Nigeria: Aliyemtukana Mungu ameachiwa huru baada ya kutumikia kifungo cha miaka minne gerezani

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Mwanaume asiyeamini kuwa Mungu yupo kutoka nchini Nigeria, Mubarak Bala (40) ameachiwa huru baada ya kutumikia kifungo cha miaka minne gerezani kwa tuhuma za kumtukana Mungu kupitia Facebook mwaka 2020.

Mubarak alikamatwa Aprili 28, 2020, kwa tuhuma za kukufuru dini na uchochezi kutokana na machapisho yake kwenye mitandao ya kijamii.

Aprili 2022, alihukumiwa kifungo cha miaka 24 gerezani baada ya kukiri makosa 18, ikiwa ni pamoja na kukufuru na uchochezi.

Hata hivyo jana Januari 7, 2025, aliachiwa huru baada ya kutumikia kifungo cha miaka minne gerezani. Baada ya kuachiliwa amesema usalama wake bado uko hatarini kutokana na vitisho.

"Wasiwasi kuhusu usalama wangu upo kila wakati," aliambia BBC katika mahojiano yake.

Mwanaume huyo kwa sasa anaishi katika nyumba ya hifadhi, huku mawakili wake wakidai maisha yake yako hatarini ikiwa atarejea kuishi katika jamii.

Snapinsta.app_472631418_635924108763499_3608894704854264704_n_1080.jpg
 
Kilichomsibu huyo mwanaume ni DINI na wala sio eti alimtukana Mungu.
Mungu hajawahi kuhitaji watu wa kumtetea au kumsemea. Mbona hatujamsikia Mungu akilalamika katukanwa? Watu wanajipa Uwakili kwa Mungu i.e. Mungu ni mteja wao.
 
Teh! Watu walisikia mungu akitukanwa na wakatoa hukumu ila aliyetukanwa hakusikia na wala hana habari na kinachoendelea wala hakutuma mtu kumsemea! Inafikirisha!
 
Mwanaume asiyeamini kuwa Mungu yupo kutoka nchini Nigeria, Mubarak Bala (40) ameachiwa huru baada ya kutumikia kifungo cha miaka minne gerezani kwa tuhuma za kumtukana Mungu kupitia Facebook mwaka 2020.

Mubarak alikamatwa Aprili 28, 2020, kwa tuhuma za kukufuru dini na uchochezi kutokana na machapisho yake kwenye mitandao ya kijamii.

Aprili 2022, alihukumiwa kifungo cha miaka 24 gerezani baada ya kukiri makosa 18, ikiwa ni pamoja na kukufuru na uchochezi.

Hata hivyo jana Januari 7, 2025, aliachiwa huru baada ya kutumikia kifungo cha miaka minne gerezani. Baada ya kuachiliwa amesema usalama wake bado uko hatarini kutokana na vitisho.

"Wasiwasi kuhusu usalama wangu upo kila wakati," aliambia BBC katika mahojiano yake.

Mwanaume huyo kwa sasa anaishi katika nyumba ya hifadhi, huku mawakili wake wakidai maisha yake yako hatarini ikiwa atarejea kuishi katika jamii.

View attachment 3195842
Walimfunga Kwa Ajili ya nini?
 
Inategemea huyo Mungu alipomtukana alimtukana akiwa ktk content zilizotokana na dini gani,kama alitumia content za ile dini ya wenyewe kumtukana ajue na atambue yeye ni maiti inayotembea muda wowote kichwa wanabeba

Ila kama ni wale wengine wa shavu hili geuza na hili hata akienda kumtukana tena leo hakuna wa kumgusa.
 
Back
Top Bottom