Nifungue project/biashara gani kwa mtaji wa milion 12

Nifungue project/biashara gani kwa mtaji wa milion 12

Yaah mkuu, hiyo ni bei ya kuuzia mashineni ambapo wanunuzi ndio hufika hapo, hasa kwa mpunga kutoka Bonde la kamsamba upo vizuri sana, na watu wengi kwa ukanda ule wanaenda kukobolea Tunduma

Mchele huu ndio kilo yake huwa inafika minimum kwa kilo ni Tsh. 1800/=

Ila kuna wenye uwezo wa kuleta mchele hadi Dar es Salaam hadi Zanzibar hawa ndio wanapata faida kubwa sana

Pia unaweza kufungua store yako kwa ajili ya kuuza mchele wako kidogo kidogo, pia kunakuwa na maharage (mchele hauozi wala maharage haya haribiki kirahisi)

Kwahyo unakuwa una kusanya mpunga wako kwa ajili ya kukoboa na kuuza kwenye store yako mwenyewe ya nafaka

Wali maharage ukishajua ni namna gani hiki ni chakula pendwa basi utajua ni namna gani pesa inapatikana hapo.
ahsante sana mkuu kwa ufafanuzi huu...Mungu akubariki naomba nikutafute ili unipe uzoefu zaidi kwenye hii biashara najua changamoto hazikosekani...ila walau kupitia wewe na uzoefu uliona utanisaidia namna ya kukabiliana nazo...
 
Salaam Alleykhum,

Wadau kwa kutumia uzoefu wenu, nishaurini nifungue project/biashara gani kwa mtaji wa million 12 nilionao ili kila mwisho wa mwezi at least nipate Net profit ya milioni mbili.

Nipo tayari kufanya biashara ktk mkoa wowote Tanzania au hata kama ni importation business kama mtaji unatosha nipo tayari.

Nipeni ushauri ili nami nitoboe.
Habari.
Kwanza kabisa hongera kwa kupata mtaji.
Biashara ziko nyingi unazoweza fanya ila kwanza kabisa lazima ujue kuwa hiyo profit margin unayotaka haiko 'realistic' yaani ni ngumu sana kwa mtaji wa milioni 12 upate milioni 24 kwa mwaka. Biashara nyingi zenye faida kubwa sana huwa na risk kubwa hivyo unaweza kupoteza pesa nyingi au hata yote kabisa.

Ushauri wangu ni huu
(1) Biashara yoyote unaweza kuifanya ila hakikisha unafanya utafiti wa kutosha ikiwemo na utafiti wa masoko. Hakikisha unaijua hiyo biashara vizuri sana baada ya hiyo tafiti.
(2) Ukitaka kupunguza risk unaweza kuwekeza kiasi kidogo kwanza kwenye hiyo biashara husika, kwa mfano milioni 2. Baada ya hapo utajifunza vitu vingi kwenye hiyo biashara ambavyo hukuviona kwenye utafiti uliofanya mwanzoni. Pia unaweza kujua haswa wateja wako au biashara yako inataka nini. Baada ya hapo unaweza kuongeza investment kidogo kidogo na baadae ukatafuta hata na mikopo kwenye bank.
(3) Hakikisha unafungua account maalumu kwa ajili ya hiyo biashara na mihamala mingi uifanye kupitia hiyo account kwa mfano usiweke akiba nyumbani au kwenye simu badala yake weka kwa account yako ya benki. Hii itakusaidia huko mbeleni uweze kukopesheka kiurahisi.

Angalizo: Usikurupuke kuanzisha biashara hakikisha kwanza unajua fika nini unachotakiwa kufanya. Pia angalia mara mbili mbili hizi biashara za faida kubwa sana maana 'associated risks' ni nyingi sana

Nawasilisha
 
Kutokana na mtoa mada anahitaji pesa au faida ya haraka basi ushauri wangu hautamfaa san ila kama anahitaji kam kuweka akiba ya faida kubwa hata miaka 5 mbele unaweza kumfaa.

Wazo n kwamba aje Kilombero anaweza kukodi shamba kwa bei ya 500k kwa kila heka na akapat heka 6 na kulihudumia na kulima kwa kila heka ni bajeti ya 1.5M

Na kilimo atakachokifanya ni cha miwa ambapo kila mvuno wa heka moja kam amehudumia vzur anaweza kupata mpk 3M kwa heka moja

Na bei io ya kukodi shamba n kwa makato 5 ndio unarudisha shamba yan kuvuniwa muwa mara 5 kwa hyo io n akiba nzuri tu ya miaka 5 mpk 10 ya kula matunda ya investment uliyofanya maan muwa ukivunwa unaota tena ww n kuweka mbolea kwa wakati na kupalilia tu

Sasa hapo piga faida yake 3M × 6 heka × mivuno 5 hapo utatoa hela ya kuhudumia shamba kdg iliyobaki n faida na ni zaid ya investment for future.
Dah hii kwa kusoma hapa utaona ni rahisi sana
 
Kaka km una kwako au kwenu eneo kubwa tuu, anza kufuga kuku wa layers kuku wale wa mayai, niamini utapiga zaidi ya hiyo milion 2 kwa mwezi ila yakupasa tu uvumilie ndan ya miez mitano hutovuna kitu ila baada ya hapo adi miaka 3 ijayo ww unavuna mamilioni.

1. Toa 2,500,000 nunua vifaranga 1000
2.Toa mil 2 uje ufungiwe cage ya kuingiza kuku 1000
3.Gharama za chanjo za siku 28 kwa vifaranga.
4.Vyakula vya kuku kuanzia starter Mash na kuendelea. Mfuko wa kilo 50 @49000 ila hapa wakishafikisha wiki tatu unaweza kuwachanganyia pumba+layers premix+layers mash
5. Vyombo vya chakula na maji.
6. Chumba maalum cha joto kwa vifaranga kwa miez 2

Yani inshort utatumia milion 7 tu mpaka kuku wanafika miezi 5 kuanza kutaga, na wakianza kutaga it means una uhakika wa kukusanya mayai 1000 kila siku iendayo kwa Mungu na hapo kuna kuku wengine wakishiba vizur wanaweza kukuangushia mayai 2 kwa siku.

Sasa chukua unakusanya mayai 1000 tu kwa siku, haya mayai 1000 ni sawa na trey 33 na mayai 10.

Trey kwa sasa ni sh 8000
Kwahiyo kwa siku 33x8000=264,000

Kwa mwezi sasa 264,000x30=7,920,000.

NB: Kwahiyo ukiwatunza vizur vifaranga kwenye chanjo, chakula braza wewe ni milionea unapiga zako Milion 7,920,000/= kwa mwezi kama faida haina tax hyo wala VAT. Na ukumbuke kuwa hawa kuku watakuwa wana uwezo wa kukutagia ndani ya miaka 3 wakichoka unawatoa unawauza nako unapiga hela kuku 1 sokoni 8000. 8000x1000= 8000,000/= baada ya miaka 3 utavuna Mil 8 km pesa yakuwauza nyama hapo umekosa nn kaka!!.


Yan ungejua mm nina shida ya milion 2 tu nitanue nitoke hapa kwny kuku 55 ambapo kwa mwez wanaingiza 440K tu.
Hivi hakuna watu wanaouza vifaranga waliotoka kwenye changamoto za mwanzo?
Na je hakuna vifo,vibaka,wanyama shambulizi?
 
Hapo kituo ambacho ni kizuri zaidi na nakuambia hivi kwasababu nimefika katika hizo field hizo katika harakati hizo za kununua hiyo mizigo ya Maboss mbalimbali.

Kuna kituo cha kamsamba/kilyamatundu,na Usangu coz hata kyela wananunua huko na wanapeleka kwao na kuwaongopea wanunuzi kwamba ni mpunga kutoka kyela kumbe ni wa kutoka kamsamba/kilyamatundu but Usangu is too much cost to handle

Kuna wengine Watasema ni hesabu za kwenye karatasi ila hizo ni hesabu ambazo nimekuwa nazo field na nina uzoefu nazo

Hahahha
 
Faida unayoitaka waweza ipata hila itatek time sio haraka haraka ivyo kama unavyowish otherwise utaangukia pua na hiyo mil12 ipotee kama upepo.
 
Nipe taarifa za ziada kwenye kukopesha na pia ktk ununuzi wahisa ktk kampuni gani au taasisi ipi ambayo ninaweza pata angalau sh. 2 mil. kwa mwezi
Investment ya 12 millioni haiwezi kukupa faida ya 2M per month. Hakuna.

Nunua mazao harafu uyauze msimu mwingine. All in all, usiingie kwenye business yoyoye kichwakichwa na kutegemea instant faida. Fanya utafiti kabla ya kuweka “mayai yote kwenye kapu moja”
 
Investment ya 12 millioni haiwezi kukupa faida ya 2M per month. Hakuna.

Nunua mazao harafu uyauze msimu mwingine. All in all, usiingie kwenye business yoyoye kichwakichwa na kutegemea instant faida. Fanya utafiti kabla ya kuweka “mayai yote kwenye kapu moja”
Mazao gani mkuu, nipe na location na uzoefu kidogo kama umewahi kufanya. Kwa sasa kamtaji kameongezeka kidogo, Nina 14 milioni Cash
 
Kwa maoni niliyoyasoma hapa ni wazi kwamba fursa zipo nyingi sana,na pia watu wanajua mengi hivyo ukitaja kufanikiwa unahitaji watu walio na uelewa wa kile unataka kufanya.
Hamna lolote ni porojo za mtandaoni tu, wengo wanaonhea kwa hisia hawana takwimi zozote
 
Mimi nina bakery iko mbezi beach ninahitaji partner...kama uko intrested nicheck 0714882311...whatsapp only
Unahitaji partner lakini kutoa tu namba una masharti kama mganga kwani ukitoa mawasiliano complete utapungukiwa nini kama upo serious
 
Back
Top Bottom