Niishi vipi na uyu baba wa watoto wangu

Nenda hata kwa majiran uombe kazi ya kufua nguo nk hutakosa chochote
 
sikuzote kocha achezi, watu kwa kushauri tu hamjambo
 
Pole sana kwa yote Mungu akusaidie katika changamoto unayopitia.
 
Haya mengine huwa yanatokea sababu mlikuwa na mapozi sana kipindi cha usichana mkikataa kila mwanaume anayekuja na siajabu mume wako ulishapishana nae ukiwa na miaka 21 huko nyuma.
Ila changamoto inakuja sababu wanadamu hatujui kazi ya MUNGU inafanyikaje tunahisi Maisha ni mchezo mchezo.

Tukirudi kwenye mada, nadhani unatakiwa kukaa na mumeo chini mjadili hizi changamoto za kifamilia. Kukaa kimya,kumnunia,kuondoka na kuanza pekee yako sidhani kama vitakuwa ni suluhu katika hatua hizi za awali za changamoto.

Kama ninyi wanawake mnavyopitia magumu ya kisaikolojia na kufanya makosa muda mwingine na wanaume hupitia magumu na namna ya kucope ni kuwajiweka mbali na familia.

Mwanamke mwerevu akishaona dalili za hizi tabia kitu cha kwanza ni kuzungumza na mwenzake kwa upendo bila kukata tamaa na huku ukiiambia akili yako kuwa jibu lipo na kama halipo litapatikana tu bila shida kwa kumshirikisha MUNGU na jitihada za pamoja.

Kaa chini tambua gharama halisi za mahitaji ya familia,kaa na wanawake wenzako uongee nao kuhusu fursa mbali mbali ambazo wataweza kukushirikisha na usije ukathubutu kuwahadithia matatizo ya ndoa yako maana wataanza kutumia hiyo kama ndio chanzo cha matatizo. Ongea na wenzako wakupe dili za kike ndogo ndogo, kisha mfuate mwenzako umwambie changamoto ulizoziona na ugumu unaopata kama mke na yeye amekaa kimya.

Sio kila mwanaume unayekutana nae anakuwa amepevuka kiakili kwasababu ana kazi na kipato, wengine bado wapo katika uvulana hawajioni kama baba wa familia na wanastruggle na hiyo shida. Ukianza kumlalamikia au kumsema yeye kutowajibika anakuona changamoto kwake na ataanza kukukwepa kama mfuko wa mbolea ya samadi. Atakuona ni shida na hatotaka mazoea na wewe na ukaribu utakufa.

So kaa nae chini na kuzungumza nae akwambie shida ipo wapi. Wanaume wameumbiwa kubembelezwa sio kupelekeshwa.
 
WANAUME WA HIVI WAJINGA WAPO,ULICHOANDIKA HAPA HUYO MWANAUME MJINGA HAWEZI KUFANYA.
 
Pole Sana dada ,nitumie namba yako ,ili unipe gharama za huyo mtoto kuanza shule nitakutumia .
Pole Sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…