Niffer: Nilianza na mtaji wa elfu 40, sasa hivi nashika hadi milioni 150

Niffer: Nilianza na mtaji wa elfu 40, sasa hivi nashika hadi milioni 150

Kwenye kila mafanikio kuna uchafu Fulani hufunikwa na kaniki nyeusi tii usionekane

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa waliosoma chile ndio wataelewa hii
IMG_20230703_225545.jpeg
 

Mlimbwende kunako kiwanda cha Utangazaji, Mjasiriamali na mwanamitandao maarufu Bongo, Niffer Jovin, maarufu kama "Niffer" amefunguka namna alivyohaha kujitafuta hadi kufikia mafanikio makubwa akiwa na umri mdogo.

Niffer ambaye ametimiza miaka 24 mwaka huu, amesema safari yake ya kuutwaa utajiri haikuwa rahisi kama watu wanavyodhani, amesema yeye ni miongoni mwa watu waliotokea katika familia za kimasikini ambazo asubuhi unalazimika kula maembe badala ya kunywa chai, mrembo huyo amesema amewahi kwenda shule bila viatu, amewahi kupigwa kisa tu kukosa sabuni ya kufulia sare zake za shule, lakini pia alikuwa akimuona mama yake namna alivyokuwa anawahangaikia ili wapate chochote kitu na wakati mwingine alikosa kabisa, amesema hiyo ndiyo ilimpa chachu ya kuyasaka mafanikio kwa udi na uvumba ili asipite walimopita familia yake.

Kama ulikuwa unadhani mtaji wa duka kubwa la Niffer "Niffer Outfitstore" lilianza na mtaji wa mamilioni kadhaa unajidanganya, mpambaji huyo amesema hakuanza na mtaji wa milioni, laki moja wala elfu 50, amesema alianza na elfu 40 pekee na haijamchukua muda mrefu tayari amekuwa tajiri kwa mtaji huo mdogo wa nyanya chungu na vitunguu.

Siri kubwa ya mafanikio ya Mwanaharakati huyo wa maisha amesema ni kuwa na nidhamu na pesa, kuwa na marafiki wa kukujenga, kumuomba Mungu huku ukifanya kazi, kwani yeye wakati anajitafuta alikuwa anafanya biashara hadi saa nane, saa tisa za usiku wa manane. Muhaya huyo wa Bukoba amesema watu wanamshangaa kwa kuwa na duka kubwa akiwa na miaka 24 kwasababu hawajui namna alivyopambana kwa bidii kuyasaka mafanikio.

Amemalizia kwa kuwashauri wasichana wenye umri mdogo na wanawake ambao umri umeenda na bado wanahaha kutafuta maisha kwamba wafanye kazi kwa bidii, waache kubwabwaja mitandaoni kufatilia maisha ya watu na badala yake wautumie huo muda wauze hata pilipiii mbuzi watafika alipofika yeye.
Hapo kati
 
Inawezekana kwa wanomfuatilia huyu dogo ni mpambanaji sana anauza online zaidi na kila muda yupo anapost bidhaa tofautitofauti hana bidhaa za aina fulani kila kitu anauza..
Biashara ya hivi wamefanya sana hadi akina Elizabeth Michael akina Kajala na akina Mobeto na kina Masogange pia.

Mimi sipingi kwa hilo.
 
Back
Top Bottom