Nikiomba tena ajira niiteni mbwa nimekaa paleee

Mkuu sasa hivi soko la ajira ni gumu na tatizo la mliochagua kusomea ualimu wengi mlifuata wepesi wa mikopo na ajira. Mkikosa ndio hivyo mnakuwa frustrated

kaka huko mtaani kapambane tu ili uishi ila usijikatie tamaa kama ni kitu unachokipenda

kila mtu ana muda wake, wengine hawakai mtaani sana na wengine ndio hadi usote kama wewe, sasa trials chache ndio ujikatie tamaa.
 
Una moyo sana. Niliomba mara moja sijui ni 2016 sikumbuki vizuri. Sijawahi omba tena
Kama darasa la 7 na 4 wanaishi vizuri. Sisi wenye elimu tutashindwa kuishi?
 
Nilivyosoma heading nimecheka vibaya mno kama mazuri vile..
 
Kila la kheri mkuu pambana
 
Tatizo lako unataka serikali ndio ikuajiri, private school bado zinahitaji walimu, hadi wasiokuwa walimu kitaaluma wanafundisha private, wewe unaferi wapi?

Mimi nina ndugu yangu ni form six lakini ametoka familia ya kielimu anafundisha Biology kama yeye ndio ameitunga, jamaa kila shule anayokwenda anapewa uhead Master na darasani anafundisha na hajawahi kukanyaga sehemu inaitwa chuo kikuu, hana Degree wala Diploma.

Kuna shida sehemu kwenu vijana wa sasa hivi.
 
Nakuambia ndugu yangu pambana, hutakuja kuyajutia maamuzi haya ya kutoomba ajira kamwe!
Mwenyezi Mungu abariki kazi za mikono yako!
 
Unazijua private school wewe? Unajua wanavolipa? By the way mm nilikuwa naiongelea ajira ya serikali , wala sjalalamikia private kwa sababu nazijua in and out
Kufanya private ni bora tu kuwahi kwenda kujiajiri maana private nyingi wanakutumia ukishachoka wanakuacha vilevile unaenda tena kuanza moja,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…