Kaka km una kwako au kwenu eneo kubwa tuu, anza kufuga kuku wa layers kuku wale wa mayai, niamini utapiga zaidi ya hiyo milion 2 kwa mwezi ila yakupasa tu uvumilie ndan ya miez mitano hutovuna kitu ila baada ya hapo adi miaka 3 ijayo ww unavuna mamilioni.
1. Toa 2,500,000 nunua vifaranga 1000
2.Toa mil 2 uje ufungiwe cage ya kuingiza kuku 1000
3.Gharama za chanjo za siku 28 kwa vifaranga.
4.Vyakula vya kuku kuanzia starter Mash na kuendelea. Mfuko wa kilo 50 @49000 ila hapa wakishafikisha wiki tatu unaweza kuwachanganyia pumba+layers premix+layers mash
5. Vyombo vya chakula na maji.
6. Chumba maalum cha joto kwa vifaranga kwa miez 2
Yani inshort utatumia milion 7 tu mpaka kuku wanafika miezi 5 kuanza kutaga, na wakianza kutaga it means una uhakika wa kukusanya mayai 1000 kila siku iendayo kwa Mungu na hapo kuna kuku wengine wakishiba vizur wanaweza kukuangushia mayai 2 kwa siku.
Sasa chukua unakusanya mayai 1000 tu kwa siku, haya mayai 1000 ni sawa na trey 33 na mayai 10.
Trey kwa sasa ni sh 8000
Kwahiyo kwa siku 33x8000=264,000
Kwa mwezi sasa 264,000x30=7,920,000.
NB: Kwahiyo ukiwatunza vizur vifaranga kwenye chanjo, chakula braza wewe ni milionea unapiga zako Milion 7,920,000/= kwa mwezi kama faida haina tax hyo wala VAT. Na ukumbuke kuwa hawa kuku watakuwa wana uwezo wa kukutagia ndani ya miaka 3 wakichoka unawatoa unawauza nako unapiga hela kuku 1 sokoni 8000. 8000x1000= 8000,000/= baada ya miaka 3 utavuna Mil 8 km pesa yakuwauza nyama hapo umekosa nn kaka!!.
Yan ungejua mm nina shida ya milion 2 tu nitanue nitoke hapa kwny kuku 55 ambapo kwa mwez wanaingiza 440K tu.