Nikilinganisha mapokezi ya Rais wa shirikisho la Ujerumani na Mfalme wa Uingereza, viongozi wetu hawajiamini. Tatizo ni nini?

Nikilinganisha mapokezi ya Rais wa shirikisho la Ujerumani na Mfalme wa Uingereza, viongozi wetu hawajiamini. Tatizo ni nini?

Mkuu,

Naomba niwe tofauti na hoja yako.

Unachopaswa kufahamu ni kuwa, kila kiongozi ana ratiba yake. Ratiba kamwe haiwezi kulingana, hivyo uharaka ama utaratibu hutegemea na ratiba. Mfano, Prince alipanga safari ya siku tatu huku Rais wa Umoja wa Ujerumani alipanga kukaa siku mbili. Nipo tayari kurekebishwa kwa idadi ya siku.

Maana yake ratiba ya Rais wa Ujerumani ipo very tight. Kuna mambo lazima yaende kwa haraka kidogo.

Lakini pia kutokana na ratiba, itifaki lazima nayo ibadilike.

Si hilo tu, kila kiongozi anapokuwa anatembelea ugenini anakuwa na lengo la ziara yake. Na lengo hilo huamua ratiba. Kama Rais wa Ujerumani alipanga kutembelea Songea, ambayo ipo mbali kidogo kutoka Dar.

Haiwezi kuwa ni swala la papo tu kuwa tumpeleke Rais ufukweni alafurahie upepo.

Kabla ya kuja, ilishawekwa kabisa kuwa atafika siku fulani ataenda sehemu fulani kisha atakutana na fulani muda fulani. Kisha atazungumza na vyombo vya habari, ksiha baadae kongamano la wafanyabiashara.

Atapata chakula cha jioni na fulani kisha atapumzika. Kesho atatembelea fukwe na baadae ataaga na kuondoka.

Wala usilaumu.
 
Back
Top Bottom