Nifungue project/biashara gani kwa mtaji wa milion 12

Nina kazi nzuri tu, hiyo ni akiba yangu ipo tu but nataka kuifanyia kazi kwa malengo
Biashara isiyoumiza kichwa ni mazao wakati wa mavuno.. kama umeajiriwa kipindi cha mavuno ongea na boss chukua likizo zama shambani kanunue mazao ya chakula, sogeza mjini weka dawa na kuhifadhi store... yatakulipa, biashara nyingi za kumuachia mtu unaweza kuja kulia tu, labda awe mkeo/mumeo na awe na uchungu sana na hiyo pesa.

Usimpe pesa mtoto wako wala baba yako, labda mama mzazi.

Over
 
Biashara isiyo umiza kichwa ni mazao wakati wa mavuno..kama umeajiliwa kipindi cha mavuno ongea na boss chukua likizo zama shambani kanunue mazao ya chakula,sogeza mjini weka dawa na kuhifandhi store...yatakulipa,biashara nyingi za kumuachia mtu unaweza kuja kulia tu,labda awe mkeo/mumeo na awe na uchungu sana na hiyo pesa.

Usimpe pesa mtoto wako wala baba yako, labda mama mzazi.

Over
Bonge LA ushauri, shukrani sana mkuu
 
Njoo kilombero,, Morogoro ufanye utafiti mdogo alafu uangalie biashara gani inakufaa maana uko kuna fursa nyingi Sana,,

But najua adi unapat m12 ushapanga la kufanya all in all njoo kilombero kuna fursa

Nambie baadhi ya fursa zilizopo huko Kilombero
 
Biashara mpya kwa mtaji huo mkubwa is too much risk kama hautasimamia mwenyewe mkuu

Ila kuna option ya kununua mazao ya chakula hasa Mpunga gunia zako za kutosha na kuziweka store na inapofika kipindi cha Masika unafanya kuzikoboa gunia zako na kupata mchele wako swafi tayari kwa kuingiza sokoni kwani kipindi hicho uhitaji wa mchele unakuwa mkubwa sana hapa Dar es Salaam na Zanzibar

Minimum profit calculation

Katika centre nyingi ninazo zifahamu kwa muda huu gunia moja la Mpunga lina range kwenye TSH. 50,000/=
Hivyo basi kwa Pesa uliyonayo yaani TSH. 12,000,000, utaweza kupata gunia zenye debe sita sita 240 za mpunga na kuzihifadhi.

Kipindi ambacho Masika imechanganya hasa mwezi wa kwanza au wa pili, wewe ndo unafanya kukoboa mpunga wako ili upate mchele na gunia 1 la mpunga la debe sita linatoa debe tatu za mchele na debe moja la chenga za mchele

Hivyo basi katika zile gunia 240 unazidisha mara 3 na utapata debe 720 za mchele clear na debe 240 za chenga za mchele

Ukija sokoni debe moja la mchele lina range kwenye 35,000/= kwahyo unazidisha mara debe zako 720 za mchele na utapata kiasi cha TSH. 25,200,000/=, pia debe moja la chenga za mchele ina range kwenye TSH 10,000/= ukizidisha na debe 240 utapata kiasi cha 2,400,000/=

Total itakuwa ni Tsh. 27,600,000/= na ukitoa mtaji wako wa 12,000,000/= utapata net profit ya TSH. 15,600,000/= katika kipindi cha miezi mitano cha kuhifadhi mpunga wako

Ila ukija kutoa gharama za kuhifadhi mpunga na kukoboa haizidi TSH. 5,000,000/=,hivyo bado net profit itabaki kama 10,000,000/= katika miezi mitano yako ya uvumilivu.

Centre zenye mpunga mzuri ni kama zifuatazo Kyela, Kamsamba na kilyatundu, Usangu, Kahama ila kwa Morogoro sizifahamu vizuri

Naomba kuwasilisha na ninakaribisha maswali
 
You are a such best mathematician bro, japo wadau wanasema hesabu za kwenye makaratasi huwa zinatofautiana ukienda kwenye field but for really, your calculations are very impressive.
Kati ya hivyo vituo vya kununulia mzigo, kipi like bomba zaidi (kinachotengeneza profit zaidi)
 
Hapo kituo ambacho ni kizuri zaidi na nakuambia hivi kwasababu nimefika katika hizo field hizo katika harakati hizo za kununua hiyo mizigo ya Maboss mbalimbali.

Kuna kituo cha kamsamba/kilyamatundu,na Usangu coz hata kyela wananunua huko na wanapeleka kwao na kuwaongopea wanunuzi kwamba ni mpunga kutoka kyela kumbe ni wa kutoka kamsamba/kilyamatundu but Usangu is too much cost to handle

Kuna wengine Watasema ni hesabu za kwenye karatasi ila hizo ni hesabu ambazo nimekuwa nazo field na nina uzoefu nazo
 
Back
Top Bottom