Kuna dem alitapeliwa mwisho wa mwaka jana ,alitoka bank akakutana na jamaa nje ya bank..jamaa kamsalimia afu dem akaitikia ndio ikawa nitolee hiyo, yaani dem akajikuta anamfuata jamaa hadi kwenye gari. Wakaingia dem wakamkalisha siti ya nyuma katikati,pembeni kuna watu wawili. Wakaenda hadi karibu bagamoyo wakamshusha. Dem akabaki kazubaa zaidi ya lisaa, hadi konda wa daladala alipomuuliza vp unaenda ndio akashtuka na kuanza kupiga wayowe. Watu wakajaa dem akazimia..peleka hospital akazinduka kesho yake..simu hana,pochi hana.... bahati nzuri kuna namba ya dadaake anayokichwani ndo kupigiwa wakaja mchukua. Dem aliumwa balaa akawa kama anamapepo...hadi kumletea shehe ndo hali ikaanza badilika kupata nafuu. Miez mitatu ndo dem kaanza kurudi kawaida ila bado anapata ganzi miguuni hadi sasa.