Nikasikia Bonge la Msonyo nyuma yangu

πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„ Kwann?
Naogopa usikute nikapiga wakati tiba ya sheikh bado haitaki mizagamuano afu ikaniletea mimi shida maana bado anaratiba za kwenda kwa huyo sheikh.
 
Hizi stori zitasababisha tuanze kupiga kimya tukisemeshwa hata na wale wanaoulizaga maeneo/ njia
 
Kumwambia mtu kwamba aje huku ashinde zawadi kama ni mteja wa muda mrefu bila kumwambia kwamba kuna hela inatakiwa kuipata hiyo zawadi ni aina fulani ya utapeli.

Yani hata kama si kumtapeli mtu moja kwa moja, unaanza kumvuta mtu kwa kutumia false advertisement.

Yani kama mtu ana shughuli zake anawahi, halafu anajikuta kapoteza dakika kumi akifikiri anashinda zawadi ya T-Shirt bure kwa kuwa mteja wa siku nyingi tu, akajikuta kabadilishiwa kibao anunue simu, ambayo hata haihitaji, huo ni utapeli.

Wangemwambia tangu mwanzo mpango wote.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ aaah kumbe you type from πŸ‡ΊπŸ‡Έ πŸ‡ΊπŸ‡Έ mzee nilisahau bora ubaki huko huko basi nikwambie huku Tz kampuni au kazi nyingi za Sales kwenye makampuni ni za kijanjajanja kama hivyo na training ndio munafundishwa hivyo Tz kazi za Sales ndio imekuwa Kimbolton la haraka strategies zake ndio kama hivyo.
 
1. Wanatumia udhaifu (take advantage) kwamba wanaume wengi huwa ni "dhaifu" mbele ya mwanamke.
2. Wana-take advantage kwamba wabongo wengi hupenda vitu vizuri lakini kwa bei ndogo. Tunapenda vya mteremko a.k.a Kwa sadala.
3. Wanajua kwamba ss Wabongo hatunaga bajeti au Mipango ambayo ni "Very Tight and Rigid" -tuko very flexible na tamaa kwa wingi hususan tunapokuwa na fedha japo ni kidogo.
4. Wabongo wengi wanakuwa na aina fulani ya Ulimbukeni na hutaka/hupenda makuu au kuonekana -show off. Unatamanishwa simu ya laki moja lakini unaambiwa leta hata buku 5 tu malipo mengine baadaye 😡 😡 😡. Ukijichanganya Unapigwa.
 
Any ways unaweza kuwa sahihi siwezi kukupinga moja Kwa Moja,nilikutana nao baada ya ile sheli ya posta mpya ukitokea crdb bank

Ila lolote lawezekana chief
Basi sio hao kuna wwngine wanakaa pale round about ya sanamu la staring kwenye miti na gari sina hakika kama matapeli au sio ila ni wanauza simu mimi naamini ni their out door selling strategies tu so siwezi amini matapeli coz wajanitapeli.
 
Mkuu,

Najua. Mwaka 2012 nilikuja likizo Tanzania.

Siku ya pili tu nikataka kupata simu ya Bongo kurahisisha mawasiliano. Nikaenda pale Mlimani City kupata simu.

Basi yale matangazo yalivyoandikwa ndiyo kama hivyo, uongouongo kibao.

Na kila nikiwabana wale watu wa sales na customer service waelezee rates zao, ambazo zilikuwa zimekaa kitapelitapeli, ikawa kama wao ndio wananishangaa mimi kwa style ya "Wewe vipi, mbona una maswali mengi? Kwani hujui kawaida yetu?.

Nikasema "hii nchi ngumu hii, nishakuwa mgeni tena".
 
Nishawakuta hapo posta Benjamin Mkapa, nikamwambia nimetoka nyumbani na mambo mengine hiyo habari kununua simu Sina ratiba hiyo ,ving'ang'anizi nikawambia kesho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…