Tupe na gharama za usafirishaji toka shamba mpk Dar pamoja na ushuru na mengineyo ili tupge hesabu ya net profit
Zifuatazo ni gharama za usafirishaji pamoja na ushuru kutoka Mbeya usangu hadi Dar es Salaam
Tone 1 ya gunia za mpunga gharama yake ni Tsh. 50,000/= katika usafiri wa malori makubwa.
Hivyo basi katika gunia 240 za mpunga nilizozungumzia hapo juu ni tone 34 za mpunga, hivyo jumla ya gharama za usafiri kwa tone zote ni Tsh. 1,700,000/=
Ushuru kwa kila gunia ni Tsh. 2000,hivyo kwa gunia zote 240 jumla ya ushuru ni Tsh. 480,000/=
Jumla ya gharama za ushuru na usafirishaji itakuwa ni Tsh. 2,180,000/=
Pia gharama za kuhifadhi mpunga kama ikatokea ukapata mashine ya kukobolea, yule mwenye mashine yuko tayari afanye kuhifadhi mzigo wako bure kwa sharti la kukoboa mzigo wako Ukisha kuwa tayari na mipango yako.
Pia na wanunuzi wengi wa mchele huwa wanapatikana palepale kwenye zile mashine za kukobolea kwa mfano hapa Dar kuna watu kutoka commoro, Kenya, Uganda na Zanzibar wanakuja kwaajili ya kuja kununua mchele
Pia unaweza kufanya maamuzi ya kuweka mchele wako katika store yako na kuuza taratibu kwa kilo kwani utaweza kupata faida maradufu zaidi
Na ndio maana katika ile faida ya TSH. 15,000,000/=,tulifanya approximation ya TSH. 5,000,000/= tunaitoa kwasababu ya gharama ya usafiri, ushuru na gharama za kukoboa na kufanya grading ya mchele wako
Ila lazima profit itabaki zaidi ya TSH. 10,000,000/= kama net profit yako
Watu wanakula na kuupenda sana wali katika nchi hii na nchi za jirani uhitaji ni mkubwa sana, ukiweza kuliona hili basi utaona na kunusa pesa faida ya Pesa ndefu hasa ukiwa na Mtaji
Try this, and thanks me later