Nifungue project/biashara gani kwa mtaji wa milion 12

Kama kweli hii pesa unayo ukipewa mchongo wa kuingiza 10M ndani ya wiki mbili ama mwezi, utakubali kutoa 40% ya Faida utakayopata?
Mkuu, ninataka tuwasiliane zaidi kwa ajili ya hizo fursa ulizonazo.
 
Mkuu nimetamani sana kujua zaidi kuhusu hii biashara na niko na maswali yafuatayo.
1.Hayo mawe unanunua kwa bei gani kutoka kwenye hilo duara?
2.Je hao wamiliki wa duara mikataba yao ikoje je huwa wanahitaji walipwe kodi kila mwezi au ukinunua tu mawe kutoka kwao inatosha?
3.Hiyo kuozesha mawe ndio inakuwaje na lengo ni nini?
4.Processes zote zikishakamilika ni wapi soko la kuuzia hayo mawe au wateja wanayafuata hapo hapo kwenye duara?
 
Na huu ndio mtego uliopo kwenye biashara ya mpunga ni kuuziwa pumba/chuya so ukiwa mgeni kwenye hii biashara lazima wakupige.
Watu wasiojua wanarahisisha tu kwenye hesabu za makaratasi.
Wazoefu wa kwenye hii biashara wakiushika tu mpunga kiganjani kama ndani hauna kitu wanajua ila wewe kama ni mgeni utaibiwa.
 
Je soko ni uhakika??
 
Mkuu mm ni mfugaji wa hao layers..!hakuna mahesabu kama hayo..!hiyo pesa akinunua cage na vifaranga akajenga banda imeisha
 
hyo hela kwenye nafaka inaingiza ml 4 kwa mwez, mfano dengu mwez wa nane, kuna choroko
 
Biashara ndogo ndogo ziko nyingi sana mkuu kwa mfano restaurant,banda la kuuza chips,balo nguo za mtumba,duka la chakula rejareja nk kutegemea na hobby yako
Yaani "restaurant" ni biashara ndogo au ni jina tu ullikuwa una maanisha biashara ya "baba/mama ntilie"!? Banda la kuuza chips sawa, hata hivyo, location yake ni muhimu sana; nguo za mitumba na duka la chakula la rejareja - KWA KWELI SIJUI, Hapa tunazungumzia pia mtaji na miundo mbinu yake ikiwa ni pamoja na sehemu ya kuuzia na kufanyia hizo biashara. Na hapa ni lazima tuelewane biashara ndogo, mtaji wake ni UPI?
 
Nauza mchele kwa bei ya jumla mkuu(Ifakara -Dar),kila wiki nasafiri mara mbili na kila safari napata faida 250K,kwa huo mtaji wa 5M,piga hesabu 250,000 X 8 = 2,000,000.
Kaka uko wapi na je nawez Nika ku pm , naitaj data zaid nataman hii biashara
 
Hii sio biashara Bali ni upumbavu, yaan uweke 12m utemgemee 1m kwa mwaka alafu faida uje upewe baad ya 20yrs huo si umri wa mtu mzee maisha yenyew mafup hatun guarantee ata ya kuish miak miak 10.
 
Dah nimejikuta nacheka asee.

Mkuu alichoeleza huyo jamaa ni process nzima ya kuitafuta dhahabu.

Sio rahisi kama inavyosomeka kwenye maandishi yake hasa ukiwa hujui chochote kuhusu dhahabu. Ni biashara ambayo kuchoma mtaji wa 500million ndani ya week ni kawaida tu.
 
Hiyo pesa nenda nayo pale dodoma nunua mashine za kukamua alizeti, jenga kiwanda kidogo... Unanunua mbegu zaalizeti toka kwa wakulima pia unakamua mafuta unayapack kwenye galon na kuuza mikoa mbalimbali... Pia unaweza kukamua mbegu za watu binafsi wanaokuja wakiwa na mbegu zao.
 
Mashine ya Alizeti milioni 12??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…