Nikiitafakari ile kauli ya Kusaga,bado sipati jibu....

Nikiitafakari ile kauli ya Kusaga,bado sipati jibu....

Kwamba "Sisi vijana tuache majivuno,kama ni pesa Ruge alikuwa nazo kuliko msanii yoyote yule. Kama ni umaarufu Ruge alikuwa maarufu kuliko msanii yoyote yule,Kibonde alikuwa na pesa kuliko msanii yoyote yule,lakini leo hii hawapo tena duniani,chuki,dharau,nyodo na majivuno hayana maana tumalize tofauti zetu dunia tunapita"....

Swali ninalojiuliza kwa nini hii kauli imetolewa wakati huu na sio wakati ule?
Mhubiri 3: 1-8
 
Hivyo vyombo najua anamiliki,lakini ulimsikia alichokiongea msiban,kazungumzia msamaha na watu wasamehane,akawambia watu pale makaburini wapeane mikono na moja ya wa maadui zake ni Jidei.Haiwezekani wewe uhubiri msamaha na kupendana,wakati wewe huishi kile ulichokizungumza,mwisho wa siku utakuwa MNAFIKI.

Msikilize Kusaga vizuri.

Uadui wa Kusaga na Jide ni kwa sababu gani
 
Hajamlenga mtu yoyote ni maneno ya kawaida tu hasa unapokuwa umepoteza watu muhimu kwako. Maneno mazuri ya kukumbushana tu yote tunayofanya yana mwisho na kuwa umaarufu au pesa ndio itakusaidia maana kuna watu mabilionea lakini walifia Hospitalini huku wakipewa matibabu bora kabisa. Kina Steve Jobs alisema haya wakati akiwa hana muda wa kuishi tena. Na hili sio funzo kwa matajiri tu hata sisi maskini unaweza kuwa maskini lakini wewe kuudhi watu kuumiza watu na hizi nasaha ukihudhuria misiba yote tunakumbushwa lakini sisi binadamu muda ukipita tunasahau kidogo na sehemu kama hizi vizuri kukumbushana. Hakuna mtu msafi ila tujitahidi kufanya mazuri. alichosema Kusaga ni kitu kinaongelewa sana tu katika misiba na hakuna sehemu nzuri ya kujitafakari zaidi ya kwenye mazishi.
 
Wapi nimeandika Aslay anapesa?au kuwa na Pesa na Umaarufu Ni kitu kimoja? uwe unasoma vizuri na kutafakari kabla ya kujibu.

La pili...wewe kuanza kumjua Ruge na Kibonde kabla ya Aslay ndo point unayotumia kutetea kuwa wao ni maarufu kuliko Aslay? Mbona wengi tumewajua kabla ya Diamond na siyo Maarufu kuliko yeye.
Unamuongelea huyu Aslay anayejulikana mpaka na watoto si mijini wala vijijini.
Stations za Uganda..Kenya...Burundi...Rwanda..Congo n.k wanacheza nyimbo za Aslay na unasema siyo maarufu?Kwahi muktadha upi?
Kibonde wanamjua Kenya au huyo Ruge kwa impact gani?watakuuliza ndo nani?
naona mlibishana sana, ni kwamba umaarufu ni swala pana sana, huyo boss wa Clouds alizungumzia umaarufu wa connection ndani na nje ya nchi sio umaarufu wa kujulikana tu mitaani
Ruge amekuwa na umaarufu wa connection kwenye biashara kabla ya wasanii wote na mpaka anakufa huenda alikuwa maarufu sana kwenye ulimwengu wa biashara kuliko wasanii wote hapa Tanzania
 
Back
Top Bottom