Odhiambo cairo
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 15,989
- 22,078
Duhh. RIP Sis Osinachi .Mwanamuziki wa Nyimbo za Injili kutoka Nigeria aitwaye Sis Osinachi Nwachukwu maarufu kwa wimbo wake “Ekwueme” amefariki dunia.
Osinachi alishirikishwa na Prospa Ochimana katika wimbo huo, amefikwa na mauti jioni ya Aprili 8, 2022, hii baada ya kupambana na ugonjwa usiojulikana kwa takriban miezi miwili huku vyanzo vingine vikidai ni kansa ya koo.
Baadhi yake nyimbo ni pamoja na “Nara Ekele” akiwa na Mchungaji Paul Enenche (Dunamis,Abuja), “Ekwueme” akiwa na Prospa Ochimana na nyinginezo.
Wimbo wa Ekwueme umejipatia umaarufu sana kutokana maudhui yake huku ukitasambaa na kuimbwa na jamii kubwa duniani.
Source: Dailypost
Siri ya kifo inakatisha tamaa