Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kweli Chief, hilo ni somo zuri umetukumbusha, tahadhari muhimu sanaSiku nyingine kitendo cha kusogea kwenye gari tu, utajikuta ushatekwa.
Hahah una mbio lakini?kuna watu humu wangepigwa hapo. au niwataje?
Naogopa usikute nikapiga wakati tiba ya sheikh bado haitaki mizagamuano afu ikaniletea mimi shida maana bado anaratiba za kwenda kwa huyo sheikh.😄😄😄 Kwann?
Hizi stori zitasababisha tuanze kupiga kimya tukisemeshwa hata na wale wanaoulizaga maeneo/ njiaKuna dem alitapeliwa mwisho wa mwaka jana ,alitoka bank akakutana na jamaa nje ya bank..jamaa kamsalimia afu dem akaitikia ndio ikawa nitolee hiyo, yaani dem akajikuta anamfuata jamaa hadi kwenye gari. Wakaingia dem wakamkalisha siti ya nyuma katikati,pembeni kuna watu wawili. Wakaenda hadi karibu bagamoyo wakamshusha. Dem akabaki kazubaa zaidi ya lisaa, hadi konda wa daladala alipomuuliza vp unaenda ndio akashtuka na kuanza kupiga wayowe. Watu wakajaa dem akazimia..peleka hospital akazinduka kesho yake..simu hana,pochi hana.... bahati nzuri kuna namba ya dadaake anayokichwani ndo kupigiwa wakaja mchukua. Dem aliumwa balaa akawa kama anamapepo...hadi kumletea shehe ndo hali ikaanza badilika kupata nafuu. Miez mitatu ndo dem kaanza kurudi kawaida ila bado anapata ganzi miguuni hadi sasa.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] ila mmetufundisha ninyiHawa wanawake sio kwa hii speed waliyonayo kuelekea ukengeufu.[emoji23]
Inaogopesha aisee, kwa style hiyo watatutesa wengiHizi stori zitasababisha tuanze kupiga kimya tukisemeshwa hata na wale wanaoulizaga maeneo/ njia
Nitaje tukuna watu humu wangepigwa hapo. au niwataje?
Huwa wanakunusisha(Vutisha bila ww kujua) scopolamine (Burundanga). 😱Huwa hakuna kitu kama kuzubaishwa. Ni maneno matamu tu ya kupumbaza.
ni binti tu hata 30 hajafika
Kumwambia mtu kwamba aje huku ashinde zawadi kama ni mteja wa muda mrefu bila kumwambia kwamba kuna hela inatakiwa kuipata hiyo zawadi ni aina fulani ya utapeli.Sidhani kama hao wadada ni matapeli, tunakimbilia sana kuita watu matapeli bila kuhakikisha hao ni wauza simu tu hio ni strategies wanazotumia kwenye sells zao ni vyema ungesikiliza mpaka mwisho ndio uhitimishe.
Bilashaka hao wadada wanakaaga pale sanamu la askari na gari Lao.
PUNYETOPapuch haziuziki mkuu. Watu wamevurugwa
😂😂😂😂 aaah kumbe you type from 🇺🇸 🇺🇸 mzee nilisahau bora ubaki huko huko basi nikwambie huku Tz kampuni au kazi nyingi za Sales kwenye makampuni ni za kijanjajanja kama hivyo na training ndio munafundishwa hivyo Tz kazi za Sales ndio imekuwa Kimbolton la haraka strategies zake ndio kama hivyo.Kumwambia mtu kwamba aje huku ashinde zawadi kama ni mteja wa muda mrefu bila kumwambia kwamba kuna hela inatakiwa kuipata hiyo zawadi ni aina fulani ya utapeli.
Yani hata kama si kumtapeli mtu moja kwa moja, unaanza kumvuta mtu kwa kutumia false advertisement.
Yani kama mtu ana shughuli zake anawahi, halafu anajikuta kapoteza dakika kumi akifikiri anashinda zawadi ya T-Shirt bure kwa kuwa mteja wa siku nyingi tu, akajikuta kabadilishiwa kibao anunue simu, ambayo hata haihitaji, huo ni utapeli.
Wangemwambia tangu mwanzo mpango wote.
1. Wanatumia udhaifu (take advantage) kwamba wanaume wengi huwa ni "dhaifu" mbele ya mwanamke.Kumwambia mtu kwamba aje huku ashinde zawadi kama ni mteja wa muda mrefu bila kumwambia kwamba kuna hela inatakiwa kuipata hiyo zawadi ni aina fulani ya utapeli.
Yani hata kama si kumtapeli mtu moja kwa moja, unaanza kumvuta mtu kwa kutumia false advertisement.
Yani kama mtu ana shughuli zake anawahi, halafu anajikuta kapoteza dakika kumi akifikiri anashinda zawadi ya T-Shirt bure kwa kuwa mteja wa siku nyingi tu, akajikuta kabadilishiwa kibao anunue simu, ambayo hata haihitaji, huo ni utapeli.
Wangemwambia tangu mwanzo mpango wote.
Basi sio hao kuna wwngine wanakaa pale round about ya sanamu la staring kwenye miti na gari sina hakika kama matapeli au sio ila ni wanauza simu mimi naamini ni their out door selling strategies tu so siwezi amini matapeli coz wajanitapeli.Any ways unaweza kuwa sahihi siwezi kukupinga moja Kwa Moja,nilikutana nao baada ya ile sheli ya posta mpya ukitokea crdb bank
Ila lolote lawezekana chief
UshahidiMatapeli hao walikuwaga Mbagala Rangi 3
Mkuu,😂😂😂😂 aaah kumbe you type from 🇺🇸 🇺🇸 mzee nilisahau bora ubaki huko huko basi nikwambie huku Tz kampuni au kazi nyingi za Sales kwenye makampuni ni za kijanjajanja kama hivyo na training ndio munafundishwa hivyo Tz kazi za Sales ndio imekuwa Kimbolton la haraka strategies zake ndio kama hivyo.
Kwa hiyo unataka kutuaminisha vinginevyo? Na ww tutakutaka ulete Ushahidi.Ushahidi
Nishawakuta hapo posta Benjamin Mkapa, nikamwambia nimetoka nyumbani na mambo mengine hiyo habari kununua simu Sina ratiba hiyo ,ving'ang'anizi nikawambia kesho.Jijini dar es Salaam maeneo ya posta mpya, ilikuwa siku ya ijumaa mwamba naelekea zangu msikiti wa Ngazija kwa ajili ya kuswali swala ya ijumaa.
Nikiwa nakatisha pembezoni mwa maduka mara pap madam mmoja huyu hapa, "kaka shikamoo" nikamuitikia marahaba, akaendelea "tuna zawadi za fulana kwa watu ambao wametumia mitandao ya simu kwa mda mrefu".
Akataja mitandao husika sitaitaja hapa sitaki kuwapa promo, akaniambia nisogee kwenye gari nipewe zawadi yangu, anyways nikaona isiwe tabu ingawa nilisita kidogo lkn nikasema ngoja nifuate nyuki nile asali.
Nakutana na madam mwengine ananiambia hapa tunapromotion kwa wateja wa mda mrefu, ndani ya gari kuna madam mwengine ana daftari nikaulizwa jina langu nikawatajia pamoja na namba yangu ya simu.
Huyu wa nje akatoa kikadi nichague karatasi moja nipate zawadi, nikachagua,kufungua akasema waoo! Umejishindia simu, akaleta box kweli kufungua simu rununu mpya.
Nikajisemea moyoni yaan mtu unashinda simu kirahisi tu hivi hivi, akaniambia kaka sasa hii simu ni laki nne na nusu ila kwasababu ya promotion utaipata kwa laki na ishirini, nikamwambia madam sina ratiba za kununua simu istoshe hapa sina bajeti hiyo.
Madam akasema unaweza weka deposit hata ya elfu hamsini halafu ukakomboa siku nyingine, nikamwambia sina hiyo hela hapa, madam akasisitiza waeza weka hata elfu tano tu! Duh nikajiuliza hii imekaaje yaan simu ya laki nne mpaka unaweza weka deposit buku tano?
Nikamwambia nayo sina, nikageuka na kusepa zangu, hatua tano toka nitoke pale ebwana eeeh nikasikia Bonge la Msonyo hahah,,, unajua nini wameshindwa kunitapeli kwahiyo wakamind, wala sikugeuka nyuma nikajisemea moyoni imekula kwenu.
Jamani walisema wadau mjini ni shule kwahiyo hakikisha mda wote unavaa unifomu madaftari utayakuta huko huko.
Ni hayo tu!