Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Furaha imetanda katika Kaya moja nchini Nigeria ambapo mwanamke mwenye umri wa miaka 40 amejifungua watoto 6 ikiwa watatu wa kiume na watatu wa kike baada ya kupita miaka zaidi ya 20 tangu alipopata mtoto wake wa kwanza.
Kuzaliwa kwa watoto hao kulitangazwa katika video iliyosambazwa TikToka na mtoto wa kwanza wa mwanamke huyo akionyesha furaha yake kubwa ya kuongezeka kwa familia yao.
"Nimekuwa mtoto wa pekee mama yangu alinizaa wakati wa ujana wake na akaolewa miaka 8 iliyopita, na tangu wakati huo amekuwa akitafuta kwa kila njia lakini mwishowe Mungu alionyesha, ametupa 6, wavulana 3 na wasichana 3. Kile ambacho Mungu hawezi kufanya hakipo" — Ameandika mtoto wa kwanza wa Mama huyo
Soma: Nigeria: Mwanamke ajifungua watoto 9 baada ya miaka 25 ya ndoa bila mtoto
Soma: Nigeria: Mwanamke ajifungua watoto 9 baada ya miaka 25 ya ndoa bila mtoto