Niishi vipi na uyu baba wa watoto wangu

Niishi vipi na uyu baba wa watoto wangu

Ipo ivi mm ni mama ninamiaka 29 sasa ..naombeni busara zenu kuishi vipi na uyu mwanaume ..tumezaa watoto wawil apa kati tuliachana lakini nyumbani awakuelewa na hawataki kusikia ilibdi niludi kulea watoto shida ni . tunaishi mimi na baba watoto na wifi yangu pamoja na watoto wawil wadog ambao awajafika miaka 5 pamoja na mtoto wake niliemkuta wakidato cha kwanza..ivyo familia ya watu sita lakin mwanaume anakuachia sh elf 5 tu siku nzima na hapo Amna kitu chochtote ndani na watoto ni wadogo ambao inabdi asubui upike chochte wapate kula uku tukisubir mchana na Sio mwanaume anauwezo hapana uwezo upo wakawaida na ela kidogo anapata shida ni ulevi namarafiki akipata ela atawaita marafiki zake watakaa watakunywa uku nyumbani inafika mda mtt mdogo anamiak 4 anatakiwa kuanza nasary lakini baba kumlipia mtoto elf 15 aende shule awez anasema ana hela akija akakuta nyumbn nmepika ugal na mlenda yeye ali anaenda kula vibandani tu ..kinachoniuma roho ni uyu motto miaka 4 anaingiza mitano ata kuanza shule yupo tu nyumbani jamani wanajamii naombeni uniambie niishi vip walau niweze kubana matumizi walau nipate mtaji tu niwe naingiza ata elf 1000 niweze kumpelek mtoto shule nimnunuliege na vitu vyake nisiwe mtu wa kugombana nae kila siku maana ata ukiongea sana yeye akujib n yule mtu anaekaa kimya tu utaona vitendo nawaza kuondok lakin apana bdo sijajipanga na watoto hawa na nyumbani awataki swala la kuondoka ata kidogo ..ivyo tu nahitaji ushaur niishi nae vip ili walau iyo anayotoa iwe inabaki nijiwekee akiba ata 500 kwa siku nipate mtaji najua kupika vitafuno mbalimbal ..unakuta unajibana lakin inashindikan unaishia kupata na madeni madukani nmechoka san nahitaji tu faraja walau roho yangu utulie moyo mzito sana wanajami nifanye walau nilipe Ada ya mtoto aende shule mimi nipambane mwenyew ...nb sim niliyonayo sio yakuuzika labda kama skrepa..Kwaiyo naombeni tu faraja yenu niishi vip walau nibane matumizi .. Ile kupata changu binafsi ata kidogo lakn kinikidhi maitaji yangu na watoto wangu ..moyo unaniuma sana nahitaji faraja yenu tu labda moyo utatulia na mtanipa njia nzuri yakuweka akiba sitatoka kama nilivyo kupitia izi huu ..samahani kama nmekosea
Nenda hata kwa majiran uombe kazi ya kufua nguo nk hutakosa chochote
 
Usibane matumizi bali tafuta njia za kuongeza kipato, pia huo muda unaotumia kumkimbia mumeo na watoto ungetumia kumuombea maana sio kawaida...
Kama hamjapanga anza kulima mboga mboga kisha uza hata matembere, kama umepangisha jifunze kupika mandazi uza ingia youtube kupitia hii simu uliyo post nayo huu uzi..
Kwa maelezo zaidi bonyeza moja
sikuzote kocha achezi, watu kwa kushauri tu hamjambo
 
Haya mengine huwa yanatokea sababu mlikuwa na mapozi sana kipindi cha usichana mkikataa kila mwanaume anayekuja na siajabu mume wako ulishapishana nae ukiwa na miaka 21 huko nyuma.
Ila changamoto inakuja sababu wanadamu hatujui kazi ya MUNGU inafanyikaje tunahisi Maisha ni mchezo mchezo.

Tukirudi kwenye mada, nadhani unatakiwa kukaa na mumeo chini mjadili hizi changamoto za kifamilia. Kukaa kimya,kumnunia,kuondoka na kuanza pekee yako sidhani kama vitakuwa ni suluhu katika hatua hizi za awali za changamoto.

Kama ninyi wanawake mnavyopitia magumu ya kisaikolojia na kufanya makosa muda mwingine na wanaume hupitia magumu na namna ya kucope ni kuwajiweka mbali na familia.

Mwanamke mwerevu akishaona dalili za hizi tabia kitu cha kwanza ni kuzungumza na mwenzake kwa upendo bila kukata tamaa na huku ukiiambia akili yako kuwa jibu lipo na kama halipo litapatikana tu bila shida kwa kumshirikisha MUNGU na jitihada za pamoja.

Kaa chini tambua gharama halisi za mahitaji ya familia,kaa na wanawake wenzako uongee nao kuhusu fursa mbali mbali ambazo wataweza kukushirikisha na usije ukathubutu kuwahadithia matatizo ya ndoa yako maana wataanza kutumia hiyo kama ndio chanzo cha matatizo. Ongea na wenzako wakupe dili za kike ndogo ndogo, kisha mfuate mwenzako umwambie changamoto ulizoziona na ugumu unaopata kama mke na yeye amekaa kimya.

Sio kila mwanaume unayekutana nae anakuwa amepevuka kiakili kwasababu ana kazi na kipato, wengine bado wapo katika uvulana hawajioni kama baba wa familia na wanastruggle na hiyo shida. Ukianza kumlalamikia au kumsema yeye kutowajibika anakuona changamoto kwake na ataanza kukukwepa kama mfuko wa mbolea ya samadi. Atakuona ni shida na hatotaka mazoea na wewe na ukaribu utakufa.

So kaa nae chini na kuzungumza nae akwambie shida ipo wapi. Wanaume wameumbiwa kubembelezwa sio kupelekeshwa.
 
WANAUME WA HIVI WAJINGA WAPO,ULICHOANDIKA HAPA HUYO MWANAUME MJINGA HAWEZI KUFANYA.
 
Ipo ivi mm ni mama ninamiaka 29 sasa ..naombeni busara zenu kuishi vipi na uyu mwanaume ..tumezaa watoto wawil apa kati tuliachana lakini nyumbani awakuelewa na hawataki kusikia ilibdi niludi kulea watoto shida ni . tunaishi mimi na baba watoto na wifi yangu pamoja na watoto wawil wadog ambao awajafika miaka 5 pamoja na mtoto wake niliemkuta wakidato cha kwanza..ivyo familia ya watu sita lakin mwanaume anakuachia sh elf 5 tu siku nzima na hapo Amna kitu chochtote ndani na watoto ni wadogo ambao inabdi asubui upike chochte wapate kula uku tukisubir mchana na Sio mwanaume anauwezo hapana uwezo upo wakawaida na ela kidogo anapata shida ni ulevi namarafiki akipata ela atawaita marafiki zake watakaa watakunywa uku nyumbani inafika mda mtt mdogo anamiak 4 anatakiwa kuanza nasary lakini baba kumlipia mtoto elf 15 aende shule awez anasema ana hela akija akakuta nyumbn nmepika ugal na mlenda yeye ali anaenda kula vibandani tu ..kinachoniuma roho ni uyu motto miaka 4 anaingiza mitano ata kuanza shule yupo tu nyumbani jamani wanajamii naombeni uniambie niishi vip walau niweze kubana matumizi walau nipate mtaji tu niwe naingiza ata elf 1000 niweze kumpelek mtoto shule nimnunuliege na vitu vyake nisiwe mtu wa kugombana nae kila siku maana ata ukiongea sana yeye akujib n yule mtu anaekaa kimya tu utaona vitendo nawaza kuondok lakin apana bdo sijajipanga na watoto hawa na nyumbani awataki swala la kuondoka ata kidogo ..ivyo tu nahitaji ushaur niishi nae vip ili walau iyo anayotoa iwe inabaki nijiwekee akiba ata 500 kwa siku nipate mtaji najua kupika vitafuno mbalimbal ..unakuta unajibana lakin inashindikan unaishia kupata na madeni madukani nmechoka san nahitaji tu faraja walau roho yangu utulie moyo mzito sana wanajami nifanye walau nilipe Ada ya mtoto aende shule mimi nipambane mwenyew ...nb sim niliyonayo sio yakuuzika labda kama skrepa..Kwaiyo naombeni tu faraja yenu niishi vip walau nibane matumizi .. Ile kupata changu binafsi ata kidogo lakn kinikidhi maitaji yangu na watoto wangu ..moyo unaniuma sana nahitaji faraja yenu tu labda moyo utatulia na mtanipa njia nzuri yakuweka akiba sitatoka kama nilivyo kupitia izi huu ..samahani kama nmekosea
Pole Sana dada ,nitumie namba yako ,ili unipe gharama za huyo mtoto kuanza shule nitakutumia .
Pole Sana
 
Back
Top Bottom