Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Sawa.Rudi nyuma kidogo.
Kupitia hizo kanuni ndizo tunazozitumia kumuelezea Mungu
Kama ambavyo unazozitumia kumpinga Mungu.
Kanuni gani? Umezitaja wapi tuzichambue?
Mimi nimekupa kanuni za kimantiki.
Kwamba, kimantiki, Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kuumba ulimwengu ambao unaruhusu mabaya kuwepo kuna contradiction.
Contradiction hiyo inaonesha Mungu huyo hayupo.
Naweza kuonesha hilo kimantiki kama ninavyoweza kukuonesha kwamba wewe mwanamme mwenyewe miaka 30 leo huna mama mzazi ambaye ana miezi 6 leo, kwa sababu wewe kuwa na mama mzazi huyo inaleta contradiction kwenye timeline.
Sasa mimi nakwambia hivyo (Mungu huyo hayupo, binti wa miezi 6 ambaye ni mama yako hayupo) wewe unaniuliza chanzo cha binadamu ni nini (unaniuliza kama huyo binti si mama yako, mama yako nani?).
Mimi sijawahi kusema najua chanzo cha binadamu ni nini. Nimesema huyo Mungu hayupo.
Mimi sijawahi kusema namjua mama yako mzazi ni nani. Nimekwambia tu kuwa huyo binti wa miezi 6 hawezi kuwa mama yako mzazi wewe mwanamme mwenye miaka 30.