Nifungue project/biashara gani kwa mtaji wa milion 12

ahsante sana mkuu kwa ufafanuzi huu...Mungu akubariki naomba nikutafute ili unipe uzoefu zaidi kwenye hii biashara najua changamoto hazikosekani...ila walau kupitia wewe na uzoefu uliona utanisaidia namna ya kukabiliana nazo...
 
Habari.
Kwanza kabisa hongera kwa kupata mtaji.
Biashara ziko nyingi unazoweza fanya ila kwanza kabisa lazima ujue kuwa hiyo profit margin unayotaka haiko 'realistic' yaani ni ngumu sana kwa mtaji wa milioni 12 upate milioni 24 kwa mwaka. Biashara nyingi zenye faida kubwa sana huwa na risk kubwa hivyo unaweza kupoteza pesa nyingi au hata yote kabisa.

Ushauri wangu ni huu
(1) Biashara yoyote unaweza kuifanya ila hakikisha unafanya utafiti wa kutosha ikiwemo na utafiti wa masoko. Hakikisha unaijua hiyo biashara vizuri sana baada ya hiyo tafiti.
(2) Ukitaka kupunguza risk unaweza kuwekeza kiasi kidogo kwanza kwenye hiyo biashara husika, kwa mfano milioni 2. Baada ya hapo utajifunza vitu vingi kwenye hiyo biashara ambavyo hukuviona kwenye utafiti uliofanya mwanzoni. Pia unaweza kujua haswa wateja wako au biashara yako inataka nini. Baada ya hapo unaweza kuongeza investment kidogo kidogo na baadae ukatafuta hata na mikopo kwenye bank.
(3) Hakikisha unafungua account maalumu kwa ajili ya hiyo biashara na mihamala mingi uifanye kupitia hiyo account kwa mfano usiweke akiba nyumbani au kwenye simu badala yake weka kwa account yako ya benki. Hii itakusaidia huko mbeleni uweze kukopesheka kiurahisi.

Angalizo: Usikurupuke kuanzisha biashara hakikisha kwanza unajua fika nini unachotakiwa kufanya. Pia angalia mara mbili mbili hizi biashara za faida kubwa sana maana 'associated risks' ni nyingi sana

Nawasilisha
 
Dah hii kwa kusoma hapa utaona ni rahisi sana
 
Kwa biashara ya spare ndio maana nimemwambia weka home. Aanze mwezi anafungua frame kkoo.. kwa nguo aende tu hakuna shida.
Na spare za gari gani zinatembea sana au ilimradi iwe spare
 
Hivi hakuna watu wanaouza vifaranga waliotoka kwenye changamoto za mwanzo?
Na je hakuna vifo,vibaka,wanyama shambulizi?
 

Hahahha
 
Faida unayoitaka waweza ipata hila itatek time sio haraka haraka ivyo kama unavyowish otherwise utaangukia pua na hiyo mil12 ipotee kama upepo.
 
Nipe taarifa za ziada kwenye kukopesha na pia ktk ununuzi wahisa ktk kampuni gani au taasisi ipi ambayo ninaweza pata angalau sh. 2 mil. kwa mwezi
Investment ya 12 millioni haiwezi kukupa faida ya 2M per month. Hakuna.

Nunua mazao harafu uyauze msimu mwingine. All in all, usiingie kwenye business yoyoye kichwakichwa na kutegemea instant faida. Fanya utafiti kabla ya kuweka “mayai yote kwenye kapu moja”
 
Mazao gani mkuu, nipe na location na uzoefu kidogo kama umewahi kufanya. Kwa sasa kamtaji kameongezeka kidogo, Nina 14 milioni Cash
 
Kwa maoni niliyoyasoma hapa ni wazi kwamba fursa zipo nyingi sana,na pia watu wanajua mengi hivyo ukitaja kufanikiwa unahitaji watu walio na uelewa wa kile unataka kufanya.
Hamna lolote ni porojo za mtandaoni tu, wengo wanaonhea kwa hisia hawana takwimi zozote
 
Mimi nina bakery iko mbezi beach ninahitaji partner...kama uko intrested nicheck 0714882311...whatsapp only
Unahitaji partner lakini kutoa tu namba una masharti kama mganga kwani ukitoa mawasiliano complete utapungukiwa nini kama upo serious
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…