ? Hii ni dharau kubwa sana !
Yuko kwenye denial haoni kama alichofanya ni koÅŸa na kinaweza kumtia hatiani!
 
"Kwanza kabisa, Alhamdulillah, namshukuru sana Allah kwa kunipa nafasi ya kuiona siku ya leo. Kwa kweli, ni jambo kubwa sana kwangu kuona Waziri Mkuu wa nchi yangu ametaja jina langu mbele ya hadhara ya watu mashuhuri. Hii ni ndoto kubwa iliyotimia kwa ulimwengu wa roho."
Imenikumbusha Fataki alisema maneno kama haya

Anyway watu hukosa imani na serikali kwakuwa walijifunza kwenye tukio la tetemeko la ardhi Bukoba
 
Ujanja mwingi huwa unaambatana na ujinga mwingi, maana hata hapo majibu yake yanasadifu, angeomba tuu radhi kwa mtazamo wangu.
Kungekuwa na sheria za wazi na zinazojulikana kuhusu fundraising.

Mfano, kuna nchi zinataka mtu anayechangisha awe na foundation na awe anaripoti mapato na matumizi wazi kwa taasisi ya kukusanya kodi na kwa wananchi.

Ni kweli kwamba kutojua sheria si excuse ya kuvunja sheria, lakini pia, sheria isiyojulikana ikivunjwa ni rahisi kwa wananchi kumuonea huruma aliyevunja sheria.

Zaidi, jamii yetu imekaa kuhukumiana zaidi ya kusaidiana. Mtu kama Niffer angeunganishwa tu katika efforts za serikali za kukusanya michango.
 
Kati ya Niffer tapeli na sisi tunaotaka alipe kodi ni nani mwenye roho mbaya?
Akili za kuambiwa changanya na zako.

Wabongo tunakasumba ya kumchukia mtu pasipo sababu yeyote ya msingi. Na hasa akiwa amepiga hatua flani hua tunatamani kumrudisha alikotoka

TRA kutwa Kila siku wanazunguka madukani wewe unavyohisi hawajawahi mfikia dukani kwake?

Ishu ilikua anavunja bei, baadhi ya washindani wake wakaona anaharibu soko ndo wakatoa na izo shtuma.
 
1. Kutokujua Sheria siyo utetezi mbele ya Sheria.

2. Huyo Jennifer (sijuwi Nifa) anadai kwamba kabla ya kuanza kuchangisha aliomba kwanza muongozo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa.

Je, alipata muongozo upi from the RC?
Je, RC alim-mislead Nifa?

-Kaveli-
 
Back
Top Bottom