Nikifa miradi hii nani ataiendeleza: Hayupo, na nchi inasonga na miradi kedekede

Nikifa miradi hii nani ataiendeleza: Hayupo, na nchi inasonga na miradi kedekede

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Nimekumbushia kauli hii tukielekea kwenye maadhimisho.

Ni kauli inayoweza kutolewa na mtu ambaye haamini taasisi, aliamini yeye ni zaidi ya taasisi na zaidi ya Kila mtu, Mungu alivyo fundi, miradi inaendelea, tena anayeendeleza mwanamama.
 
Ila jamaa alitupeleka mchaka mchaka wa hatari, dah noma sana!!! Amani ilitoweka si mtaani wala kwenye mitandao ya kijamii!!! Mtaani tunaogopana!!! Trafiki na TRA waliwaka moto aisee!!! Watu hatujui kesho tunaamka na mwelekeo gani na taifa letu!!!

Viherehere wa JF kina GENTAMYCINE na Erythrocyte na sisi wengine tulikuwa tunawindwa kama swala!!! Una log in ukiwa chooni hata unaelala nae humuamini kwenye username ya JF!!! Ilikua kasheshe na nusu!!! Full mtanange!!!

Zero IQ huyu mwamba alikua anatupoza roho na nyuzi zake za kuwala wake za watu kwenye kibanda chake cha chips!!![emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hizo taasisi zilikuwepo aliyoyafanya mbona hawakua wameyafanya ama hizo taasisi zimefanya hadi yeye alipoamua kufanya.

Hizo taasisi hazikua zinaona kama hii nchi inahitaji reli ya SGR? Hizo taasisi hazikua zinaona kama hii nchi inahitaji umeme wa kutosha wa uhakika badala ya umeme wa kutapeli wa kina IPTL, Singas, Agreko nk, hazikua zinaona?

Faida ni kwamba amekufa ameacha hiyo miradi katika hali ambayo haiwezi kuacha kumaliziwa, hakuna.

Upinde wa mvua Mtapiga kelele weee lakini Magufuli atakumbukwa vizazi na vizazi kwa mambo makubwa aliyoifanyia hii nchi.
 
Nimekumbushia kauli hii tukielekea kwenye maadhimisho.

Ni kauli inayoweza kutolewa na mtu ambaye haamini taasisi, aliamini yeye ni zaidi ya taasisi na zaidi ya Kila mtu, Mungu alivyo fundi, miradi inaendelea, tena anayeendeleza mwanamama
Hivi kweli ina endelea! Kusema ukweli, ulizia watu, wengi watakwambia kwamba hatuna habari yoyote kwamba miradi inaendelea. Maana kwa miaka sita ya awamu ya tano, tulizoeshwa kila hatua ya mradi tulijulishwa : kipande cha reli (SGR) kutoka Dar - Moro, bwana MwanaNtara alikuwa anatueleza imefika wapi na nani wametembelea mradi na % ngapi zimeisha kwisha.
Vilevile kwa miradi mingine na shughuli zote. Kila mtanzania hata umwamshe usingizini alikuwa anajua kila mradi unaotekelezwa nchini na umefika wapi..
Wewe leo umesema miradi inaendelea! Je! Ulijuaje? Maana sisi hatujajulishwa!
Halafu Sentensi yako ya mwisho umesema - "halafu inaendelea na mwana mama"! Una maana gani? - kama hujui pia kumbuka hii ni wiki ya wanawake duniani, unadhubutuje kumaliza na Sentensi hiyo au kuwa na fikra kama hizo?
 
Nimekumbushia kauli hii tukielekea kwenye maadhimisho.

Ni kauli inayoweza kutolewa na mtu ambaye haamini taasisi, aliamini yeye ni zaidi ya taasisi na zaidi ya Kila mtu, Mungu alivyo fundi, miradi inaendelea, tena anayeendeleza mwanamama
JPM alikuwa na akili kubwa sana hata mtukane. Katika ujenzi wa SGR alianza Dar - Moro kisha Moro- Makutupora. Kisha akaruka kwenda kuanza Isaka - Mwanza ili kumlazimisha successor wake kuunga Makutupora - Isaka. Vinginevyo watu wangesema tuishie Makutupora tujenge bandari kavu hapo.
 
Nimekumbushia kauli hii tukielekea kwenye maadhimisho.

Ni kauli inayoweza kutolewa na mtu ambaye haamini taasisi, aliamini yeye ni zaidi ya taasisi na zaidi ya Kila mtu, Mungu alivyo fundi, miradi inaendelea, tena anayeendeleza mwanamama
Alikuwa anawaaminisha huo utoto wajinga,alikufa Nyerere achilia mbali kung'atuka sembuse yule mihemko?
 
Back
Top Bottom