Yesu ni Mungu Kamili na ni Mwanadamu Kamili!
Yesu Aliongea kuhusu Kutumwa Alipokuwa katika Hali yake ya Ubinadamu Kamili!
[emoji116][emoji116]
Yohana 1
1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.
3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.
14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.
Ratiba ya Huduma ya Yesu duniani Ilikuwa hivi kabla ya Ufufuko!
[emoji116][emoji2535][emoji116][emoji2535]
Isaya 49
6 naam, asema hivi, Ni neno dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu ili kuziinua kabila za Yakobo, na kuwarejeza watu wa Israeli waliohifadhiwa; zaidi ya hayo nitakutoa uwe nuru ya mataifa, upate kuwa wokovu wangu hata miisho ya dunia.
Baada ya Ufufuko!
[emoji116][emoji2535][emoji116][emoji2535]
Mathayo 28
16 Na wale wanafunzi kumi na mmoja wakaenda Galilaya mpaka mlima ule aliowaagiza Yesu.
17 Nao walipomwona, walimsujudia; lakini baadhi yao waliona shaka.
18 Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.
19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
View attachment 2234652